Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,202
- 213
Wakati Fulani mwaka jana nilikuwa napiga gumzo na rafiki yangu mkenya nikamuuliza mbona sikuhizi simwoni amepotelea wapi akaniambia anajiandaa kwa safari yake ya marekani ndio anafanya mipango yake ili akaanze maisha mapya .
Nilishituka kidogo nikaanza kuhoji maswali zaidi , nikagundua alitumiwa mualiko wa mkutano kutokea marekani , kwamba huo mkutano utafanyikia marekani .
Nikamuuliza tena kisha huo mkutano utafanyikia nchi za afrika magharibi ? unahusu mambo ya jamii ? Ndio akanijibu kama nilivyotegemea .
Basi nikamwambia aende ubalozi wa marekani kuulizia kama hiyo NGO iliyomwandikia mualiko inajulikana , inausajili na kama huo mkutano una idhini ya serikali ya nchi husika manake wanaenda watu wengi zaidi ya 500 si ndio ??
Akaenda kule baada ya muda na kugundua ni uwongo hakuna NGO kama hiyo na mtu aliyekuwa anawasiliana nae yuko Nchi za afrika magharibi kutokana na IP Address zake na taarifa zingine alizotoa .
Sasa huyu amealikwa katika mkutano kuna wengine wanaandikiwa mialiko ya kufanya kazi nchi za ulaya , wanapojisajili wanakutanishwa na watanzania wenzao ambao wanafanya kazi kama wakala wa hawa wanaotafuta hawa watu .
Watu wanajisajili haswa wasichana warembo kwenda kufanya kazi nchi za ulaya , wengi wanaishia nchi za asia na ghuba wanauzwa katika vilabu vya pombe na sehemu zingine za starehe wakishatumika wanarudishwa makwao .
Mfano pale mtaa wa jamhuri kuna kijana mmoja sijui kama saa hizi bado yuko huyu kazi yake ilikuwa ni kutengeneza barua haramu na kuzipeleka katika baadhi ya balozi kujifanya kwamba ni mialiko kutoka ulaya na anawauzia watu kwa bei nzuri tu watu wananunua .
Pia amekuwa na shuguli za kupeleka watu ulaya haswa nchi ya uholanzi , ukifika huko uholanzi unakaa kambini kwa miezi 6 hivi unajifunza baadhi ya desturi za kule na lugha kidogo halafu passport yako wanaichukuwa .
Ukitoka hapo sasa unaenda kufanya kazi kuhakikisha unarudisha zile gharama za kukutoa Tanzania mpaka kule na muda ule wa kukuweka kambini basi ukishamaliza unaachiwa huru .
Na hizi ndio safari za miujiza ambazo vijana wengi wanafikiri za kweli n ache badala yake wanaishia huko kuuzwa haswa wasichana kwa watu wa mataifa mengine .
Wengine wanabebeshwa madawa ya kulevya haswa wanaume au kulazimishwa kusafirisha bidhaa haramu kati ya mipaka ya nchi za ulaya wanapofika huko kwenye shuguli zenyewe .
Hivi mtu hafikiii mara nyingi anapoambiwa naweza kukupeleka ukaishi japani bila wewe kujua kijapani bila wewe kuwa na taarifa zozote za sehemu unazofika ?
Kama wewe unataka kwenda ulaya , unaweza kujaribu bahati yako kujisajili ujione .