Unapofuta namba ya simu......

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Hii huwa inatokea sana, alafu mtu akipigiwa simu huwa zinakuja sababu za "nimerenew line" au "nimepoteza simu". Kumbuka hawa wafuta namba wengine ni marafiki tu. Ninachojiuliza> inawezekana watu huwa wanakuwa na malengo gani wanapochukua namba na kuifuta baada ya siku chache? Nawasilisha.
 
Kupoteza simu kupo na wengine wanazuga2,wakishakuchoka labda huna jipya au wanakuona unapoteza mda wao ukipiga huna lamana.
 
mara nyingi huwa sio kweli huwa tunapoteza au ku renew namba za simu, hii hutokea kwa sababu maalum unakuta unaifuta namba ya simu ktk phonebook yako, hata mimi huwa ninafanya hivyo ninapoona mtu anakua msumbufu au anakua analeta mambo fulani ya kutangaza njaa kila wakati
 
Dharau, unaweza ukawa umesoma na rafiki yako wa damu, siku inatokea kapata kazi nzuri kuliko ya kwako hata kukupigia simu taabu, atakuona kama hutakuwa na jipya kwake, we ukitosa ukampigia sababu ndo zinakuja ohh nilipoteza simu nika renew line, mara oohh nilibadilisha simu na nahisi namba yako ilikuwa kwenye scean ya ile simu ya mwanzo, mara ooh simu yangu sijui ina tatizo gani, haionyeshi majina ya watu.........
Wakati niko na yeye karibu mbona haya matatizo hayakuwepo?
Walahi kwa jinsi hii kitu inavoniboa, mtu ambae alikuwa rafiki yangu nikimpigia simu akaniuliza nitakachokifanya na mimi ni kuziondoa za kwake!!!
 
Haya mambo yapo sana na mtu anajikuta anasema uongo bila sababu ya msingi.though i also do.make unakuta mtu we ndo umpigie tu usipomtafuta hata mwaka hajigusi asa mi nsifute namba yake namfuga?
 
mara nyingi huwa sio kweli huwa tunapoteza au ku renew namba za simu, hii hutokea kwa sababu maalum unakuta unaifuta namba ya simu ktk phonebook yako, hata mimi huwa ninafanya hivyo ninapoona mtu anakua msumbufu au anakua analeta mambo fulani ya kutangaza njaa kila wakati
lakini kufuta ni suluhisho? Si bora umwambie ukwel kwamba hutak mawasiliano naye?
 
Kwa mtazamo wangu simu tunazitumia ili kuwasiliana na watu tunaowaona ni wa muhimu/msaada kwetu...
Binafsi nikimpigia mtu simu mara huwa najitambulisha hata kama tulishawahi kubadilishana namba...
Najua kuwa anaweza kuifuta au hata kutokuhifadhi namba yangu kulingana na anavyonichukulia..
Manake siya lazima ahifadhi namba yangu ilhali mimi ndiye nina mahitaji naye/kwake..

Hivyo siyo lazima sana kuhifadhi namba ya mtu wakati huoni kama kuna jambo linalokulazimu uwe nayo...
 
Hii huwa inatokea sana, alafu mtu akipigiwa simu huwa zinakuja sababu za "nimerenew line" au "nimepoteza simu". Kumbuka hawa wafuta namba wengine ni marafiki tu. Ninachojiuliza> inawezekana watu huwa wanakuwa na malengo gani wanapochukua namba na kuifuta baada ya siku chache? Nawasilisha.

Mimi ukiwa unanibeep beep sana huwa naifuta namba yako maana ni usumbufu.
 
wengine nyodo tu zinawasumbua, anadelete namba, nikigundua umenidelete nami na kudelete
 
Kwa mtazamo wangu simu tunazitumia ili kuwasiliana na watu tunaowaona ni wa muhimu/msaada kwetu...
Binafsi nikimpigia mtu simu mara huwa najitambulisha hata kama tulishawahi kubadilishana namba...
Najua kuwa anaweza kuifuta au hata kutokuhifadhi namba yangu kulingana na anavyonichukulia..
Manake siya lazima ahifadhi namba yangu ilhali mimi ndiye nina mahitaji naye/kwake..

Hivyo siyo lazima sana kuhifadhi namba ya mtu wakati huoni kama kuna jambo linalokulazimu uwe nayo...

Umesema kweli mkuu
Ila kufuta no za simu inategemea kuna no ya mtu unakaa nayo kwenye simu yako mwaka mzima hajawahi hata kukukumbuka na sometime wewe umemtumia hata sms ila hujawahi kupata majibu na siku umempigia ndo anaanza kukuambia mbona umepotea sana wakati hajawahi kukutafuta sasa no ya mtu kama huyo inakaa kwenye simu ya kazi gani
Wengine kazi ni kubeep na kutuma zile sms za tafadhali nipigie au recharge me au kupiga mzinga kila anapokukumbuka sasa no ya mtu kama hiyo niihifadhi ya kazi gani
Kuna mengi sana yanayochangia ikiwemo poa dharau kila ninapokupigia simu ni lazima uulize wewe ni nani hata kama within a short period ni lazima uulizwe the same qn sasa hapo unaona kuwa yeye anaona hana haja na no yako so wewe utaihifadhi ya kazi gani
 
Hii huwa inatokea sana, alafu mtu akipigiwa simu huwa zinakuja sababu za "nimerenew line" au "nimepoteza simu". Kumbuka hawa wafuta namba wengine ni marafiki tu. Ninachojiuliza> inawezekana watu huwa wanakuwa na malengo gani wanapochukua namba na kuifuta baada ya siku chache? Nawasilisha.

Nahisi naonekana mbaya ila nasemaga 'nilifuta namba yako, nani mwenzangu' ...hata mtu akikata simpigii!!..muda mwingine inabidi nifute namba zilizojaa kwenye simu bila sababu na hakuna mawasiliano ya zaidi miezi 6..simu kuwasiliana siyo kutunza namba!! Huwa sikasiriki mtu kufuta namba yangu yasimu pia!!
 
sometimes mtu anabadili handset na anakuwa hajakopi namba zote kutoka kwenye ile simu ya zamani...
 
Mie sifuti namba ya mtu yeyote, huwezi jua mbeleni unaweza mhitaji kwa jambo fulani na kuanza kujuta
 
Mie sifuti namba ya mtu yeyote, huwezi jua mbeleni unaweza mhitaji kwa jambo fulani na kuanza kujuta
kweli inaweza kutokea ukaiitaji. Mimi huwa nafuta nikigundua kwamba kuna one way communication.
 
number inafutwa kama haina maana yoyote....nakumbuka ndugu yangu mmoja kila nikimsms eti anauliza wewe nani? unamwambia anaomba msamaha eti simu ilipotea, after sometimes ukimtafuta anauliza tena..kama mara nne hivi...je kuna umuhimu wa mimi kukaa na number yake? NAFUTA na hata nikihitaji msaada kwake na imagine kama hayupo vile...
 
Nini kujaza jaza manamba usiyoyatumia kwenye simu?kuwa black and white,ndio hawa watu wanakaa na makopo ya losheni yaliyoisha chumbani
 
Back
Top Bottom