Unatumiaje laki tatu kwa mwezi?

Babu sea

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
953
742
Jamani wanajamiiforums ninapokea mshahara laki tatu na nina mke na watoto wawili ninalipa kodi 30,000 kwa mwezi, kinachonitesa ni hesabu za kubalance mpaka hiyo hela ieneee mpaka mwisho we mwezi nifanyaje ili niweze kubakisha kiasi niweke akiba.

Msaada wenu please..
 
Punguza matumizi yasiyo ya lazima, nunua mahitaji muhimu tu hasa vyakula.

Nunua vitu kwa jumla, usinunue kidogodogo.
Hakikisha unafahamu vitu vya msingi kama mnatumia mchele, unga, sukari & mafuta kiasi gani kwa mwezi.

Kwa aina yako ya maisha kama chumba ni 30K unashindwaje kubalance 300K?

Kitu cha msingi uwe unanote kila ufanyapo matumizi/manunuzi. Hapo utafahamu unatumia kiasi gani na jinsi ya kupunguza visivyo na msingi.
 
Jamani wanajamii forum ninapokea mshahara laki tatu na ninamke na watoto wawili ninalipa kodi 30000 kwa mwezi kinachonitesa ni hesabu za kubalance mpaka hio hela ieneee mpaka mwisho we mwezi nifanyaje ili niwezekubakisha kiasi niweke akiba.

Msaada wenu please..
Achana na kuweka akiba kwanza dili na mahitaji ya lazima.. Ukifosi kuweka akiba utaitesa familia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nunua vitu kwa jumla, usinunue kidogodogo.
Hakikisha unafahamu vitu vya msingi kama mnatumia mchele, unga, sukari & mafuta kiasi gani kwa mwezi.

Kwa aina yako ya maisha kama chumba ni 30K unashindwaje kubalance 300K?

Kitu cha msingi uwe unanote kila ufanyapo matumizi/manunuzi. Hapo utafahamu unatumia kiasi gani na jinsi ya kupunguza visivyo na msingi.
Natamani nilete posa, uko mtaa gani Nifah
 
Jamani wanajamii forum ninapokea mshahara laki tatu na ninamke na watoto wawili ninalipa kodi 30000 kwa mwezi kinachonitesa ni hesabu za kubalance mpaka hio hela ieneee mpaka mwisho we mwezi nifanyaje ili niwezekubakisha kiasi niweke akiba.

Msaada wenu please..
Suala la kuweka akiba ni suala muhimu na zuri sana katika maisha yetu! weka asilimia 5% ya kipato chako iwe akiba yako kila mwezi. Zinazobakia...mpe mke wako 150,000/ hela ya matumizi kwa Mwezi mzima ( sifa za mwanamke ni kuhakikisha anabalance fedha hiyo kwa Mwezi mzima na itoshe) jitahidi chakula Cha familia kinunuliwe kwa ujumla, sabuni za kufua zisisahaulike, mpe nafasi mkeo atafute chochote kitu ili kuongeza Pato la familia. Inawezekana!; Baba lipa maji na umeme, lipa Kodi, hakikisha una emergency ya sh. 10,000 tu kila mwezi.
 
Aisee, Kuna Muda inabidi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa alilokujaalia. Kuna watu hiyo 300k ni posho yake ya mawasiliano au ndio posho ya kikao cha siku mbili...

Bajeti ya 300k kwa mwezi.
Kila siku utumie 10k.
Ina maana hapo unatakiwa upige hesabu kwa siku 10k unaitumiaje?
Chakula pekee tenga 6k
Kodi tenga 1k, hapo inabaki 3k.
Chukua 1k weka akiba.
Chukua 2k ifanye nauli na contingency.
 
Jamani wanajamii forum ninapokea mshahara laki tatu na ninamke na watoto wawili ninalipa kodi 30000 kwa mwezi kinachonitesa ni hesabu za kubalance mpaka hio hela ieneee mpaka mwisho we mwezi nifanyaje ili niwezekubakisha kiasi niweke akiba.

Msaada wenu please..
Dah! tafuta connection uhamie sehem yenye mshahara mkubwa ili uweze kufanya maendeleo maana kwa laki 3 unayopata kwa mwezi ni fedha ndogo mno na usilogwe ukakopa Benki ndio life litazidi kuwa gumu.
kumiliki usafir hapo ni changamoto yan hata ki-Ist kwako itakuwa ishu sana.

pia tawanya pesa yako kwa kufungua miradi/mirija mingine yakukuingizia kipato angalau hata 3000-5000 per day. ili upunguze ukali wa maisha na usonge mbele kwenye maendeleo ikiwemo kununua uwanja nk.
 
1. Ishi ndani ya uwezo wako,
2. Acha anasa kama michepuko na gambe
3. Usinunue vitu mdomdo, nunua vya pamoja kama unga, mchela mafuta na maharage
4. Mshirikishe mama yoyoo ajue hali halisi

Cha msingi: tafuta chazo kingine cha mapato,

Mtafutie mke kitu cha kufanya
 
Dah! tafuta connection uhamie sehem yenye mshahara mkubwa ili uweze kufanya maendeleo maana kwa laki 3 unayopata kwa mwezi ni fedha ndogo mno na usilogwe ukakopa Benki ndio life litazidi kuwa gumu.
kumiliki usafir hapo ni changamoto yan hata ki-Ist kwako itakuwa ishu sana.

pia tawanya pesa yako kwa kufungua miradi/mirija mingine yakukuingizia kipato angalau hata 3000-5000 per day. ili upunguze ukali wa maisha na usonge mbele kwenye maendeleo ikiwemo kununua uwanja nk.
Dah, unaishi wapi, watu wanalipwa chini ya hapo, laki mbili na wanafamilia maisha yanaenda, nenda viwanda vya wahindi, mshahara kwa mwezi laki na nusu
 
Punguza matumizi yasiyo ya lazima, nunua mahitaji muhimu tu hasa vyakula.

Nunua vitu kwa jumla, usinunue kidogodogo.
Hakikisha unafahamu vitu vya msingi kama mnatumia mchele, unga, sukari & mafuta kiasi gani kwa mwezi.

Kwa aina yako ya maisha kama chumba ni 30K unashindwaje kubalance 300K?

Kitu cha msingi uwe unanote kila ufanyapo matumizi/manunuzi. Hapo utafahamu unatumia kiasi gani na jinsi ya kupunguza visivyo na msingi.
Exactly mm pia Huwa nafanya hivo na inasaidia sana sio tu wenye kipato kidogo hata wanaopenda kuweka akiba ni rahis sana unakuwa unajua Kwa mwez matumizyako ni kias gani na kipi usave
 
Back
Top Bottom