Naweza kujenga kwa mshahara wa laki tatu?

Naweza kujenga kwa mshahara wa laki tatu?

Erick MR

Member
Joined
Nov 11, 2022
Posts
77
Reaction score
166
Wakuu naombeni ushauri nimeajriwa na nalipwa mshahara wa laki tatu kwa mwezi Nina ndoto za kununua kiwanja na kujenga pia

Naombeni ushauri nifanye nini au kitu gani nizingatie niweze kufikia lengo. Kwasababu mshahara huu ndio nautegemea kwa Kila kitu.
 
Wakuu naombeni ushauri nimeajriwa na nalipwa mshahara wa laki tatu kwa mwezi Nina ndoto za kununua kiwania na kujenga pia .naombeni ushauri nifanye nini au kitu gani nizingatie niweze kufikia lengo . kwasababu mshahara huhu ndio nautegemea kwa Kila kitu.
Unaweza kujenga tena ndani ya mwezi tu
Kufuga kuku inahitaji uanze na banda dogo kwanza hata la elfu 30,kadri mtaji unavokua mkubwa unaongeza banda lako
 
Kila kitu kinawezekana, Ila inabidi ukuze kipato chako kupitia uwekezaji mwingine nje ya mshahara ili zikuwezeshe kukuza kipato chako then ukafikiria swala la kujenga. Ujengaji unategemea nature ya eneo;
  • Kuna maeneo materials ya ujengaji kama udongo wa tofali na mota vinapatikana hapo hapo kiwanjani kwako (Ujengaji usio na garama kubwa)
  • Maeneo ya kuchanga
  • Maeneo yenye miamba
 
Swali la 1. Una miaka mingapi ?
2. Una mchumba au mke ?
3. Una mtoto au familia ?
4. Una mpango wa kuwa na mtoto au watoto ?( wangapi )
5. Una mpango wa kuwa na familia/kuoa ?

Nitarudi kwa maswali ya nyongeza nijibu kwanza hayo
 
Kiwanja unataka kitoke humo kwenye 300k?
Ni ngumu mkuu, labda ukope hela ununue kiwanja!
Au ukanunue kaeneo mkoani kijijini ujenge kajumba.
Hajazema hizo ndoto anataka zitimie baada ya miaka mingapi.

Akiweka akiba ya laki 2 kila mwezi na kujibana kwa miaka 2 mbona anunua kiwanja na kuanza ujenzi wa nyumba ndogo nje ya mji.
 
Wakuu naombeni ushauri nimeajriwa na nalipwa mshahara wa laki tatu kwa mwezi Nina ndoto za kununua kiwania na kujenga pia .naombeni ushauri nifanye nini au kitu gani nizingatie niweze kufikia lengo . kwasababu mshahara huhu ndio nautegemea kwa Kila kitu.
Kwa mshara huo ukijenga lazima tukuite tukuhoji kama huuzi bangi
 
Wakuu naombeni ushauri nimeajriwa na nalipwa mshahara wa laki tatu kwa mwezi Nina ndoto za kununua kiwania na kujenga pia .naombeni ushauri nifanye nini au kitu gani nizingatie niweze kufikia lengo . kwasababu mshahara huhu ndio nautegemea kwa Kila kitu.
kama uko peke yako unaweza
kama uko na gf, mchumba au mke, mpige chini
 
Katika maisha unatakiwa uwe na mipango mikakati ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Kwa wewe nakushauri uweke mipango vizuri kwanza ili kuhakikisha kuwa mshahara wako unaongezeka kuweza kukidhi mahitaji yako na kuweka akiba ziada.

Kama kazi yako inahitaji elimu basi jiendeleze kielimu na baada ya kuhitimu na kupanda cheo utajenga nyumba ya ndoto yako.

Kwa sasa hivi hiyo laki tatu utaishia kujenga banda la mabati kama yale wanayouzia mkaa ushwazini
 
Swali la 1. Una miaka mingapi ?
2. Una mchumba au mke ?
3. Una mtoto au familia ?
4. Una mpango wa kuwa na mtoto au watoto ?( wangapi )
5. Una mpango wa kuwa na familia/kuoa ?

Nitarudi kwa maswali ya nyongeza nijibu kwanza hayo
Acha kumkatisha mwenzako tamaa na mawazo yako ya kizinzi .
Katika maelezo yake hajasema kama ana familia.
 
Wakuu naombeni ushauri nimeajriwa na nalipwa mshahara wa laki tatu kwa mwezi Nina ndoto za kununua kiwania na kujenga pia .naombeni ushauri nifanye nini au kitu gani nizingatie niweze kufikia lengo . kwasababu mshahara huhu ndio nautegemea kwa Kila kitu.
Mkuu Anza. Mimi nyumba yangu nilianza kununua misumari kwanza vingine vikafuata.
 
Wakuu naombeni ushauri nimeajriwa na nalipwa mshahara wa laki tatu kwa mwezi Nina ndoto za kununua kiwania na kujenga pia .naombeni ushauri nifanye nini au kitu gani nizingatie niweze kufikia lengo . kwasababu mshahara huhu ndio nautegemea kwa Kila kitu.
Kwanza upo mkoa gani?
Mkoa ambao maisha yako juu utaweza kutoboa na gharama za maisha? Kama utaweza bhasi tenga kiasi cha kila mwezi cha kutoa kwa ajili ya kiwanja.baada ya kununua kiwanja (sijui ni cha ukubwa gani na mkoa gani na kijijini au mjini) ndio uanze savings za kujenga wakati huo ulishaplan kwamba utajenga nyumba ya aina gani na kwa gharama gani za makadirio.
 
Back
Top Bottom