Hii mada hii. Naungana na waliosema twende na wakati. Nafasi ya mke na mume haijabadilika toka zamani hadi sasa. Bado baba ni mtawala na mama ni msaidizi. Kilichobadilika ni mfumo wa utawala tu - kutoka imla kwenda demokrasia. Sifa za msaidizi wa sasa zimeongezeka ila hazijabadili nafasi yake. Ana elimu na kipato hivyo havumilii vipigo na manyanayaso kisa kwa kwao keshaagwa, wala kurithiwa na shemeji kama zamani. Hata angetaka kurithiwa, mashemeji hawataki, maisha magumu. Hakuna asiyejua mchango mkubwa wa mwanamke kwenye dunia. Mke ni msaidizi, ni mlinzi, ni mshauri wa mumewe. Wababa wenye wake wema wanaweza kushuhudia hili. Ndo maana tunaambiwa tukosee kuchagua magari na viatu ila si mwenzi wa maisha. Ukimpata mtu sahihi wala hakuna mjadala wa nani awe mkia, nani awe kiuno. Kila mmoja anajua nafasi yake. Wenzi sahihi wanaoheshimiana na kupendana wanatambuana madhaifu na nguvu za kila mmoja. Ndo maana utakuta kuna familia shopping anaenda baba kwa kuwa mama hajui kulalama juu ya bei au hana mpangilio. Ikifika wakati watoto wamevuka mpaka baba anasema "mama hili shughulikia wewe maana una uvumilivu, mimi nitaua". wakati wa ujenzi mama anasema "baba hawa mafundi simamia wewe maana mimi hata ratio ya simenti na mchanga sijui, watatuibia tu. Baba naye anasema mimi sina muda zaidi ya wikiendi, basi tutafute mtu mwaminifu anayejua atusaidie kusimamia tumlipe". "baba X kazini kwetu tumeamua kujiunga wanawake sita tupokezane laki kila mwezi. Zitatusaidia ada ya mtoto"..mume anamwambia " sidhani kama hilo ni wazo jema maana hapo katikati kuna watakaopata dharura au kukiuka tu kwa makusudi. Kwa nini usifungue fixed account ukaweka huko hiyo laki kila mwezi baada ya miezi 6 ukaichukua?" Utawala wa aina hii hata msipokubaliana ndoa haitayumba. Penye pendo pana heshima na kinyume chake. Watu wanaingia kwenye ndoa wamejihami utafikiri wako syria! Hizi mali na elimu na tgnp wala havina shida. Ndoa ni jinsi mnavyotaka iwe ndo maana utakuta ndoa mbili zimekumbwa na dhoruba inayofanana, moja inaparanganyika, moja inayumba na baadae kuimarika zaidi. Tupunguze munkari, tuenende kwa hekma.