Unapoondokewa (kufiwa) na wazazi wako

Mungu atabaki kuwa Mungu, kifo kipo kila siku lakini kifo hakizoeleki, kifo kisikie kwa jirani.
Kinacho nitia moyo ni BIBLIA. yesu alisema msiogope lazaro hajafa amelala.. japo kua kabla ya kusema maneno hayo yesu alilia kwa uchungu baada ya kuona watu wanavyo huzunika mtu anapo kufa. hiyo inaonesha hata yesu anachukia kifo na hapendi binadamu wanapo kufa.. lakini kwakua tupo katika utawala wa shetani hakuna budi.
 
Nimejikuta nayatafakari kwa kina hayo maneno yako mkuu

Kufikwa kuna uma sana asikwambie mtu hasa kwa mpendwa/wapendwa wetu wa karibu

Nakumbuka siku BABA yangu mzazi anaanga dunia nikiwa namwangalia hivi kwa macho yangu ya nyama

Ilikuwa saa tano na dakika alobaini na tano usiku nikiwa nae hivi kitandani anahangaika kukata roho

Nakumbuka nilitoka mbio kumuita dactari wa zamu tulivyofika tu kwa baba tukakuta ndo anaishilizia kukata roho

Hiyo siku usiku nililia sana hasa alipoanza kugeuzwa shingo kulia na kushoto daktari akasema hatupo nae tena akafunikwa shuka gubi gubi

Kuna muda akaanza kuchomwa sindano za kutoharibika mwili wake

Aiseeee!!wapendwa ni hudhuni mno

Endelea kupumzika kwa amani BABA yangu/yetu mpendwa.
 
Kuna mzee mmoja aliwahi kuniambia kwamba uchungu wa kufiwa na mzazi au wazazi anaujua yule aliyefiwa..
Kisha akaniambia kwamba kama una rafiki aliyefiwa na mzazi au wazazi halafu itokee ukamweleza kuwa unauguliwa na mzazi wako, usidhani atakusikitikia sana....

"Si afe tu ili tufanane" anaweza hata kuwaza hivyo......

Sina uhakika kama maneno ya huyo mzee ambaye ameshatangulia mbele ya haki yana ukweli.

Lakini ninachotaka kusema hapa ni kwamba ni wale tu waliofiwa na wazazi ndio wanaojua uchungu wa kufiwa lakini yule ambaye wazazi wake wote wapo hai hawezi kujua uchungu wa kufiwa.................
100% agreed. Kila msiba unamwenzie
 
hii thread IMENILIZA, NA WOTE MLIOCHANGIA! i have both parents though my mama is seriously sick huu ni mwaka wa 3! hawezi kuongea anaongea kw ishara na akihuzunika au kama kuna kitu kinamuuma hulia! my dad is ONE in a million man! kila anapokwenda huenda na mama, kabla ya kwenda kazini anahakikisha mum kapewa dawa, chakula etc, labda tu niseme kuwa hata kula mum hali kwa mdomo ana mwaka wa tatu pia, amewekewa tube TUMBONI, SO KILA KITU KINAPITA KWA TUBE!

NIMESHALIA SANA, NIMESHAKUWA SUGU, NAMUOMBEA UJASIRI WA KUVUMILIA YOTE NAIOMBEA PIA FAMILIA YANGU TUSHIKAMANE KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUMUUGUZA MAMA MPAKA HAPO MUNGU ITAKAPOMPENDEZA KUMPONYA KABISA!

SIJUI NI KWA NINI, ILA NINA IMANI KUBWAAAAAAA KUWA ATAPONA KABISA! ATAKUJA KUONGEA NA KUWA MZIMA TENA!! poleni wapendwa wote mliopoteza wazazi,. HAKIKA INAUMA SANA, I CAN IMAGINE WHAT U HAVE BEEN THROUGH!! MUNGU WETU AWAPE FARAJA, ATUPE NA SISI MAISHA MAREFU, ILI tuweze kuwalea watoto wetu mpaka wawe wakubwaaaaaaa, na wajukuu TUWAONE! amen!
Mama anaendeleaje
 
Mkuu Mimi nimepoteza wazazi wote wawili..

Mama alikufa 1995 nikiwa bado nipo secondary..
Baba alikufa 2003 nikiwa na utimamu wa akili na shughuli zangu..

Lakini naumia hadi sasa,,,,kumbe nimegunduwa wale ndugu au jamaa adui ya wazazi wangu ,,
wote wamehamishia uadui kwangu..

Utakapofiwa na wazazi ndy wale walimwengu utawaona live..

Ndy maana hata kwenye vitabu vya dini vimesisitiza sana kuwafanyia hisani yatima.

MUNGU ni muweza wa yote,,alijuwa fika kwamba mtoto bila wazazi ni sawa na kifaranga cha Kuku bila mtetea,,
kinapitia mitihani mingi sana kufikia kukua.,
kunguru anamuwinda,,,
paka wanamsaka,,
nguchiro nao wananamtamani,
Mradi tu,,wazazi wake hawapo.

Siku zote yatima hadeki..mkuu.

Sometimes huwa naamka usiku nalia sana,,
tena peke yangu chumbani,,
nikifikiria wazazi wangu,,huwa najiuliza ni wapi wamekwenda?
Na kwanini ndugu wasubiri hadi wazazi wangu waondoke ,,wanifanyie hivi?

Mzazi ni nguzo muhimu sana ktk maisha,,ambao wanakukinga na mengi sana ktk maisha,,haswa ndugu za baba au ndugu za mama..au hata mambo mengine ya kidunia,,mzazi atakulinda na kukutetea na kukutia moyo pale unapoelekea kushindwa.

Yapo mambo mengi ambayo ndugu wa baba au mama watashindwa kukufanyia ikiwa bado wazazi wako wapo hai...pengine wakiwahofia wazazi wako.

Siku wakiondoka ,,basi ndy hapo utawaona wale walimwengu halisi..watakufanyia watakavyo na hutoamini.

wanajuwa huna nguzo yeyote ya kuegemea,,na huna kwa kushika
wala huna mtu wa kukusimamia jambo lako lolote ,,kama wangekuwapo wazazi wako ..

Hakuna ndugu atakayekupenda wewe zaidi ya wazazi wako...
Watakuchekea wazazi wakiwapo,,,
Wakiondoka wazazi hutoamini kitakachofuata.

Mzazi ni mzazi hata awe Chizi,,
siku akiondoka,,utaona umuhimu wake..
Mungu awasamehe ,,walale salama wazazi wangu..
Ameen.
 
Doh pole sana mkuu
 
nlifiwa na mama nikiwa na 5 years, sura siikumbuki vizuri sahivi niko 20+
 
Mchambuzi, ukifiwa na wazazi unakuwa kama umepooza. Unajua, toka wazazi wangu wafriki huwa hata sisikii uchungu sana mtu akifiwa na wazazi wake. Nachukulia kawaida lakini si kwa minajili kuwa tufanane, la hasha, bali ni kuwa unakuwa hujielewi!
UPO SAHIHI
 
Doh pole sana mkuu
Tena mama ananitoa machozi zaidi ,,
maana siku anakufa alinambiya ,,mwanangu kesho usikose kuniletea shuka ,,
nenda kwa bibi yako niletee shuka..

Mm niliamka asubuhi mama anaumwa ila alikuwa na matumaini ya kupona..hakuwa serious sana.

Akanisisitiza tena Jana nilikwambiya niletee shuka,,hii siitaki...nenda kwa bibi yako.

Nilitembea umbali mrefu kufata shuka kwa bibi,,
Kufika kule nakuta watu wote wapo nje,,,barazani kama wanajadili jambo.
nauliza bibi yupo wapi?
Naambiwa kaenda kule nyumbani nilipotoka,,

Nikauliza nimetumwa shuka na mama,,

Wakajibu,,
bibi kishaondoka na shuka tayari,,wewe rudi nyumbani..

Mkuu huwezi amini.
Nikiwa njiani narudi,,kama kuna mtu anaongea na Mimi kwenye akili yangu..

Hivi mama yako akifa. .utaishije bila mama?
Basi nikapata hisia kama mama keshakufa tayari,,
Kama nusu saa nilipata mawazo yale yale,, na swali linajirudia..
Na sikupata majibu.

baadae nikarudi ktk hali ya kawaida kwamba labda ni hisia tu..

Kufika karibu na nyumbani nakuta mtaa mzima unaniangalia Mimi kama wananishangaa hivi.

Sikuhitaji kuambiwa,,tayari nikapata hisia kamili mzazi wangu,,katangulia,,
Mbele ya haki...

Lile swali lililonijia hivi mama yako akifa utaishije bila mama?
Kumbe lilikuwa la maana sana..
Mpaka leo najiona kwann yule mtu aliniuiza swali lile..
Kumbe ilikuwa ni really kabisa..lile swali ni jibu la ndugu wa mama wanayoyafanya kwangu Leo.
Najiona kama nimetengwa,,na sina mtetezi.
Huwa najiuliza mama angekuwapo wasingenifanyia hivi.

MUNGU amsamehe mama yangu huko alipo...
 
Back
Top Bottom