Unataka kumjua anayekuibia mumeo? Mbinu hizi zitakufaa!

Kwa hiyo definition ya kujiamini kwako ni kutokufahamu ukweli (au kutokujishughulisha kuufahamu ukweli) au kukubali kuchangia???


Mimi ninajiamini sana lakini still nina mbinu za kipelelezi kuliko za FBI.

Na niko tayari kufanya maamuzi magumu. Watu mnakuwa wazembe tu...mpaka mtu anaanza kuwa na dalili za HIV hana hili wala lile kumbe anaishi na popo bawa ndani. Ukweli lazima utafutwe bana.

Ndoa hiyo lazima ivunjike!
Charminglad una wapoteza wenzioz!

Uko nikuto jiamini
 
hali zenu wadau wa Jf kuna hii nimekutana nayo naomba tuijadili..........

1. Ikague simu yake
Katika mazingira ya kawaida, haishauriwi kuikaguakagua simu ya mumeo kwani kufanya hivyo ni kuonesha jinsi usivyomuamini lakini unapohisi unaibiwa na hujui ni nani mwizi wako, unaweza kuanza kuikagua simu ya mpenzi wako kwa siri sana. Angalia simu zilizoingia na kutoka, meseji zilizotumwa na kuingia. Kama kuna mtu ambaye ana uhusiano naye, utagundua lakini tambua kwamba ni zoezi la muda mrefu na fanya hivyo bila mpenzi wako kugundua. Tumia muda anaokwenda kuoga, chooni na anapoisahau simu nyumbani, ipo siku utabaini siri nzito.

2. Ingia kwenye Facebook yake
Kama mumeo ni mtu wa facebook na unajua password yake, ingia mara kwa mara kwenye ukurasa wake. Kama ulikuwa hujui mtandao huo wa kijamii sasa hivi unatumiwa na wengi katika kuzisaliti ndoa zao. Waume za watu wanatumia njia hiyo kuwasiliana na vimada baada ya kubaini wakitumia simu ni rahisi kukamatwa. Kwa maana hiyo, tumia mbinu ya ushawishi kupata password yake na huko unaweza kumbaini mtu anayekuharibia.

3. Mfanyie ‘sapraizi' kazini
Kama mumeo anafanya kazi, elewa kwamba wengi hutumia muda wa ‘lunch' kuwa na wapenzi wao wa pembeni. Unaweza kumuibukia siku mojamoja kazini kwake au kwenda sehemu ambayo hupendelea kula chakula cha mchana.
Kwa mfano siku ya kwanza umemkuta yuko na demu, ukaondoka kisha siku nyingine ukawakuta tena pamoja, ukaondoka na siku nyingine tena ukawaona katika mazingira hayo, akili yako itakupa jibu. Hata hivyo, katika njia hii uwe makini kwani inawezekana huyo msichana ni mfanyakazi mwenzake ambaye hupendelea kwenda naye lunch tu na hakuna kingine cha zaidi.

4. Chunguza nguo zake unapozifua
Wakati unafua nguo zake, tumia muda mwingi kuzichunguza. Angalia kwenye waleti yake, unaweza kukutana na risiti zinazoonesha amenunua vitu vya kike ambavyo wewe hujaviona. Pia unaweza kukutana na vikaratasi vyenye namba za simu ambazo ukizipiga ni za mwanamke na ukimwambia wewe ni mke wa fulani, anakupa majibu ya kiwiziwizi. Pia kwenye nguo zake unaweza kubaini ‘lipstick' nyekundu wakati wewe hutumii hiyo.

5. Muazime gari lake
Kama mpenzi wako analo gari, mshitukize kisha muombe gari lake uende sehemu. Kwa kumshitukiza atakuwa hajapata nafasi ya kulisafisha hivyo ukiwa nalo lichunguze kila sehemu. Unaweza kukutana na risiti, namba za simu au nguo na vitu vya kike ambavyo huvijui. Wapo ambao waliwahi kufanya hivyo na wamefanikiwa kubaini usaliti wanaofanyiwa.

6. Mshitukize baa
Yawezekana mumeo ni mnywaji wa pombe na umekuwa ukimpa uhuru wa kufanya hivyo bila kumfuatilia. Kama umebaini unasalitiwa na humjui anayekuibia penzi lako, siku moja muulize anakunywa pombe wapi, kwa kuwa amezoea huna tabia ya kumfuatilia, atakujibu. Siku hiyo mfuate, mwanamke utakayemkuta naye mnoti kisha ondoka bila mpenzi wako kujua. Siku nyingine, mbabatize tena akiwa baa na kama utamkuta na msichana yuleyule, basi mwekee alama na kwa uchunguzi ambao utaendelea nao, kuna siku utajua ukweli.

7. Mfuatilie
Hili nalo halishauriwi kulifanya kwani mpenzi wako akijua unamfuatilia, anaweza kukuacha kwani atajua humuamini na wengi hawapendi kuendelea kuishi na watu ambao hawawaamini. Ila sasa, ukishahisi unasalitiwa huna budi kufanya hivyo. Tumia watu kufuatilia nyendo zake kila anapokwenda na haitachukua siku nyingi utajua huyo mpenzi wako anakusaliti na mtu gani.

Kwa kifupi ni kwamba, unastahili kuwa na mtu muaminifu, anayekujali na kukupenda kwa dhati. Unapohisi mumeo si muaminifu, usikimbilie kuomba talaka au kuja juu kama moto wa kifuu bila kuwa na ushahidi. Tumia mbinu hizo hapo juu kutafuta ushahidi wa kile unachokihisi na mwishowe utafanya uamuzi sahihi.

POLENI KWA KUWACHOSHA ILA NI NJIA YA KUJIFUNZA........

Wastage of time.
 
Wanaume wanabonda mbinu zozote za kuchunguzwa kwa kuwa wana maslahi yao binafsi. Nashangaa kwa mwanamke kusema mi najiamini napendwa...Sasa kama unajiamini unapendwa na huko peke yako si ina maana hata ukichunguza hutapata kitu...Kimoyo moyo hakuna hata anayejiamini ni kwamba mmekubali matokeo na mnaogopa kugundua kwa kuwa hamna uwezo wa kuamua chochote hata mkijua.
 
charminglady katika hizi zote ulizoandika hakuna hata moja ambayo itafanya kazi kwangu kama ningekuwa mwizi, ntajaribu kujadili baadhi ya hoja; Suala la simu: Hii haina mashiko maana huwa nampa uhuru na simu yangu sana na kwamba any incoming text hua naifuta baada ya kuisoma, hua nafuta calls zote ambazo mke wangu anaweza kuzi-suspect (narudia kama ningekua mwizi), pia kuna huduma nyingi san akwene simu za ku-restrict/blacklist number; mfano; baadhi ya simu za Samsung ukisha-activate unaifuta hio namba kwahio simu hairuhusu simu yoyote ngeni (ambayo haiko kwene Phonebook) Kuna Blacklist hadi ya text sms, so kwa ishu ya simu naweza kukuachia kutwa nzima na usipate hicho unachokitaka.


Suala la kufua ni nadra sana kuweka docs kwene suruali hilo sahau, mmmh ngoja niendelee na kazi kwanza
 
Last edited by a moderator:
Huku ni kutafuta ugonjwa wa moyo kwa mwanamke.Huna haja ya kufanya yote haya eti kisa unamfuatilia ili iweje sasa?Kama humuamini jipange katafute huyo anayeminika ambaye bado hajazaliwa.Mi nikijua tu unanifuatilia hivi naongeza na nyumba ndogo ya pili kabisaa
 
kuna watu hawajui mapenzi, hawajui kujiamini , na waojidhalilisha.... mmoja wapo ni huyo anayechunguza mwenzake
 
jamani msinishambulie, mie hiyo nimeikuta somewhere nikaona ni bora niilete hapa ili nione mtazamoa wenu pia...

si maneno yangu hata kidogo, nawashuruku wote kwa michango yenu sasa naanza kuelewa
 
Wanaume wanabonda mbinu zozote za kuchunguzwa kwa kuwa wana maslahi yao binafsi. Nashangaa kwa mwanamke kusema mi najiamini napendwa...Sasa kama unajiamini unapendwa na huko peke yako si ina maana hata ukichunguza hutapata kitu...Kimoyo moyo hakuna hata anayejiamini ni kwamba mmekubali matokeo na mnaogopa kugundua kwa kuwa hamna uwezo wa kuamua chochote hata mkijua.

yani uko sawa kabisa mamito ninachokiona kwa wanawake wengi hapa ni woga wa kuujua ukweli kwamba waume/wapenzi wao hawajatulia,wanahofia life after knowing the truth itakuaje??kama kweli unajiamini kwamba mumeo/mpenzio hawezi kwenda kwa mwingine kwa nini unaogopa kushika simu yake?lol!
 
Naungana na nyumba kubwa, big up
Nashangaa watu walivyoponda hii mada, kwahiyo ukihisi mwenzio anachepuka, ujifanye mnjinga tu huku roho inakuuma.

nionavyo mimi ukihisi mwenzio si muaminifu ni jukumu lako kufind out the truth, ni vizuri ujue ili umuonye mwenzio na ajue kuwa umejua, na pia uchukue hatua kujikinga na magonjwa.
Sasa ukae kimya mfe wote muache watoto wanateseka!!!
Au ukae kimya mwisho ahamie kabisa kwa huyo kimada!!!! kwa kweli Mmenishangaza sana

wanawake jitahidini muwe independent, hii itasaidia pale utakapoitajika kuchukua maamuzi magumu.....
 
Last edited by a moderator:
Wazungu wanafanya haya kwa sana tu, ndo maana relationships zao ni delicate mno kiasi kwamba ndoto tu inaweza kusababisha mwenzio akakuacha, kila siku ni presha inapanda presha inashuka loh!
 
jamani msinishambulie, mie hiyo nimeikuta somewhere nikaona ni bora niilete hapa ili nione mtazamoa wenu pia...

si maneno yangu hata kidogo, nawashuruku wote kwa michango yenu sasa naanza kuelewa

Huna haja ya kua apologise, i think you are very right!
na mada umeiweka vizuri, kwamba 'ukuhisi mwenzi sio muaminifu" unaanzaje kutafuta ukweli.
mtoa mada hajasema kuwa hii itakuwa shughuli yako ya kila siku za mahusiano yenu. I stand to be corrected
 
Akhaa! nataka kufa na BP mie! atajua mwenyewe badala yakujitia bp bora niende shule nikajiendeleze kusoma kuliko kumchunguza mtu mzima na mvi mpaka kwenye nanihii...
 
Dear charminglady,

Hii barua uliyotuwekea hapa nimeisoma kwa makini sana na kujaribu ku diggest yale yote uliyoyasema ili kuwapa mwanga wanawake wenzio namna ya kumkamata mwizi wa mumeo. Huu ndio mrejesho wangu kuhusiana na hayo;

Talking from men's perspective, wanaume tunapenda sana kufuatiliwa na wake/wapenzi wetu ila sio ifikie extreme. Inapokwenda extreme kiasi cha kujua kwamba unakagua simu yake kila akitoka kazini au unaingia kwenye FB account yake (ambayo siku hizi imepoteza msisimko hata hivyo) sio tu kwamba hatapenda ila atakudharau na kukushia hadhi. Men wants women who are strong and who believes in themselves. Kwa hilo this is my advice, never touch your man/woman's phone.

Surprise kazini, yeah this is good lakini kuna mazingira ambayo unaweza kuhisi unajenga kumbe unabomoa. Tunapokuwa makazini huku tunakuwa na vitu vingi sana ambavyo wakati mwingine hatupendi wanawake wetu wavijue. Kwa mfano we umeenda na surprise yako ukakuta mpenzi wako/mumeo anakoromewa na bosi wake, na mabosi wanavyopenda sifa ataongeza wewe ukitokea. Unajua what will happen? When he comes back akikuhurumia sana basi hataongea na wewe wiki nzima

Ngoja niishie hapa kwa sasa ila tu maneno ya busara, binadamu hachungwi ila hujichunga mwenyewe, be a gud woman to him and believe me kabla hatujaruka ruka huwa tunajiuliza maswali mengi sana na mojawapo ni how my woman would feel kama akijua nafanya hivi? Kama mwanamke mwenyewe waluwalu then you dont even think about it. Kumfuatilia haisaidii mama
 
mmmh!magonjwa yasiyokuwa na vipimo hospitali yanaletwa na mambo kama haya. Halafu siku hizi ndoa zetu hizi tuna tabu kweli, watu badala ya kutumia muda mwingi kupendana na kuheshimiana tunachunguzana ili tuumizane.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom