Unapodai bila mafanikio tumia njia mbadala

Think Hard

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
318
Reaction score
307
Endelea…

Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea pesa zangu.

Baada ya wiki moja nampigia simu hapokei simu zangu, nimempigia zaidi ya mara kumi (10) bila ya mafanikio!

Kila nikimpigia simu hajibu simu zangu, nikahamua kumwandikia message kwa WhatsApp...!

_Hello Mamu, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba Ngina). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama ana akili nzuri._

--
_*Kisha nikaituma ile message*_

Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu nami wala sikupokea simu yake... Akapiga tena na tena kama mara ishirini hivi wala sikupokea.

*Akatuma message akiniuliza...*

_Hao wanawake unawajuwa, ...mume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, wewe unawajuwa hao wanawake waliopigana, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweli...!_

Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaa...!

Akanipigia tena simu mara tano, sikupokea simu zake, kimyaaa...! Akaniandikia message nyingine....

*...Nakupigia jamani pokea simu basi nina pesa zako nataka nikupe... Naomba basi tukutane mjini unihadithie vizuri...!*

Nami nikamjibu...

_Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa, ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke mahala walipo...!_

Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza pesa zangu zote ninazo mdai...!

Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaa.... Kama sio mie!

MJINI SHULE....
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Hiyo kweli mbinu shirikishi, ila ungemsaidia tuu kuokoa ndoa yake kwa kumwambia ilikua ni mbinu ili ulipwe pesa zako.
 
!
!
akili kubwa mno hii.
 
Nina mdeni wangu ni mdada tu sio mke wa mtu. Hivi nafanyaje anilipe pesa yangu?
 
Huyo hela alikuwa nayo..sasa huyo dada asingekuwa na mume huoni kama ingekuwa mission failed
 
Back
Top Bottom