Unazikumbuka enzi hizi? Hakika hazitarudia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unazikumbuka enzi hizi? Hakika hazitarudia!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by babukijana, May 22, 2010.

 1. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,818
  Likes Received: 1,166
  Trophy Points: 280
  yondosisiter.jpg
  AurlusMabele1_.jpg HAKIKA maisha ni safari ndefu, mara nyingine mtu unalazimika kukubali kuwa watu tunatoka mbali nikiwa na maana kuwa mpaka unakuja kuupata utu uzima unakuwa ulishafanya mambo kibao, mazuri kwa mabaya na pia mema na ya hatari du! Kweli acheni Mungu aitwe Mungu.

  Lakini leo siandiki makala haya kwa lengo la kukutisha ama kukufanya ulie kwa machungu , bali unaweza kudondosha chozi dogo la kishikaji kwa furaha kama ulikuwa mdau wa kweli wa burudani.

  Miaka ya 80 hadi miaka ya 90 mpaka 93 ni kipindi ambacho kilikuwa kimechangamka zaidi kiburudani kwani wakati huo ndiyo kilikuwa kinatawala kizazi kipya cha muziki wa Soukouss kutoka huko nchini Zaire (sasa Congo DR) hasa baaada ya kumalizika kwa enzi za akina Luambo Luanzo Makiadi (Franco).

  Kabla ya kwenda mbali hebu ngoja nikukumbushe miaka ya karibuni, wanjanja wengi kipindi hicho tulikuwa tunakutana pande za Kinondoni kwenye kiwanja kimoja kilichokuwa na jina la Tazara Hostel.

  Hapo ‘baba' kulikuwa kunapigwa ngoma na bolingo za kufa mtu hakuna kulala mpaka kunakucha ni mwendo wa ‘Soukouss' kwa kwenda mbele chini ya DJ maarufu ‘Le Generali' Charles Mhamiji.
  Lakini leo hii maeneo hayo yako kimyaa! hakuna bolingo wala disco watu wanapiga usingizi tu kwenye majengo hayo baada ya kubadilishwa na kuwa Hostel.[​IMG]

  Hapo nadhani nimekugusa kidogo, sasa mpango mzima uko hivi, kwa wewe uliyependa burudani ya muziki wa Kiafrika hasahasa kutoka pande hizo za Zaire nadhani unakumbuka enzi hiyo ambayo tulikuwa tunaalikana kwa maneno ya "Ebwana leo vipi hatuendi Buggy" halafu utasikia mtu anajibu "wewe tusiende nani kasema" na hatimaye mida fulani ya jioni tunajisogea pande hizo za Tazara Hostel kusongesha Buggy lenyewe.

  Hakika ilikuwa utamu kolea lakini sasa burudani hiyo haipo tena hapa bongo kilichopo ni mlolongo wa shoo za wana bongo fleva huku bendi zinazopiga muziki staili hiyo kama Akudo na FM Academia taratibu zinaanza kukosa wadau.

  Sina hakika sana pengine hii inachangiwa na nini. Labda kupanda kwa gharama za maisha, au kukosekana kwa wanamuziki nyota kama waliokuwepo enzi hizo.

  Kila mpenda 'Buggy' anakumbuka ngoma kali zilizokuwa zinapigwa na wakali kutoka kundi la Loketo Group, hivi ni nani aliyekaa kwenye kiti wakati ngoma kama 'Evelina' ama 'Huke loketo' zikiwa hewani chini ya DJ Charles mhamiji.

  Utamu wa sauti kutoka kwa Lucian Bokilo na utundu wa kucharaza gitaa wa Dally Kimoko ulitosha kabisa kuwapagawisha watu mpaka wanasahau kama kuna kesho.

  Lakini leo hii hakuna vitu adimu ama hivyo baba, zaidi ya kusikia ‘yoyoo' na pedeshee fulani halafu muziki wenyewe umedoodaa da! Hii inaniuma sasa nani leo anaweza kutufuta chozi la kukosa vitu hivyo adimu.

  Hebu kumbuka hii wakati unendelea kuburudika na Loketo ya Aurus Mabele iliyokuwa inanogeshwa na akina Lokasa ya Mbongo, ghafla anapandishwa hewani 'Mzee Benz' Bozi Boziana, na kwa mbaali unaisika sauti ya mwanadada Scola Miel wakilisukuma Nzawisa, mama Nzawisa, jamani ilikuwa ni nusu kupata uchizi.

  Wakati unapagwa na ngoma za ‘Soukouss' hapo hapo kichwani kuna Pilsner kama saba hivi wewee mama wacha!!! lakini bia hiyo leo haipo tena baba du !!!!!!!!!!!

  Kali zaidi mida fulani ya saa nane nane wakati watu mshaanza kuchoka anapandishwa hewani "Mzee wa Fujo" Alan Kounkou hapo hata waliojificha kwenye kona wanaibuka na baada ya sekunde kadhaa Jean Baron anaingia na songi lake 'Mami lolo' du! Hakika ni balaa kutoka unataka, kubaki unataka, basi unajikuta upo kati ukiendelea kusukuma Buggy mpaka busheee.

  Wajanja wengi tulikuwa tunajua kuwa ukiona ngoma zinapungua kasi na kuanza kupigwa za akina Solomon 'Rama rama' au 'Double Double' ya Nyboma ujue asubuhi iko karibu basi hapo tunaitana na kukata maji ya mwisho mwisho na kuchukua totoz zetu halafu haooooo ‘mahome'

  Barabarani tunakutana na ndata (Polisi) kibao wakiwa wanajiwahisha sehemu zao za kazi lakini kwa kuwa tuko matingas (ulevi kupindukia) tunaanchana nao.

  Halafu kesho yake Jumapili haooo tunaenda zetu uwanja wa Taifa, kucheki bonge la mechi la watoto wa mjini Nyota Nyekundu na Sigara. Upo hapo? Na wikiendi inakuwa imekamilika SAAAAAAFI.

  Jamani nimeandika hii kukumbukia enzi kidogo, kwani leo hii mambo hayo hakuna tena!! Najua sijataja kila kitu lakini Mungu awalaze pema marehemu Kabasele Yampanya 'Pepe Kale' Madilu Systeme na wengine kwani ngoma zao zilitupagawisha mno enzi hizo.

  Kwa mengi zaidi usikose kutembelea www.dismas10.blogspot.com

  source:global.
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  safi sana kwa ninyi wazee
   
 3. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,818
  Likes Received: 1,166
  Trophy Points: 280
  sio uzee mkuu 90´s hapo we ulikua unanyonya?
   
 4. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  poa sana, zamani kulikuwa ni kutamu kuliko leo, halafu leo hii na gonjwa lisilo na tiba lipo.
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ukimwi umeharibu kabisa ladha unafanya huku na mawazo kibao
   
 6. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,818
  Likes Received: 1,166
  Trophy Points: 280
  he he hee,acha au kamua tu bila mawazo,kifo baadae
   
 7. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  kuna wale kina Robin, Sade, Tracy Chapman, Karyn White n.k
   
 12. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  senki yuu shem Bala najua leo Babukijana kakufikisha mahali pake....utakumbusha mambo mengi kwenye hii nyanja ya burudani
   
 14. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Karibu...........BabuKijana mchokozi sana aisee
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Bala, you just made my day! Umenirudisha nyuma karibu miaka 20! Hebu nambie, unatumia kinywaji gani vile...! I owe you quite alot man!
   
 16. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,818
  Likes Received: 1,166
  Trophy Points: 280
  he he hhheeee,mkuu vipi hatuonani bana toka jukwaa jipya lianze tunapoteana sana.upo lakini?naikumbuka thread yako ya enzi zileee
   
 17. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,818
  Likes Received: 1,166
  Trophy Points: 280

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,818
  Likes Received: 1,166
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,818
  Likes Received: 1,166
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...