Faida za kunywa maji asubuhi

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Katika mwili wa binadamu, unywaji maji husaidia sio tu kuondoa kiu anayokuwa nayo mtu, bali pia kufanya kazi mbalimbali katika mwili ikiwa ni pamoja na kutuepusha dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Maji huchukua karibu asilimia 70 ya mwili wa binadamu, na seli za ubongo zina karibu asilimia 85 ya maji, misuli huwa na asilimia 75 ya maji, mifupa huwa na asilimia 25 ya maji na damu huwa na karibu asilimia 82 ya maji.

Watu wengi tuna mazoea ya kunywa maji pale tunapojisikia kufanya hivyo, ila kiafya mili yetu huhitaji maji muda wote. Tunapokunywa maji muda wa asubuhi tunapoamka, tunapata faida zifuatazo:

Kunywa maji asubuhi kabla hujala kitu chochote, huwezesha utumbo kufyonza chakula vizuri na kufanya virutubisho viingie mwilini kwa urahisi.

Husaidia ukuaji wa ngozi yenye afya kwani' maji huwezesha sumu zilizoko katika damu zitoke mwilini.

Kunywa maji asubuhi husaidia kuweka uwiano katika kinga ya mwili na hivyo kuwezesha mwili kupambana na magonjwa na kukupa uwezo wa kufanya kazi zako siku nzima.
Maji yanaponyweka asubuhi huwezesha seli mpya katika misuli na damu kutengenezwa kwa haraka zaidi na kuzidi kukufanya kuwa na afya imara.

Unywaji wa maji asubuhi imegundulika kuwa, husaidia kuondoa matatizo kama vile kuhisi kichefuchefu, matatizo ya koo, macho, tumbo kama kuharisha, matatizo ya figo, mkojo, matatizo ya kupata maumivu ya kichwa na mengine mengi.

Ili kuweza kupata matokeo mazuri kiafya kwa kunywa maji asubuhi, ni vizuri ukazingatia yafuatayo:
1. Kwanza ni kuhakikisha muda wa saa moja kabla ya kunywa maji uwe hujala kitu chochote na pia baada ya kunywa maji, subiri kwa muda wa saa moja ndipo ule chakula.

2. Kuhakikisha kuwa, kiwango cha maji utakayokunywa ni sawa na lita moja na nusu yaani sawa na glasi sita, ni ngumu kunywa kama mtu ndiyo unaanza na kadri siku zinavyoenda mwili utazoea na unaweza kuanza kwa kunywa glasi tatu za maji ukapumzika kama muda wa dakika kadhaa halafu ukamalizia nyingine tatu zilizobaki.

3. Jambo la tatu ni kwamba, uwe hujatumia kinywaji chenye kilevi usiku, kwa maana kuwa isije ikawa usiku umetumia kilevi halafu asubuhi ukategemea unywe maji na kupata matokeo sawa na mtu ambaye hakutumia kinywaji chenye kilevi au pombe.

Maji ni kwa afya na uhai wetu, tujenge mazoea ya kunywa maji yanayotosheleza mahitaji ya mili yetu. Kwa siku kunywa lita mbili hadi tatu za maii husaidia kuweka mwili katika hali nzuri kiafya.

Faida za kunywa maii kabla ya kula chochote unapoamka.
1. Huboresha metaboli

Metaboli ni mchakato ambao mwilli hutumia vyakula (wanga, protini na mafuta) kupata nguvu na kujijenga. Hivyo basi, unywaji wa maji huwezesha mchakato huu kwenda vema na kuufanya mwili kuwa na afya njema. Kunywa maji kabla ya kula chochote unapoamka huufanya utumbo kuwa tayari kufyonza virutubisho. Kumbuka, maji ni muhimu kwa watoto na watu wazima pia.

2. Husaidia kupunguza uzito
Wapo watu wanaopenda kupunguza uzito wa miili vao kwani uzito mkubwa si jambo zuri kiafya. Yakupasa kukumbuka kuwa, unapoamka na kuanza kutumia vinywaji kama vile soda na juisi (sharubati) vitachangia sana kuongeza uzito wako wa mwili. Utafiti unaonyesha kuwa, soda ina sukari gramu 35 na gramu 140 za kalori ikilinganisha na maji ambayo vote ni sifuri. Hivyo basi, ni vyema ukapendelea kunywa maji zaidi kuliko vinywaji vingine.

3. Huondoa kiungulia na matatizo ya umeng'enyaji wa chakula. Kunywa maji kutakusaidia kuzimua asidi inayopatikana tumboni ambayo ndiyo husababisha tatizo la kiungulia. Pamoja na unywaji wa maji utarahisisha na kuhimiza mchakato mzima wa umeng'enywaji wa chakula. Hivyo basi, kama unakabiliwa na matatizo haya ni vyema kuzingatia unywaji wa maji kabla ya kutumia dawa mbalimbali.

4. Huboresha na kuimarisha ngozi
Utafiti unaonyesha kuwa, kunywa maji milimilita 500 kunarahisisha mzunguko mzuri wa damu katika ngozi. Hivyo basi, hili husababisha kuondoa sumu mbalimbali kwenye ngozi na kuiacha katika hali nzuri kiafya.

5. Huzuia mawe katika figo
Unywaji wa maji huzimua asidi inayosababisha mawe katika figo ambayo hupatikana tumboni. Unywaji wa maji ya kutosha kutakuepusha kwa kiasi kikubwa na matatizo ya figo. Ili kurahisisha utendaji kazi wa figo zako pamoja na afya yake, zingatia kunywa maji ya kutosha hasa asubuhi.

6. Huongeza kinga ya mwili
Kujijenga kwa kinga mwili hutegemea sana maii katika mwili wako. Hivyo ni vyema kuhakikisha unaongeza kinga ya mwili wako kwa kunywa maji ya kutosha hasa kabla ya kula kitu chochote.

HITIMISHO
Ninakuhimiza kujenga utamaduni wa kujali na kulinda afya yako, uweze kuwa mtu mwenye mafanikio zaidi. Tumeona suala la unywaii wa maji lilivyo na umuhimu; hili ni wewe kuamua tu kulifanyia kazi kwani halina gharama yoyote.​
 
Its just one of the factor but kuna vitu vingi vya kufanya asubuhi ili kuweka mwili wako vizuri.. maji pekee yake haitoshi.
 
Maji kwangu ni kama sala, asubuh nakunywa japo haifiki Lita Moja na nusu, mchana nakunywa mengi jioni sio sana!

Pia kila siku jioni nakua na ratiba ya matunda yale yanayouzwa yanakua mchanganyiko tikiti, nanasi, ndizi, parachichi, tango, embe na papai

Lkn bado napata changamoto ya kichefu chefu🤔
 
kila mtu achague kunywa maji au cha asubuhi na sikia vyote vinafanya kazi sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maji kwangu ni kama sala, asubuh nakunywa japo haifiki Lita Moja na nusu, mchana nakunywa mengi jioni sio sana!

Pia kila siku jioni nakua na ratiba ya matunda yale yanayouzwa yanakua mchanganyiko tikiti, nanasi, ndizi, parachichi, tango, embe na papai

Lkn bado napata changamoto ya kichefu chefu🤔
Unaweza kujaribu yale maji yenye ladha mfano ya lemon yanaweza kukusaidia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom