Lokii
JF-Expert Member
- Sep 23, 2016
- 709
- 2,084
Amani iwe kwenu wanabodi, Ni zaidi ya mwaka sasa natumia haya maharage wengine wanayaita fiwi.
Mwanzo nililetewa na rafiki yangu huwa anayatumia mda mrefu akanishauri na mimi nianze kuyatumia kwa kuwa yana faida sana kiafya na pia yana virutubisho vingi zaidi.
Sikuwahi kuzingatia faida yake zaidi kiafya mpaka siku nilipo google benefits zake na ndio ikawa mwanzo wa kuyatumia zaidi.
Kama utaamua ku google kwa kiingereza yanaitwa black turtle beans.
Nawaza kama watanzania tulio wengi tunafahamu faida za fiwi kiafya maana siyaoni sana mitaani yakitumika, rafiki yangu anayenileteaga huwa anayanunulia maeneo ya hedaru nahisi ndio yanalimwa zaidi sehemu hizo sifahamu sana.
Kuna jamaa yangu mkenya nilimuonyesha akaniambia kenya yapo sana sometimes yanatumika mpaka kutengenezea githeri (makande).
Kwa uchache faida za fiwi kiafya;
Kiufupi naona haya ndio maharage yenye faida zaidi kiafya kuliko haya tunayokula sijui maharage mekundu au soya lakini nashidwa kuelewa kwanini hizi fiwi hazipatikani mitaani ama labda bado hatujaelewa umuhimu wake.
Wangapi mmeshawahi kula fiwi na mnadhani ni kwanini hayapo kwa wingi mitaani?
Natamani kufahamu pia fiwi zinalimwa maeneo gani mengine hapa tanzania. Hii inaweza ikawa ni fursa iliyojificha kwa wakulima na wafanyabiashara. Nawakilisha.

- Hupunguza sumu mwilini
- Zina protini nyingi zaidi
- Huzuia matatizo ya moyo
- Huzuia matatizo ya cancer
- Zina faiba nyingi zaidi
- Zinasaidia mmeng'enyo wa chakula
- Zinaimarisha mfumo wa neva
- Zinazuia ugumba kwa wanaume