Unazuia sherehe za Uhuru, unaadhimisha birthday ya CCM

Unazuia sherehe za Uhuru, unaadhimisha birthday ya CCM

Naomba kuuliza
(1) Hilo lilikuwa kusanyiko la kichama au la kiserikali?

(2) Kama lilikuwa la kichama ina maana ilikuwa ni shuguri ya kisiasa inafanyika.Je ni lini makusanyiko ya kisiasa yaliruhusiwa? Nakumbuka yalipigwa marufuku mapema kabisa na serikali.
 
Chama ndicho kimeiweka serikali madarakani na sio kinyume chake. Serikali inatekeleza ilani ya chama. Rais Magufuli anachopinga ni matumizi yasiyo na ulazima, mbwembwe na kula bata pasipo sababu za msingi. Unaweza ukaadhimisha miaka 39 ya uhai wa chama bila ya matumizi makubwa. Nadhani ndicho kilichofanyika. Hakuna rais wa Tanzania aliyewahi kukizua chama kutoadhimisha kumbukumbu za uhai wake.
 
Mbona gari nyingi tu za serikali tunapishana nazo j2 ilihali si siku za kazi na hazitumiki kiofisi?
Ni utaratibu usio sawa. Lakini umehalalishwa na serikali za CCM. Magari ya serikali kutumika katika shughuli binafsi haswa kwa viongozi waandamizi (mawaziri, wakuu wa wilaya na mkoa, DEDs, DASs, RASs, makatibu wakuu, wakurugenzi, makamishina, majaji n.k) ni matumizi mabaya ya mali za umma.

Siwezi kuongelea juu ya viongozi wakuu wa dola: Rais, Spika, Jaji Mkuu na Waziri Mkuu. Hawa wanastahili hiyo 'favour' ingawa ni vyema nao kuongozwa na sheria za namna ya kutumia mali za umma kwa mambo binafsi. Hapa mambo binafsi hayuhusiana na wao kuhudhuria sherehe za chama. Hili si sawa. Lakini wengine wote hawastahili kutumia mali za umma kwa matumizi binafsi.

Watu wa CCM uwa wanapenda sana kutoa mifano ya nchi zingine pale wanapohalalisha jambo lililo upande wao. Lakini ung'aka pale watu wanapotoa mifano ya nchi zingine kwa mambo wasiyoyataka. Utawasikia, "kila nchi inaamua mambo yake". Kwenye hili la matumizi ya mali za umma, serikali ya CCM ijifunze kwa nchi nyingine kama, Uingereza, Uswisi na nchi za Scandanavia.

NB: si Magufuli alisema ataachana na 'mashangingi'? Mbona bado yanatawala fleet ya serikali?!
 

319b4d1ad7167c432b6056c4b7d1dc90.jpg
 
Birthday ya ccm ni tukio la kichama kwa hiyo gharama ni za ccm. Raisi popote aendapo lazima atumie gharama za serikali hata akienda church lazima awe na ulinzi na gari ya ikulu pia atatumia.
Great. But, was it necessary for Rais to be physically at the celebrations?!? He could have stayed in Dar and 'attended' and made the speech via video conferencing. And that could have proved that he means it when preaching about austerity.
 
Watu wengine akili fupi. Lakini umeuliza ili ufahamu. Sheri za maadhimisho ya kuzaliwa CCM ni ya kichama haihusiani na serikali.
 
Chama ndicho kimeiweka serikali madarakani na sio kinyume chake. Serikali inatekeleza ilani ya chama. Rais Magufuli anachopinga ni matumizi yasiyo na ulazima, mbwembwe na kula bata pasipo sababu za msingi. Unaweza ukaadhimisha miaka 39 ya uhai wa chama bila ya matumizi makubwa. Nadhani ndicho kilichofanyika. Hakuna rais wa Tanzania aliyewahi kukizua chama kutoadhimisha kumbukumbu za uhai wake.
Kwa kutumia rasilimali za watanzania?
 
Darn us Tanzanians!!

Rais Magufuli ni mwanachama hai wa CCM. Na ndio mwanachama muhimu kwa chama kwa sasa kwa kuwa ndio Rais wa nchi! Uwepo wake pale husingekwepeka. CCM ni zaidi ya chama cha siasa!! Ndio maana wengine tunatumia muda wetu mwingi sana kupiga kelele kwa viongozi wengine wa vyama vya Siasa vya upinzania (hasa CHADEMA) kujijenga na kujitegemea hasa katika mapato ili angalau wawe sawa na adui wanaepigana nae!

Kufanya maadhimisho ya kitu Fulani kwa binaadam ni zaidi tu ya kumbukumbu, ikija kwenye chama cha siasa ni muhimu zaidi maana hiyo njia ni rahisi sana katika kuwaweka wanachama karibu na kujenga mshikamano halisi (kumbukeni kampeni za CDM 2015 ule umoja uliokuwepo mitaani mpaka mitandaoni haukutakiwa kuisha wala kupungua!!) lakini hawa jamaa wa CCM wapo ever since na watazidi kuwepo (wapo hata sasa).

Wanachama wa CCM ukifuatilia kiukaribu utagundua karibia 70% wanafahamiana (kutokana na Matukio yao ya kichama kila mwaka na almost kila mkoa bara na visiwani) lakini ukija kwa vyama vingine vya Siasa wanachama wengi hawafahamiani, hakuna solidarity ya ALL DAY EVERY DAY ALL YEAR FOR A LIFE TIME, vyama vingi vinasubiri kampeni au Matukio (ya kitaifa) kutokeza kwa u karibu zaidi na wanachama/wananchi!! This has to change!!!

CCM ina vyanzo vya mapato vingi sana lakini pia resource yao kubwa ni hazina ya wanachama walionao ambao wako radhi wale ugali tembele ili tu wapeleke michango yao katika chama Chao (wafia chama), ila pia ina wanachama ambao ni wafanyabiashara wakubwa sana ambao kwa kiasi kikubwa wanakisaidia chama katika mambo mengi (hasa Matukio ya kichama).

Some people may say "if you can not beat them join them" but in the current world that we live in kila mmoja wants to be at the top na the only way to do that now is "if you can not beat them just OUTSMART them", wakati wa siasa za kishabiki umepita sasa wote hapa (CCM, CDA, NCCR, ACT, CHAUMA, WASIOKUWA NA VYAMA, n.k) ni Watanzania wenye kutamani kuishi a decent life (a life of clean water, full time power supply, quality education, great infrastructure, superb health care n.k) inabidi tubadilike sasa na kufanya Siasa za kujenga (constructive politics) sio kubomoa!

**Sio kila criticism iko poa kiivyo!

Na wale mnaotaka kutumia ajali na vifo vya Askari wetu please please I beg you people kujifikiria mara mbili nini maana ya AJALI!
R. I. P kwa walinzi muhimu wa Taifa letu.
 
Kwa kutumia rasilimali za watanzania?
Rasilimali za watanzania milioni 8 waliopatia ridhaa za CCM na wengine wengi tu ambao hawakupiga kura kwa sababu mbalimbali lakini wanaukubali uwezo wa CCM. Sio dhambi, na CHADEMA hamjakatazwa kufanya birthday yenu, na pesa mnazo kwani mnao wafanyabiashara wengi tu.
 
Swala linakuja chama kilichopo madarakani ndicho pia kinadhamana ya kuunda serikali... kwa hiyo kinaweza kutumia rasimali za serikali endapo itahitajika hivyo kwenye shughuli za kichama ila kwa gharama za chama... na hata kwa kibali...
Kwa kuwa serikali inategemea kodi kutoka kwa wananchi wote (wanachama wa CCM, wanachama wa vyama vingine na wananchi wasio wanachama wa vyama vyovyote), huoni kuwa si sawa kwa CCM kutumia fedha zitokanazo na kodi hizo kwa manufaa ya chama??? Huu si ufisadi? Na je, kunakuwepo na usawa wa kidemokrasia?!? Kwa sababu vyama vingine haviwezi kutumia mali za umma kwa manufaa yao!
 
Kwa kuwa serikali inategemea kodi kutoka kwa wananchi wote (wanachama wa CCM, wanachama wa vyama vingine na wananchi wasio wanachama wa vyama vyovyote), huoni kuwa si sawa kwa CCM kutumia fedha zitokanazo na kodi hizo kwa manufaa ya chama??? Huu si ufisadi? Na je, kunakuwepo na usawa wa kidemokrasia?!? Kwa sababu vyama vingine haviwezi kutumia mali za umma kwa manufaa yao!
Ni shughuli ya kichama... pesa zinazotumika ni za kutoka kwenye mfuko wa chama... vifaa vinaweza kuwa vya serikali..
 
Rasilimali za watanzania milioni 8 waliopatia ridhaa za CCM na wengine wengi tu ambao hawakupiga kura kwa sababu mbalimbali lakini wanaukubali uwezo wa CCM. Sio dhambi, na CHADEMA hamjakatazwa kufanya birthday yenu, na pesa mnazo kwani mnao wafanyabiashara wengi tu.
Tutatumia rasilimali za wapiga kura milioni 10 waliotupa ridhaa lkn mkatunyang'anya
 
Tutatumia rasilimali za wapiga kura milioni 10 waliotupa ridhaa lkn mkatunyang'anya
Hao milioni 10 waliwapigia kura ni kwa mujibu wa tume yenu pori ya uchaguzi ambayo wajumbe wake walikamatwa wakati uchaguzi ukiendelea. Mliitaka sana nchi kwa udi na uvumba mpaka mkawa tayari kutumia mbinu chafu, lakini mkasahau kuwa CCM inazijua mbinu za kistaarabu na hata zile za chini kwa chini. Jipangeni upya, tafuteni mgombea urais kijana aanze mchakato wa kutafuta majimbo mengi zaidi ili mwaka 2020 angalau muweze kuongeza majimbo. Kinyume cha hapo mtaendelea kusubiri sana, na kama alivyosema mbunge Lusinde, chama kikishindwa uchaguzi mara tatu mfululizo kinageuka kuwa cha kigaidi.
 
Wanabodi
Salaam;

Serikali ya awamu ya 5 inajinasibu kubana matumizi na kufuta baadhi ya sherehe za kitaifa kwa lengo hilo la kuzuia matumizi yasiyo ya lazima.

Kichekesho kimeonekana leo baada ya serikali nzima kuhamia singinda kwenye sherehe za birthday ya ccm ya kutimiza miaka 39.

Huko nyuma tulishuhudia sherehe za uhuru zikipigwa kumbo,sherehe za wabunge zikapigwa ban,baadae tbc nayo ikapigwa ban kwa lengo hilo hilo la kubana matumizi. Cha kushangaza Rais na serikali nzima walikuwa kwenye birthday hiyo ya ccm kwa ajili ya kutoa hotuba za mipasho!!

Kweli hii nchi ngumu sana aisee!

Mi nasemaga kama kweli zile kura mil 8+ walizipata kihalali basi nchi hii bado ina wajinga na mazezeta mil 8+
 
Ni shughuli ya kichama... pesa zinazotumika ni za kutoka kwenye mfuko wa chama... vifaa vinaweza kuwa vya serikali..
Can you prove that?!? Yaani magari ya viongozi wa serikali, polisi, hata ya viongozi wastaafu yaliwekewa mafuta na CCM? Na walinzi na security details wa viongozi walilipwa na CCM?
 
na kama alivyosema mbunge Lusinde, chama kikishindwa uchaguzi mara tatu mfululizo kinageuka kuwa cha kigaidi.
Hivi huyo jamaa alisema hivyo kwa hisia tu ama kuna nadharia katika sayansi ya siasa inayosema hivyo? Kama ipo unaweza kunitajia ili nijifunze.
 
Ni zipi hizo pesa za chama kwakuwa kabla ya uchaguzi akaunti zake nyingi zilikuwa hoi bin taaban
Hiyo ilipelekea wafanyakazi wa idara zao mbalimbali kugoma kuendelea kutumikishwa kwa ujanja ujanja bila kulipwa,sasa wanasema ni ela za chama
 
You mean unasema kuwa chadema, ACT, Nccr, Tadea, Chaumma wakitaka kufanya sherehe zao magufuli aingilie??

Sherehe za CCM sio za kitaifa, sherehe ya uhuru ni ya kitaifa

sherehe ya ccm ni ya kichama, ya uhuru ni ya serikali

acha upuuzi
Kweeeli kabisaaa lkn tunapoteza nguvu nyingi kujibishana humu kwani wengine aidha hawaelewi au ni wabishi tu ka kabila fulani hivi
...
 
Back
Top Bottom