Unapotaka kuoa, usidharau kigezo hiki

Unapotaka kuoa, usidharau kigezo hiki

chief72

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
627
Reaction score
309
Watu wengi wanapotaka kuoa huwa wanatoa kipaumbele kikubwa kwenye tabia ya yule anaetaka kumuoa, hata kama yeye hana tabia nzuri, hilo huwa muoaji hajali kabisa, lakini katika research yangu yaki-layman nimegundua kuwa uzuri wa unaetaka kumuoa lazima uzingatiwe, sio lazima awe mzuri hadi anaharibu tension za watu, laa!!!!ila kwa kifupi awe ni mtu ambae roho imeridhia na anakidhi haja zako.

Kama wewe unapenda wanawake wenye maumbile fulani au shepu fulani au rangi fulani, basi hakikisha unaoa mwanamke mwenye sampuli hiyo maana kama uta li-ignore jambo hilo basi hutaacha kuruba ruba kwenye ma BAR, na kwingineko kwa ajili ya michepuko, ingawa suala la michepuko ni hulka ya mtu lakini kuna asilimia fulani za watu hawatulii kwa sababu wake zao hawana mvuto na waliwaoa kwa sababu ya tabia zao nzuri.

Naomba nitoe pole kwa wale wote walio oa wanawake ambao nafsi zao haziwakubali hadi inafikia wakati kuongozana nae kwenye harusi au shereh unaogopa ogopa pia hongereni wale ambao mmeoa wake zenu mnaowakubali,hadi mnajiskia raha kiwango cha kudharau kabisa michepuko.
 
Asante sana mkuu kwa hiki kipande kizuri cha ushauri.......UBARIKIWE SANA
 
nafuarahi kupitia hapa ....ntaufanyia kazi
 
Unachagua sana mwisho wa siku unajikuta unaoa kutimiza wajibu
 
Back
Top Bottom