Unayakumbuka Maneno haya ya Kiswahili?

Bazazi

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
2,806
3,476
Hebu tujikumbushe maneno ya kiswahili ambayo kwa sasa aidha yamesahaulika au yanatumika kwa nadara sana.


  1. Jokofu = Friji
  2. Sigiri = Jiko la Mkaa
  3. Kishida = Underskirt,
  4. Msusa = Majani ya Maboga,
  5. ......... =........

Hebu na wewe ongezea mengine katika kukienzi Kiswahili
 
Hebu tujikumbushe maneno ya kiswahili ambayo kwa sasa aidha yamesahaulika au yanatumika kwa nadara sana.


  1. Jokofu = Friji
  2. Sigiri = Jiko la Mkaa
  3. Kishida = Underskirt,
  4. Msusa = Majani ya Maboga,
  5. ......... =........

Hebu na wewe ongezea mengine katika kukienzi Kiswahili
aiss!!ngoja nikamnunulie wife kishinda!!na dukani nitauliza kwa jina hilo hilo,sijui tutaelewana!
 
Tkumbuke na misemo hii!!!!

Tutakula au fitna?

Ndege itatua, au kiwanja kimejaa tope?
 
Tonoradi-atom, superintendent-mrakibu,,lap top - dedevuzi mpakatwa,,television-luninga,,pamphlets-kitini,faculty-kitivo.
 
Bilauli=Glasi
Shumizi=Singilendi
Sarawili=Suruali
Shifti=Dira(gauni ndefu)
Kurunzi = Tochi
Hidaya =Zawadi
 
stove = jiko la mafuta
Bichkoma = kipedo
Msalani = Chooni
Maliwatoni = Bafuni
Injika = Bandika
 
masaburi=ngongingo=wowowo
gagulo=under skirt
skipa=fulana=tshirt
njumu=daluga=viatu vya kuchezea mpira
DSC03248.JPG
 
hata neno bukta maana yake kaptula limesahaulika sana
Actually neno "bukta" ni brand/trade name kama ilivyo adidas, nike etc. Sema kwa sababu ya mazoea watu wameyatohoa na kuyatumia kama majina. Ni kama vile watu wengi wanavyotumia maneno "Thermos" (semosi), "Shell" (sheli) etc
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom