Ni ngumu kueleweka na ila kiasili sisi wanaume tumeumbwa kuwa na mke zaidi ya mmoja na kwa upande wa waislamu imehalalishwa ila kwa ndugu zangu wakristo ni mke mmoja tu na sina uhakika kama imeandikwa iwe hivyo wajuvi wa mambo wanielimishe.
Cha kushangaza wale wote wenye mwanamke mmoja wanapaparika na vimada na ndio hao ukiwaambia mke mmoja hatoshi watakupinga waziwazi mbele za watu ila nafsi zao zinacheat.
Nawaambia wanawake ukiona mume wako hana dalili zozote za kucheat na mke uko peke yako jua anakuheshimu sana na lakini usijipe moyo hafanyi jua wenzako wapo coz asili ya mwanaume yeyote ni polygamy.
NB: Mwanaume yeyote aliyetimia ni polygamist.
Binafsi siwezi kuwa na mke 1 natarajia kuongeza wa 3 inshallah!
prenge samahani kwa kutofautiana hoja, kwani kwa imani zetu mtu wa kwanaza kuumbwa na Mungu ni Adam baadaye Mungu alimuumba mwenza wake Hawa na ailikuwa mmoja kwani Mungu kama angetaka angewaumba wanawake wengi tu kwa ajili ya Adam ili hoja yako ipate mshiko. Lakini turudi katika suala la mwanamume kuoa mke zaidi ya mmoja (Polygyny), ni hali iliyokuja kutokana na kuwa wanawake wanahitaji kusitiriwa na kusimamiwa katika mambo yao kutokana na hali halisi ya uasilia wao wa kuwa ni dhaifu katika maumbile yao, kwanza tusimchukulie mwanamke kama kiumbe cha kukidhi matamanio yetu ya ngono basi, hapana, bali mwanamke mwenye hadhi ya kuwa mke ni rafiki, mfariji, mshauri, mzazi, mlezi, mtunza siri zako, mwenye kukuletea heshima na mwenye kukustarehesha na kupitia kwake unaweza kujua hali halisi ya mwanamke ambayo hutaweza kuijua kupitia kwa mama, dada, shangazi au bibi yako.
Ruhusa ya kuoa mke zaidi ya mmoja na kutozidi wanne katika uislamu ina masharti yake na sharti lake kubwa ni kuwa muadilifu baina ya hao wake, hiyo ndiyo changamoto kubwa ya
mwawe (Muoa/Mwenye WAke WEngi) ambayo kwa tabia za kibinadamu huwa tunamili zaidi kwa mke mmoja zaidi ya wengine, hivyo kunaweza kutupelekea kuwa na wakati mgumu kwenye ndoa zetu. Kuna masharti ya kuwatimizia haki zao za msingi (tendo la ndoa), kuna kuwatimizia haki zao za kiuchumi (malazi, mavazi na chakula) hivyo kuwa na mke zaidi ya mmoja si kitu rahisi kama tufikiriavyo, huo ni mlango ulioachwa wazi kwa kwa watu maalum waliyokuwa na uwezo wa kumudu hali hizo, ndiyo maana Mungu alisema kwenye kitabu chake kitakatifu cha Kuran na nadhani ndiyo kitabu pekee cha dini kilichoandika kuwa mtu aoe mke mmoja tu ikiwa atahofia kutofanya uadilifu baina ya wake zake. Hivyo mwanamume kuwa
mumkemo (MUoa MKe mMoja) ni bora kuliko kuwa
mwawe ambaye si muadilifu.
Sipingani na mwanaume kuoa mke zaidi ya mmoja bali naunga mkono hoja hiyo lakini masharti ya ndoa na uadilifu viwe ndiyo vitu vya msingi na kuzingatiwa katika ndoa hizo, na wenye kuoa mke mmoja waacheni msiwabughudhi kwani wanazo hoja zao pia za kufanya hivyo labda imani zao haziruhusu au afya ni mgogoro au hali ya kiuchumi haipo sawa lakini si ustaarabu au ungwana au uaminifu kuwa na mke mmoja halafu ukawa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine. Hayo ni mawazo yangu tu.