Unataka kumjua anayekuibia mumeo? Mbinu hizi zitakufaa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unataka kumjua anayekuibia mumeo? Mbinu hizi zitakufaa!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by charminglady, Jul 19, 2012.

 1. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,852
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  hali zenu wadau wa Jf kuna hii nimekutana nayo naomba tuijadili..........

  1. Ikague simu yake
  Katika mazingira ya kawaida, haishauriwi kuikaguakagua simu ya mumeo kwani kufanya hivyo ni kuonesha jinsi usivyomuamini lakini unapohisi unaibiwa na hujui ni nani mwizi wako, unaweza kuanza kuikagua simu ya mpenzi wako kwa siri sana. Angalia simu zilizoingia na kutoka, meseji zilizotumwa na kuingia. Kama kuna mtu ambaye ana uhusiano naye, utagundua lakini tambua kwamba ni zoezi la muda mrefu na fanya hivyo bila mpenzi wako kugundua. Tumia muda anaokwenda kuoga, chooni na anapoisahau simu nyumbani, ipo siku utabaini siri nzito.

  2. Ingia kwenye Facebook yake
  Kama mumeo ni mtu wa facebook na unajua password yake, ingia mara kwa mara kwenye ukurasa wake. Kama ulikuwa hujui mtandao huo wa kijamii sasa hivi unatumiwa na wengi katika kuzisaliti ndoa zao. Waume za watu wanatumia njia hiyo kuwasiliana na vimada baada ya kubaini wakitumia simu ni rahisi kukamatwa. Kwa maana hiyo, tumia mbinu ya ushawishi kupata password yake na huko unaweza kumbaini mtu anayekuharibia.

  3. Mfanyie ‘sapraizi’ kazini
  Kama mumeo anafanya kazi, elewa kwamba wengi hutumia muda wa ‘lunch’ kuwa na wapenzi wao wa pembeni. Unaweza kumuibukia siku mojamoja kazini kwake au kwenda sehemu ambayo hupendelea kula chakula cha mchana.
  Kwa mfano siku ya kwanza umemkuta yuko na demu, ukaondoka kisha siku nyingine ukawakuta tena pamoja, ukaondoka na siku nyingine tena ukawaona katika mazingira hayo, akili yako itakupa jibu. Hata hivyo, katika njia hii uwe makini kwani inawezekana huyo msichana ni mfanyakazi mwenzake ambaye hupendelea kwenda naye lunch tu na hakuna kingine cha zaidi.

  4. Chunguza nguo zake unapozifua
  Wakati unafua nguo zake, tumia muda mwingi kuzichunguza. Angalia kwenye waleti yake, unaweza kukutana na risiti zinazoonesha amenunua vitu vya kike ambavyo wewe hujaviona. Pia unaweza kukutana na vikaratasi vyenye namba za simu ambazo ukizipiga ni za mwanamke na ukimwambia wewe ni mke wa fulani, anakupa majibu ya kiwiziwizi. Pia kwenye nguo zake unaweza kubaini ‘lipstick’ nyekundu wakati wewe hutumii hiyo.

  5. Muazime gari lake
  Kama mpenzi wako analo gari, mshitukize kisha muombe gari lake uende sehemu. Kwa kumshitukiza atakuwa hajapata nafasi ya kulisafisha hivyo ukiwa nalo lichunguze kila sehemu. Unaweza kukutana na risiti, namba za simu au nguo na vitu vya kike ambavyo huvijui. Wapo ambao waliwahi kufanya hivyo na wamefanikiwa kubaini usaliti wanaofanyiwa.

  6. Mshitukize baa
  Yawezekana mumeo ni mnywaji wa pombe na umekuwa ukimpa uhuru wa kufanya hivyo bila kumfuatilia. Kama umebaini unasalitiwa na humjui anayekuibia penzi lako, siku moja muulize anakunywa pombe wapi, kwa kuwa amezoea huna tabia ya kumfuatilia, atakujibu. Siku hiyo mfuate, mwanamke utakayemkuta naye mnoti kisha ondoka bila mpenzi wako kujua. Siku nyingine, mbabatize tena akiwa baa na kama utamkuta na msichana yuleyule, basi mwekee alama na kwa uchunguzi ambao utaendelea nao, kuna siku utajua ukweli.

  7. Mfuatilie
  Hili nalo halishauriwi kulifanya kwani mpenzi wako akijua unamfuatilia, anaweza kukuacha kwani atajua humuamini na wengi hawapendi kuendelea kuishi na watu ambao hawawaamini. Ila sasa, ukishahisi unasalitiwa huna budi kufanya hivyo. Tumia watu kufuatilia nyendo zake kila anapokwenda na haitachukua siku nyingi utajua huyo mpenzi wako anakusaliti na mtu gani.

  Kwa kifupi ni kwamba, unastahili kuwa na mtu muaminifu, anayekujali na kukupenda kwa dhati. Unapohisi mumeo si muaminifu, usikimbilie kuomba talaka au kuja juu kama moto wa kifuu bila kuwa na ushahidi. Tumia mbinu hizo hapo juu kutafuta ushahidi wa kile unachokihisi na mwishowe utafanya uamuzi sahihi.

  POLENI KWA KUWACHOSHA ILA NI NJIA YA KUJIFUNZA........
   
 2. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  [​IMG] charminglady..Waswahili walisema Ukimchunguza sana nanilihii hutamla....
   
 3. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  ukishajua what next!! Ni bora kutokujua ukweli utakaokuumiza....advise ya bure kwa wadada.
   
 4. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  we mwana we! angalia utawaponza wenzio.watakaofuata ushauri waje baadae na feedback!!
   
 5. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Ndoa naiona kabisa inavyovunjika hapo lazima tu utamakamata
  halafu itakuaje utaumia roho kwani kuchukua maamuyzi magumu nayo ni ngumu
   
 6. Iselamagazi

  Iselamagazi JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 2,221
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Kazi kweli kweli!
   
 7. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  unataka watu kuwa majeruhi wa mapenzi,,,,,, hahaa na mimi ushauri huu nitauzingatia na nitakua makini na hayo uliyoyasema ili nisije kugundulika kwa mpenzi wangu
   
 8. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mbona wanawake hawaji hapa kumuunga mkono mwenzao? Kwa mtindo huu ndoa zote zitavunjika tu ikiwemo ya kwangu...Hadi Bar, Kazini, facebook e.t.c lol!
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Ndoa hiyo lazima ivunjike!
  Charminglad una wapoteza wenzioz!

  Uko nikuto jiamini
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  charminglady, halafu ukimfunania inakuwaje? Si utakufa siku sio zako bila sababu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Dah my waifu wangu akinifuatilaia hivi naandika talaka.
   
 12. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,267
  Likes Received: 1,419
  Trophy Points: 280


  kama hujiamini na una muda mchafu utafanya haya.
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kusema kweli sijaelewa lengo la kujiingiza katika biashara ngumu kama hiyo anayoshauri charminglady

  Kama ningekuwa mie, ningetumia muda wangu mwingi kufanya vitu vya maana zaidi na pia kumuonesha partner wangu kwamba anao uhuru wa kuitumia freedom yake apendavyo...ila kama anafanya usaliti...haweza kuficha milele!!

  Babu DC!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  hivi wanawake hatunaga kazi za kufanya? for god sake yaani nikaaanze kuchunguza sijui sim fb to hell.............kama sina kazi kabisa bora nioshe gari aisee kuliko haya. binafsi ni bora nikaenda kucheza mziki kuliko kumfuatilia mwanaume unless kama hujawah kutendewa aisee.

  hebu humo majumbani bunini kazi leo panda ukoka kesho ng'oa panda mboga ili ukose muda wa kuwaza haya yanayovunja ndoa.
   
 15. d

  decruca JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hivi wewe, naona huna ndoa so unataka wenzio tuvunje ndoa zetu ili tuwe pamoja. hayo yafanye ww mwenyewe. nilishaapa kifo kitatugenganisha sasa nikiyafanya hayo nikimshika then what next. hebu tuambie tena tukishawakamata tufanyeje labda utaconvice othewise its nonsense kumchunguza mumeo.
   
 16. T

  Tiger JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  naku-support katika hilo.
  Mi nadhani jambo la muhimu sana katika mahusiano ni kuwa honest to your self.
  Kama unampenda mtu, love that person truly.
  Wanasema you will never loose completely if you love truly.
  Hayo mambo ya kufuatiliana kulikopitiliza ni sawa na kuishi maisha ya mtu mwingine wakati you 've got your own life to live.
   
 17. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  desperate situations call for desperate measures... ukitaka kuwa systematic zaidi katika crusade yako ya kumulika mwizi, subscribe upate assistance ya cheaters.com
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Halafu kitu kingine kinachonitatiza ni kwamba, mtu anayetaka kufanya ushushu wa kiasi hicho, je yeye ni msafi sana kiasi kwamba hajawahi kuchepuka??

  Babu DC!!
   
 19. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  hapo chacha hapo!
   
 20. N

  Neylu JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Aaah... Raha nijipe mwenyewe.. Maadam naamini ananipenda na ananijali hilo kwangu linatosha saaana.. Kisa cha kujipa ma presha nikashindwa ku enjoy maisha mie!! Siwezi kuthubutu kumpeleleza mpenzi wangu hata iweje!
   
Loading...