Unazifahamu fiwi? Umeshawahi kuzitumia?

Unazifahamu fiwi? Umeshawahi kuzitumia?

Nilipo google niliongeza ufahamu zaidi wa hii kitu ndo mana nikaziweka kwenye list ya mlo wangu wa mara kwa mara au ulimaanisha nione impact ya muda mfupi mwilini kama nafanya workout au nimemeza pill?
Hapana sikumaanisha hivyo. Hivi hizi ndizo black beans kuna kipindi nilisikia sijui black beans deal watu wakachukua mashamba huko tanga na kuanza kulima
 
Hapana sikumaanisha hivyo. Hivi hizi ndizo black beans kuna kipindi nilisikia sijui black beans deal watu wakachukua mashamba huko tanga na kuanza kulima
Ndo hayo hayo mkuu, mi nadhani ni dili kwa mana ni useful sana kiafya lakini wabongo bado hawajahamasika sana kuyatumia
 
Matupu..nilimkuta Mama angu anakula kuyaonja..uwiii mmh
Haha offcourse sio matamu kama soya, hata sembe ni tamu kuliko dona lakini dona ni muhimu zaidi mwilini
 
Offcourse sio matamu sana kama yale mekundu au ya soya lakini mkuu kwa upishi wa jirani zetu wakenya ulitegemea yanoge? Haha
Upushi ule! wakenya mapishi yao wanajua wenyewe. Ila nitayajaribu tena kupika pishi lakibongo nione taste yake iko vipi?
 
Yanapatikana wapi? Hayo jesca ndo yakoje na imekuaje yameitwa hivyo lazima yatakuwa yana mvuto flani kwa muonekano kama pisi kali
 
Maeneo ya korogwe katika vijiji vya makuyuni na kwasunga wanalima sana zinaitwa ngwara na wakenya ndio wanunuzi sana wanasema wanaenda kutengenezea biskuti.
Kenya wanayala sana kama mboga
 
Yanapatikana wapi? Hayo jesca ndo yakoje na imekuaje yameitwa hivyo lazima yatakuwa yana mvuto flani kwa muonekana kama pisi kali
Maharage jesca ndio yepi hayo?
37ECE94E-2EC6-48DB-8E6B-5D44D6E02A5A.jpeg

Yanapatikana Arusha na Meru huko

Mnaweza google for more info… ila ni mazuri sana
 
Amani iwe kwenu wanabodi, Ni zaidi ya mwaka sasa natumia haya maharage wengine wanayaita fiwi.

Mwanzo nililetewa na rafiki yangu huwa anayatumia mda mrefu akanishauri na mimi nianze kuyatumia kwa kuwa yana faida sana kiafya na pia yana virutubisho vingi zaidi.

Sikuwahi kuzingatia faida yake zaidi kiafya mpaka siku nilipo google benefits zake na ndio ikawa mwanzo wa kuyatumia zaidi.

Kama utaamua ku google kwa kiingereza yanaitwa black turtle beans.
Nawaza kama watanzania tulio wengi tunafahamu faida za fiwi kiafya maana siyaoni sana mitaani yakitumika, rafiki yangu anayenileteaga huwa anayanunulia maeneo ya hedaru nahisi ndio yanalimwa zaidi sehemu hizo sifahamu sana.

Kuna jamaa yangu mkenya nilimuonyesha akaniambia kenya yapo sana sometimes yanatumika mpaka kutengenezea githeri (makande).

Kwa uchache faida za fiwi kiafya;

  • Hupunguza sumu mwilini
  • Zina protini nyingi zaidi
  • Huzuia matatizo ya moyo
  • Huzuia matatizo ya cancer
  • Zina faiba nyingi zaidi
  • Zinasaidia mmeng'enyo wa chakula
  • Zinaimarisha mfumo wa neva
  • Zinazuia ugumba kwa wanaume

Kiufupi naona haya ndio maharage yenye faida zaidi kiafya kuliko haya tunayokula sijui maharage mekundu au soya lakini nashidwa kuelewa kwanini hizi fiwi hazipatikani mitaani ama labda bado hatujaelewa umuhimu wake.

Wangapi mmeshawahi kula fiwi na mnadhani ni kwanini hayapo kwa wingi mitaani?

Natamani kufahamu pia fiwi zinalimwa maeneo gani mengine hapa tanzania. Hii inaweza ikawa ni fursa iliyojificha kwa wakulima na wafanyabiashara. Nawakilisha.

View attachment 2222822

Ni kama unataka kufanya biashara kijanja janja hivi. Unaweza kutuhakikishia kitalaamu hizo faida za kiafya ulizotuorodheshea hapo? au basi sema "nasikia" kwamba fiwi zinasaidia .....
 
... hayo maeneo mlikotaja yanastawi tayari inatoa picha aina ya chakula chenyewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom