Hiyo ndio hasa inayotakiwa hata wenzetu walioligundua hilo ndivo wanavofanya. Kitakwimu, wanaume wengi ndio wanaotangulia kufa mapema kabla ya wanawake. Na hili linathibitishwa na kwamba watoto wengi wanaozaliwa mahospitalini ni watoto wa kiume, tatizo ni kwamba wanaume wengi wanatangulia kufa mapema kuliko wanawake. Hata ukiangalia wanawake wajane ni wengi kuliko wajane wanaume. Zipo sababu za vifo vya mapema kwa wanaume mojawapo ikiwa ni ajali ukizingatia kwamba wanaume wengi ndio wahangaikaji/watafutaji. Faida za kuoa mwanamke anayekuzidi umri ni pamoja na mwanamke huyo kuwa na uzoefu wa kutosha kuhusu maisha na suala zima la mapenzi. Hata mtume Mohamed naambiwa kwamba alimuoa mke wake wa kwanza mwenye umri wa miaka 40 wakati yeye akiwa na umri wa miaka 20, sina uhakika na hili. Wenye kuzijua faida zingine za kuoa mwanamke mwenye umri mkubwa kumzidi mume wake hebu tiririkeni.