selestei
JF-Expert Member
- May 10, 2014
- 243
- 60
Ukweli kila binadamu anapenda kupendwa,,au kukubalika na jamii inayomzunguka, lakini tunaweza jikuta katika mazingira watu wengi hawakupendi au unachukiwa na watu wengi.
Mpaka kufikia hatua ya kusema labda umerogwa, wengine mpaka wanaenda kwa waganga ili wapendwe au sijui nyota imeibiwa, damu ya kunguni na nk.
Lakini tunasahau kujiuliza ni kwanini hupendwi na wengi?
Hizi ni sababu zinazofanya usipendwe na jamii inayokuzunguka either mahala unapofanya kazi, nyumbani, jirani, na nk.
(1)Salam ndio msingi mzima wa mahusiano. Kama hamna salam hamna mahusiano. Usimpite mfanyakazi mwenzako bila kumsalimia hata awe na cheo kidogo sana kuliko wewe, mfano mlinzi, cleaner, karani, nk.
Kadhalika ukiwa nyumbani pia wasalimie wote ulionao nyumbani..
Jirani zako usiwapite bila kuwasalimia..
(2) Shiriki kwenye kazi inayohusu jamii mfano misiba, hapa ukiona watu wanapika wanachambua mchele, fanya na wewe. Hii kwa wanawake. Lakini pia kuna vishughuli vya wanaume, jitahidi ujumuike nao.
Unapokuwa kazini fanya kazi yako kwa bidii,, unaweza pia ukafanya zile ambazo za kujitolea,, shiriki na hizo walau mara chache kuliko kutoshiriki kabisa.
Ukiwa nyumbani kama wewe unaishi na wazazi, shiriki kazi za nyumbani, usikae tuu kila kitu unasubiri house girl afanye.
(3) Saidia wenye shida, when you give you get back in return, pia kutoa si lazima kwa masikini tuu hata kwa kutoa zawadi ndogo ndogo, watu hujisikia kupendwa wakipewa zawadi, tajiri akipewa zawadi hufurahia pia.
(4) Ongea kwa kiasi unapokuwa sehemu ya mijumuiko, ni rahisi kujizuia na mengi unapokuwa na kiasi.
(4).. Upendo.. Utasemaje unampenda Mungu usiyemuona huku unamchukia jirani yako,, ukifanya hayo ya juu utakuwa umependa, Upendo huvumilia, upendo hauhesabu mabaya, hauchukii, haujivuni, hausengenyi.
Kuna mengi ila hayo ni ndio msingi wenyewe,, ukifanya haya aisee utakuja niambia.. Utapendwa na watu mpaka watakuuliza mganga wako nani.. Mimi nilifanya hivi sehemu ya kazini nilipendwa na wafanyakazi mpaka ilikuwa kero kuanzia managers mpaka wafanyakazi wadogo.