NullPointer
JF-Expert Member
- Feb 7, 2011
- 3,461
- 2,275
- Thread starter
- #121
language gani nzuri kushinda zote me ndo naanza na java nimeipenda sabab ukikosea inakuonyesha
Hakuna language nzuri kushinda zote, language zote zina strength na weakness zake, kwa hiyo kila language inatumika pale ambapo ina strength zaidi.
Na kusema java inakuonyesha ukikosea, language nyingi zina hii feature, ukicompile kama umekosea inakuonyesha wapi ime~fail. Kama unaongelea "Auto-complete" yaani ile ukiwa unaandika inakuonyesha na majina ya methods, hata languages nyingine zinayo, hiyo siyo feature ya language, ni environment tu unayotumia.
Hakuna kitu special kwenye Java ambacho huwezi fanya kwenye language nyingine, japo ndio, Java ni language moja nzuri sana na inatumika sana.