Unazifahamu fiwi? Umeshawahi kuzitumia?

Unazifahamu fiwi? Umeshawahi kuzitumia?

View attachment 2224565
Yanapatikana Arusha na Meru huko

Mnaweza google for more info… ila ni mazuri sana
Nimesoma mkuu yanasifika kweli ni mazuri nimeona blogs nyingi zinasema yanaongeza nguvu za kiume.

Haya maharange mbegu zake zimezalishwa hapa hapa nchini na chuo cha uyole huko mbeya chini ya TARI kwa kuongezewa virutubisho zaidi, kuhimili ukame na kukomaa mda mfupi.

Nikitofautisha na fiwi naona kama fiwi ni organic na pia sio gmo, so naona kama fiwi ndo maharage ya asili yaliyobakia
 
Ni kama unataka kufanya biashara kijanja janja hivi. Unaweza kutuhakikishia kitalaamu hizo faida za kiafya ulizotuorodheshea hapo? au basi sema "nasikia" kwamba fiwi zinasaidia .....
Biashara ya hizi fiwi inaonekana ipo huko kenya zaidi, mi nataka tuzitumie wenyewe kama tunazilima lakini inaonekana wakenya wanajua zaidi umuhimu wake ndo mana wanazishambulia
 
Nawezaje kupata haya maharage. Mkuu
Mkuu; hayo sio maharage ni Fiwi almaaruf kama Ngwara. Ukizitaka ni mawasiliano na mipango tu. Ieleweke mm sio mfanyabiashara ila naweza kukutafutia BURE kiasi kidogo tu ukaoteshe kwako. 🙏
 
Amani iwe kwenu wanabodi, Ni zaidi ya mwaka sasa natumia haya maharage wengine wanayaita fiwi.

Mwanzo nililetewa na rafiki yangu huwa anayatumia mda mrefu akanishauri na mimi nianze kuyatumia kwa kuwa yana faida sana kiafya na pia yana virutubisho vingi zaidi.

Sikuwahi kuzingatia faida yake zaidi kiafya mpaka siku nilipo google benefits zake na ndio ikawa mwanzo wa kuyatumia zaidi.

Kama utaamua ku google kwa kiingereza yanaitwa black turtle beans.
Nawaza kama watanzania tulio wengi tunafahamu faida za fiwi kiafya maana siyaoni sana mitaani yakitumika, rafiki yangu anayenileteaga huwa anayanunulia maeneo ya hedaru nahisi ndio yanalimwa zaidi sehemu hizo sifahamu sana.

Kuna jamaa yangu mkenya nilimuonyesha akaniambia kenya yapo sana sometimes yanatumika mpaka kutengenezea githeri (makande).

Kwa uchache faida za fiwi kiafya;

  • Hupunguza sumu mwilini
  • Zina protini nyingi zaidi
  • Huzuia matatizo ya moyo
  • Huzuia matatizo ya cancer
  • Zina faiba nyingi zaidi
  • Zinasaidia mmeng'enyo wa chakula
  • Zinaimarisha mfumo wa neva
  • Zinazuia ugumba kwa wanaume

Kiufupi naona haya ndio maharage yenye faida zaidi kiafya kuliko haya tunayokula sijui maharage mekundu au soya lakini nashidwa kuelewa kwanini hizi fiwi hazipatikani mitaani ama labda bado hatujaelewa umuhimu wake.

Wangapi mmeshawahi kula fiwi na mnadhani ni kwanini hayapo kwa wingi mitaani?

Natamani kufahamu pia fiwi zinalimwa maeneo gani mengine hapa tanzania. Hii inaweza ikawa ni fursa iliyojificha kwa wakulima na wafanyabiashara. Nawakilisha.

View attachment 2222822
🤣🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Nchi ngumu hii. Ni Tanzania pekee ambayo raia wake wanaishi na sumu mwilini na mara kwa mara hu-share posts kwenye social media wakijulishana vitu vya kula vinavyosaidia kupunguza sumu kwenye miili yao!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom