Unatumiaje laki tatu kwa mwezi?

Hio pesa hutoboi mwezi niamini mim ....

Maneno ya kukutia moyo na budget za humu za kuandika Kwa hisia Ni tofauti na huku mtaani ,....

Jiandae kukopa elfu hamsin ambayo itakufanya umalize mwezi ...hapo chunga Sana ...

Kiufupi ili utoboe Kwa hio pesa mwezi inabidi uishi kama shetani ....
Labda kama yupo dar au Arusha. Mikoani anatoboa ila asahau kununua Nguo
 
Laki tatu Hana uwezo wa kutoboa Kwa familia ya mke na watoto wawili tuache kumpa matarajio hewa ...

Mke na watoto wawili wanahitaji Milo miratu Kwa siku ,....hapa tuseme amenunua ...

Kilo Kumi za Michele -25,000
Unga Kila 10 ,- 20,000
Mafuta ya Kula Lita 5- 25,000
Sukali kilo 5-16,000
Maharage kilo 5-10,000

Hapo tuseme Laki imeisha Kwa vitu vya mhimu sanaaaaa.....hivyo vyakula nimeassume vitamaliza mwezi japo Sina uhakika .....

Hapo Laki imeisha imebaki Laki mbili (200,000)


Twende matumizi mengine ..

-Kubadili mboga mboga ,dagaa ,nyama kidogo ,mchicha ,sio Kila siku mtakula mahalage ...---20,000
-gesi au mkaa --25,000
-chumvi ,majani ya chai --4000
-sabuni ,kipande na Unga &steel wire kusugulia sufuria -5000

Maji ya kununua Kwa mwezi /bill -5000

Umeme kulipa Kwa mwezi -5000

Nauli ya kwenda kazin na Kurudi baba pekee yake -30,000

Nauli za mke na watoto kutoka sehemu kwenda sehemu Kwa emergency, mkee hawezi kaa nyumbani kama jiwe ,kwenda sokon n.k-20,0000

Hapo umetumia Laki na uchafu (130,000) ...



Baada ya yote hayo imebaki 70k..

Hujanunua vocha ya kuwasiliana na mkeo tuseme Kwa mwezi utatumua -5000

Mtoto amepata kikohozi ,au kichwa kinauma ,umenunua hata Panado .n.k -5000

Kanisani hujatoa sadaka wewe na mke ,Kwa mwezi wote wawili tuseme -10,000

Hela ya takataka ,ulinzi shirikishi mtaani maana mjumbe atakuja kudai -5000

Mwanaume hauwezi kaa nyumbani tu utaangalia hata mpira ,bia moja ,-20,000

Hapo hujanunua nguo ,mkeo hajaenda saloon ,wewe hujaenda saloon kunyoa ndevu ,watoto hawajaenda hata kutembea kokote hata beach ,watoto hujawanunulia hata biscuit,ndugu hujawapa hata 100, mama mzazi hajakuomba hata 5000,,,, hujapata emergency ya kuumwa hata hospital,,hujahonga Kwa michepuko ,hujapoteza pesa (maana kuna hela zinapotea tu automatic bila kujua sababu ...

Laki tatu hutoboi aiseee....

Na hapo ili utoboe mwezi lazima uishi kama shetani kwa matumizi ya hapo juu.....
:D:D:D:D:D
 
Kabla sijasema umeshanichamba hivi? Nikisema je?
Nimechekaaaaaa
Nakuambia ukweli nifah, ulikuwa uko vizuri sana, lakin baada ya kuwa na yule jamaa ukabadilika, jamaa mtu wa kujisikia sana, majivuno meengi wakati hela hana. ujanja janja tu amekutumia kupata umaarufu tu
 
Nimesoma maelezo ya wengi, lakini hiyo laki3 inategemea mazingira aliyomo, lakini hata kama Yuko wapi Bado hiyo laki 3 itamfanyia KAZI na maisha yataenda tu, watu wanashangaa tu kuwa pesa ndogo hiyo lakini Kuna watanzania hata laki moja hawapati Kwa mwezi, wanazo familia na maisha yanasonga tu
 
Tatizo hujasema unaishi mkoa gani na umri wa watoto pia. Kuna mikoa hiyo hela ni kubwa mengine ni ndogo na mingine ni kiduchu.

Swala la matumizi muachie mkeo, wewe focus na kuitafuta hela tu, ishu za matumizi muachie mkeo.

Ila Mkuu ilikuwaje ukaanza familia kubwa kwa kipato kidogo au ni mambo yalienda arijojo wakati fulani?
 
Suala la kuweka akiba ni suala muhimu na zuri sana katika maisha yetu! weka asilimia 5% ya kipato chako iwe akiba yako kila mwezi. Zinazobakia...mpe mke wako 150,000/ hela ya matumizi kwa Mwezi mzima ( sifa za mwanamke ni kuhakikisha anabalance fedha hiyo kwa Mwezi mzima na itoshe) jitahidi chakula Cha familia kinunuliwe kwa ujumla, sabuni za kufua zisisahaulike, mpe nafasi mkeo atafute chochote kitu ili kuongeza Pato la familia. Inawezekana!; Baba lipa maji na umeme, lipa Kodi, hakikisha una emergency ya sh. 10,000 tu kila mwezi.
Mbona ndogo sana elf 10?, walau 30 ya dharura
 
1. Ishi ndani ya uwezo wako,
2. Acha anasa kama michepuko na gambe
3. Usinunue vitu mdomdo, nunua vya pamoja kama unga, mchela mafuta na maharage
4. Mshirikishe mama yoyoo ajue hali halisi

Cha msingi: tafuta chazo kingine cha mapato,

Mtafutie mke kitu cha kufanya
Wageni wasimtembelee
 
Jamani wanajamiiforums ninapokea mshahara laki tatu na nina mke na watoto wawili ninalipa kodi 30,000 kwa mwezi, kinachonitesa ni hesabu za kubalance mpaka hiyo hela ieneee mpaka mwisho we mwezi nifanyaje ili niweze kubakisha kiasi niweke akiba.

Msaada wenu please..
Kama unafanya kazi mbali kiasi cha kupanda daladala nunua baiskeli. Hela laki 2.5 inatosha sana kula na kulipa umeme na maji kwa familia ya watu4. Ila tu
Unga kilo 1 kila siku 30kg mwezi mchele 1kg kila week
Mboga elf60 mwezi, maji na umeme elf10. Sabuni ya kufua na kuoga 10k, mafuta pika 20k, chumvi 3000, sukari ya uji asubuhi 4kg mwezi,
 
Hakikisha unakodi shamba ekari moja. Lima mahindi nusu eka na maharage nusu eka.
Hapo utakuwa kwanza umetatua changamoto ya misosi.
Wapigie simu ndugu zako kijijini wakutafutie shamba la kukodi.
Tuma hela ya kulimia, mbegu na mbolea.
Kwa mwaka utaweza kuokoa hadi Tsh milioni moja kwenye gharama za chakula.
 
Jamani wanajamiiforums ninapokea mshahara laki tatu na nina mke na watoto wawili ninalipa kodi 30,000 kwa mwezi, kinachonitesa ni hesabu za kubalance mpaka hiyo hela ieneee mpaka mwisho we mwezi nifanyaje ili niweze kubakisha kiasi niweke akiba.

Msaada wenu please..

Panga na mkeo acha kutusumbua sisi
Mbona hamuwaamini wake zenu?
Uje hapa utuombe wazo la biashara
Mambo ya matumizi ni wewe na mke wako
 
Back
Top Bottom