CCM kimekuwa chama chenye milengo mbalimbali (rangi nyingi), na kwa maoni yangu hii ni sababu mojawapo inayofanya vyama vya upinzani wapate taabu sana kukikabiri barabara chama hiki na kukiondoa kwenye madaraka.
Ni hoja yangu kwamba, ni ndani ya CCM hiyo hiyo kwa kuwa na makundi mbalimbali, yenye milengo mbalimbali kiasi kwamba hivi vyama vya upinzani vilivyoko nje ya chama hicho, mahitaji yao (wenzao wenye milengo kama wao) tayari wamo ndani ya CCM.
Kwa hiyo, kwa chama kama CHADEMA, walipata taabu sana toka kwa kundi lililo upande wa Magufuli, huku wenzao waliomo ndani ya chama hicho, kutokana na muundo wa chama, hawakuweza kuinua kidole na kuwatetea CHADEMA.
Baada ya Magufuli kuondoka, kama alivyoondoka, na kundi lililokuwa limenyamaza likiwa upande wa akina Samia, sasa ndio wanaotawala anga. Kundi hili ni kundi lenye misimamo inayokubaliana karibu kwa kila kitu na CHADEMA, kasoro kuwaachia washike serikali. CHADEMA imejikuta haina wigo wa kumkabiri Samia, ambaye naye hatumii njia zilezile za kuwakandamiza kama alizotumia Magufuli.
Kwa hali hii, ni ajenda gani wanayoweza kuishika na kumkabiri nayo Samia? Ukandamizaji hakuna, Katiba Mpya, inazungumzika, Tume Huru, hili tutalifanyia kazi. Sasa CHADEMA imebaki na kitu gani kuwapelekea wananchi wawaunge mkono!
Mbowe kautazama ukweli huu, na kuamua kama alivyo amua ni nini chama chake kifanye.
Wakati huo huo, huko ndani ya CCM vikelele vya kundi la Magufuli linatafutiwa dawa. Kamati Kuu na Kamati mhimu zinasukwa upya kuondoa takataka za Magufuli huko. Hawa wanaopiga kelele pembeni, wakati wakiwa ndani ya chama, wengi wanatupiwa minofu, na wale ambao ni sugu kama akina Polex2, akina Bashiru, akina Kalamaganda wote wamekwishawekwa pembeni.
Hiyo ndiyo CCM, ambayo, kwa rangi zake mabalimbali na uwezo wa kujigeuza kila mara, imeapa" kutawala nchi hii milele"! Kweli?
Kama vyama vyote vya upinzani tayari wanayo makundi yao ndani ya CCM, yako wapi tena matumaini ya waTanzania?
Kwa mwendo huu huu, kuna siku tutajikuta akina Thomas Sankara wakiibuka bila ya kutegemewa. Hilo ndilo litakaloiondoa CCM na makundi yake yote, ndani na nje ya chama.
Sikuhariri chochote, naomba usinilaumu kwa makosa ya uandishi.