Unawezaje 'kuwin' moyo wa binti aliyetendwa?

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
8,943
16,858
Kuna binti namfukuzia lakini kila nikitupa ndoano zangu ananiambia yeye kwa sasa hayuko tayari kuwa na mtu yeyote coz mwanaume aliyekua anampenda kuliko chochote amemsaliti hivyo hataki kuwa na mtu tena.

Huyu binti nimempenda na nataka kufanya nae maisha, je kuna namna yoyote naweza fanya ili kuwin moyo wake?
 
As long ushamwambia nia yako...
Anza kuwa Rafiki yake.. Mjali na kumuonyesha upendo wako wote..
Elewa hali na mtie moyo...
Taratbu utapata nafasi na mda wake..
NB: zuia hisia zako na jikite zaidi katka kujenga urafiki
At the end u will win back her trust
Her pain is Your pain.. Start from there..
Caution.. Angalia Sana Wanawake walioumizwa sna na watu wao mara nyingi hurudiana nao.
Usije ukanywa sumu na wewe
 
Peleka posa kwa wazazi wake...SIO kila wakati unahitaji kuimba au kutupa ndoano...

unaweza kupiga sebene la vyombo vitupu au unaweza kondoa maji yote bwawani samaki wakabaki chini...

achana na nyimbo na ndoano zako peleka mshenga kwa wazazi...

tiba YA binti aliyetendwa ni kuvaa shela nyeupe anaingia kanisani na kupigiwa matarumbeta.
 
As long ushamwambia nia yako...
Anza kuwa Rafiki yake.. Mjali na kumuonyesha upendo wako wote..
Elewa hali na mtie moyo...
Taratbu utapata nafasi na mda wake..
NB: zuia hisia zako na jikite zaidi katka kujenga urafiki
At the end u will win back her trust
Her pain is Your pain.. Start from there..
Caution.. Angalia Sana Wanawake walioumizwa sna na watu wao mara nyingi hurudiana nao.
Usije ukanywa sumu na wewe
BORA UMEMPA CAUTION
 
"I shoulda seen you was trouble from the start, taught me so many lessons / How to not mess with broken hearts, so many questions /"

Muache amalizane na maumivu yake, ukilazimisha atakuja na baggage za mahusiano yaliyoisha halafu inakuwa noma.

 
As long ushamwambia nia yako...
Anza kuwa Rafiki yake.. Mjali na kumuonyesha upendo wako wote..
Elewa hali na mtie moyo...
Taratbu utapata nafasi na mda wake..
NB: zuia hisia zako na jikite zaidi katka kujenga urafiki
At the end u will win back her trust
Her pain is Your pain.. Start from there..
Caution.. Angalia Sana Wanawake walioumizwa sna na watu wao mara nyingi hurudiana nao.
Usije ukanywa sumu na wewe
Last line!
 
Mkuu .......
Pole sana kwa jambo zito lilioko mbele yako.

Nitakupa ushauri kama si mawazo yangu kulingana na uzoefu wangu wa kuanzisha mahusiano na wanawake walio umizwa kimapenzi na wapenzi wao wa zamani.

Mwanamke akiwa katika kipindi cha maumivu baada ya kuachwa ama kutendwa kimapenzi, kwanza kuwa naye karibu, ukaribu wenu uwe zaidi ya marafiki.
Katika kipindi hicho jaribu kuwa wa kawaida lakini nadhifu na uwe na mvuto & romantic kwa huyo binti,
Kamwe usioneshe hisia zako mapema, uhusiano wenu wa kirafiki uwe wa muda mrefu kusudi apate kukuamini na kufarijika moyoni mwake. Then baadaye unamuonesha hisia zako na kumuhakikishia utamtunza na kumpa mapenzi ya kweli.

* ( hakuna mkate mgumu mbele ya chai ) *

Kila kitu kinawezekana mkuu.....
Jitihada zako tu zitakufanya ufanikiwe katika kila jambo ufanyalo.
 
Angalizo...
Hawa wanawake walioumizwa asilimia kubwa bado wanafeeling za ma.ex wao..
Hivyo usishtuke siku unamkuta kakamatiwa na jamaa yake/muumizajii...

kunamdau mmja alisema hawa viumbe kuwaelewa unahitaji moyo wa bundukii..
 
Pesa ndo kila kitu tupia Tigo pesa ulainisha maumivu kwa haraka zaidi kuliko process hizo za kuwa rafiki utachelewa...

Tigo pesa ×3
 
Ukiona mdada anaumia hivyo ujue bado anampenda ex ila bhasi tu kwa kuwa ex kawa mbali naye, sasa ukiingia kichwakichwa kuhusiana naye/kumuoa utajikuta unakuwa Mfariji tu na siyo Mme apendwaye yaani ex wake akirudi kumbembeleza unabaki huna chako(anakwambia ulikuwa COMFORTER tu).
 
Back
Top Bottom