ooh yeah, vipi na hao waume zetu wanaokiduana huko nje na kutudhalilisha kwa hao mahawara zao? hawara anakudharau na haoni haya kuwa na mob no yako na kuku text/call? hiyo nguvu kaitolea wapi kama si kupitia kwa huyu mume? "tunadharaulishana"...wote waume/wake za watu hatutakiwi kukiduana nje coz "tunadhalilishana/dharaulishana"...i hope hapa sijatafsiri makengeza kwamba ni wanawake tusitoke nje tunawadhalilisha waume zetu but wao ni poa kusagula?
Nyamayao hata huyo mwanamke akikudharau vipi, bado hatakuwa wewe!!! WEWE NI MKEWE NA HUYO HAWARA ANALITAMBUA! na mwanaume aki-cheat unadhani wanamuita malaya??? ila wewe ka-cheat uone utakavyoitwa, kifagio, mapepe, kichenchere, malaya, easy-go, na mengine meeeengiiiiiiiiiiiii! USISHINDANE NAYE, MAANA MWISHO WA-SIKU WOTE MTAUMIA, JARIBU KUWA MJINGA ESPECIALLY KWENYE ISSUES KAMA HIZI ZA NDOA, UTAUONA MWISHO MZURI SANA!!
Sisemi wanaume wana haki ya kuwa WAZINZI! LAHASHA, WOTE JAMANI TUNATAKIWA KUBADILIKA, ILA nasema mashindano kwenye ndoa, ndio mara nyingi mwisho wake huwa ni mbayaaaaaa mnooooooooooo!!
nina mfano hai, mama mmoja tulikuwa tunakaa wote mtaani miaka hiyoooooooo, alikuwa mwandishi wa gazeti la MZALENDO nakumbuka! nilikuwa mdogo, ila nilikuwa naibia maongezi yao akija kumuelezea mama yangu matatizo ya mumewe kurudi asubuhi kila siku! akamwambia mamangu ALISHAHAMA CHUMBA ANA MIEZI MI4 SASA, NA BABA YAKE AISHIYE NJE AMEAMUA KUM-SUPORT YEYE NA WATOTO WAENDE NJE!
Yule mama akweli akaja kuondoka na watoto wake wawili wa kiume! yule baba haukupita mwaka, akaanza kuugua, akaumwa sana, miaka ile hakukuwa na ARV'S, so mamangu na babangu walishajua jirani anaumwa UKIMWI. mamangu akaamua kuwasiliana na yule mke wa yule baba na kumuelezea hali halisi, kuwa kama anaweza aje, mwenzie hali si nzuri, yule mama kweli akaja, mumewe akamwambia ULIKUWA MWEREVU KUTOSHINDANA NA MIMI, NAKUACHIA WATOTO NAJUA UTAWATUNZA VEMA! NAOMBA MSAMAHA KWA YOTE NILIYOKOSEA, NISAMEHE WEWE NA MUNGU ANISAMEHE! ALIPOMALIZA HAYO ALIKATA ROHO!
nilipokuwa naolewa, mama alinikumbushia hiyo story, na kuniambia, unajua kwanini mama 'k' hakudhurika?? ni kwasababu aliepusha MASHINDANO NA MUMEWE!! JINYEYEKESHE, JIFANYE MJINGA! MWISHO WA SIKU UTAKUWA MWEREVU MARA MIA KULIKO YEYE!
Tuwaonee watoto wetu huruma pia, kuwaacha yatima bila sababu!! kuwaacha mikononi mwa ndugu bila sababu!! TUTAMANI KUONA WAJUKUU NA VITUKUU,
TUONDOKE DUNIANI KWA MAPENZI YA MUNGU NA SI KWA UZINZI!