Unataka kujifunza programming?

Unataka kujifunza programming?

Ninahitaji kujua watu wangapi wako interested kujifunza programming na ambao wanahisi wakielezwa kwa kiswahili is better kuliko kiingereza. Kama ndio tupia hapa ungependa kujua nini.

Nafikiria kutengeneza Youtube series kwa kiswahili ambayo itakua na playlists mbalimbali zitakazo waintroduce watu kwenye concepts za Java, Android Programming, C++, C, Javascript, Datastructures, common algorithms, Swift n iOS Programming, na ikiwezekana kutengeneza full apps kuanzia mwanzo kabisa hadi completion.

Nafikiria kuifanya kama weekend project ambapo every weekend nitaupload few videos polepole kama itaendelea it will probably take a year or more kumaliza playlists zote hapo juu, sema nataka kujua kama kuna audience even if its 100 people, najua english tutorials zimejaa.

Ukijibu ingependeza ukisema unataka nianzie wapi, kama huna experience kabisa au hujiamini hata kidogo unaweza sema hujui mi ntajua kua unataka nianze mwanzo kabisa kwenye basics

Hii post ina zaid ya wiki moja, JamiiForums ina zaidi ya members laki tatu, najua uliexpect kuona flow yakutosha ya watu wakikuencourage na kupost comments and their suggestions ndipo uanze kuwork on the project,, kama hivyo ndivyo mzee utasubiri sana na utatufanya tuchelewe kusogea.. kama una skills na ungependa kushea nasi go and make it right now..

i expected hii post ingekuwa na video moja kama demo kwamba the issue will look like this ungekuwa mwanzo mzuri sana.. matatizo yetu yanafahamika saaana hakuna asiyejua kwamba 99% utawachanganya kama hutaanza kwenye basics kwaajili ya beginners .. by the way count me on your side mkuu..
 
Nika hapa bro maana mi ni programmer mtarajiwa shule ishusje hapa
 
Mimi nahitaji kujua tena uanzie mwanzo kabisa maana ufahamu Wangu umepwaya kabisa.
 
Duh! Nilitaka kufanya hiki kitu kwa muda, tatizo ni kwamba huwa sijiamini sana kwenye Kiswahili changu cha hapa kwetu Kenya. NullPointer ubarikiwe sana na Mungu, najua utakua umetumia nguvu nyingi sana kufanikisha hii shughuli, naomba wana jamii mtie subira na kumpa nguvu.

Nimetaka sana kunufaisha jamii, haswa mitaa ya huku Nairobi, kwa kuwafundisha vijana programming kwa lugha wanayoweza elewa vizuri. Inatia moyo kuona kuna mdau ameanza, hii iwe changamoto kwa programmers wote wanaopita humu, kwamba hamna haja ya kwenda kaburini na maujuzi yote haya bila kuachia walau vijana kadhaa wanufaike na kuendeleza.
 
Umesema vyema MK254 lakini na wewe bado unaweza kutoa ujuzi wako na tukaufaidi. Usijali kuhusu kiswahili, kama unaweza kuandika vizuri basi utaweza hata kuongea.
 
Jana na leo, shusha madude mkuu tena kwa kiswahili ndo rahisi kuelewa zaidi
 
#include<iostream>
#include<conio>
void main()
{
int x;
int y;
float z;

cout<<"enter x"<<endl;
cin>>x;
cout<<"enter y"<<endl;
cin>>y;
z=x/y;
cout<<"the results is "<<endl;
cout<<z;
getch();
}
 
#include<iostream>
#include<conio>
void main()
{
cout<<"poa mkuu nitakuwa mwanachama wako"<<endl;
cout<<"naitwa Pure mathematician"<<endl;
cout<<"mkazi wa ukonga"<<endl;
getch();
}
 
Ninahitaji kujua watu wangapi wako interested kujifunza programming na ambao wanahisi wakielezwa kwa kiswahili is better kuliko kiingereza. Kama ndio tupia hapa ungependa kujua nini.

Nafikiria kutengeneza Youtube series kwa kiswahili ambayo itakua na playlists mbalimbali zitakazo waintroduce watu kwenye concepts za Java, Android Programming, C++, C, Javascript, Datastructures, common algorithms, Swift n iOS Programming, na ikiwezekana kutengeneza full apps kuanzia mwanzo kabisa hadi completion.

Nafikiria kuifanya kama weekend project ambapo every weekend nitaupload few videos polepole kama itaendelea it will probably take a year or more kumaliza playlists zote hapo juu, sema nataka kujua kama kuna audience even if its 100 people, najua english tutorials zimejaa.

Ukijibu ingependeza ukisema unataka nianzie wapi, kama huna experience kabisa au hujiamini hata kidogo unaweza sema hujui mi ntajua kua unataka nianze mwanzo kabisa kwenye basics
Mkuu kwa mfano mimi niko Arusha, lakini nahitaji sana kujifunza programming sasa unatusaidiaje sisi wa mikoani?
 
Back
Top Bottom