Unataka heshima? Waheshimu wengine kwanza

lara 1 ni drama queen?....based on the context....I am curious to see her point of view,,,,.Kuwa na amani.hakuna drama..
Did i say that or did you??I think you are missing the big picture!You should probably read my previous thread.
 
Nimekumiss sana Mwalimu.
 
Mada zenye kujenga kama hizi ni nzuri.Watu muache uchonganishi na ucatalyst.
 

Nimeishia Kucheka tu,mama Ngaiza hata ukimwambia umependeza kwake ni unyanyasaji qa Kijinsia.Khaaaaa!!!!!labda aambiwe na mwanamke mwenzie
 
'Its a man's job to respect women but it's a woman's job to give him something to respect'.

Ukiistahili heshima utaipata tu kutoka kwa mwanaume....na wanaume mkiistahili heshima kwa kusimama kwenye nafasi zenu mtaipata pia heshima na upendo kutoka kwa wanawake.

Ni lazima kwenye mahusiano tuvumiliane sana na kuelewana kwa kuwa approach yetu ya ku-deal na changamoto au mikasa ya kila siku ya maisha hazifanani. Binadamu tumeumbwa tofauti sana lakini pia maisha yametufanya vile tulivyo na namna ambazo tuna-respond kwenye changamoto,kukosewa au kufanyiwa kinyume na matarajio. Ni vizuri ukamuelewa partner wako vizuri kabla ya kuona hakuheshimu,kuna watu tu toka amekua au kwa kuwatizama watu wa karibu yao amezoea kuona wakikosewa namna ya kuondoa hiyo hasira ni kutukana au kuongea kwa karaha ila deep down sio mtu mbaya au wahuni....kama anabadilishika na iwe hivyo na abadilishwe kwa upendo na walio karibu nae.

Nina rafiki zangu wapenzi ambao lugha yao huko nyuma ukiisikia unaweza shangaa walikokulia,na ukiwaudhi ni mitusi mwanzo mwisho na kashfa za ajabu but ndani yao sio watu wabaya. Mungu mwema walibahatika kupata wenzi wanaowaelewa na kuwapenda wakijua mapungufu yao na sasa ile kuwa na watu tofauti na walivyo taratibu wakaacha matusi na fitna za ajabu. Nikagundua kuwa elimu haikuwabadili (manake nimewajua kazini) ila kuwa na watu wa tofauti wanaowapenda na wanaokuwa nao muda mwingi karibu kuliwabadili sana maneno,mawazo,mtizamo na hata namna ya ku-deal na mikasa kwenye maisha yao ya kila siku. Nia tu iwepo na uelewa.

Mwisho, heshima ni tokeo la tafsiri/mtazamo wa binadamu mwenzio kwako. Huu mtazamo unajengwa na visababishi mbalimbali kama ufahamu,uzoefu na hata matarajio aliyonayo mtu kwako. Hakikisha huwi sababu ya mtu kukukosea heshima, jitizame vizuri pia kabla ya ku-demand respect.
 
Very wise words,women can change the world but they can't change their position by equalizing themselves with Men kwa kubishana,shouting,kutukana tadharaurika na kuachika milele....You must know your position before shouting back...Wise woman
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…