Unapenda hotuba ipi ya Hayati Nyerere au ya JK ya sas? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unapenda hotuba ipi ya Hayati Nyerere au ya JK ya sas?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mkulimamwema, May 5, 2011.

 1. m

  mkulimamwema Senior Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku moja nikiwa stendi ya daladala ubungo pale kuna jamaa walikuwa wanabishana :Mmoja alidai ni kheri asikilize hotuba za mwl za 1970 kuliko za JK hata ikiwa ni live,sasa mimi nawauliza wanajamii nanyi mtoe majibu yenu hotuba ipi tukiitekeleza italeta maendeleo ya mwl ya 1967 juu ya azimio la Arusha au ya JK akifungua bunge la kumi mwaka jana mjini Dodoma?
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  .. Uwezo wa kumpiga tunao,
  ... Sababu ya kumpiga tunayo,
  ... Tunataka dunia ituelewe hivyo...

  Baada ya hapo tukaelekea Mtukula!!!
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sio mtu unashauliwa na mkeo usiku .................
   
 4. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  na sasa tunaelekea kutafuta vijana wenye hotuba zenye mvuto.
  ubalozi wa vijana umeandaa shindano hilo.
  nategemea kuwaona vijana wenzangu tukisimama nao kuonyesha uwezo wa kutoa speech zitakozodumu miaka 50 ijayo.


  kwa jk II, hakuna kipya wala cha 'kukoti'
  bt mzee wa butiama kila mwisho wa msitari ni moto.
   
 5. m

  mkulimamwema Senior Member

  #5
  May 5, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mimi ndio mtoa hoja ila ni tamu nisipoonyesha upande wangu nitakuwa nainyanyasa nafsi yangu,mimi ningesikiliza za mwanaume Nyerere kwa sababu alikuwa anatekeleza anachosema nitatoa mifano:Kabla hatujaanza kumpiga Nduli Idd Amin Mwl alitangaza ushindi kama ifuatavyo na ikawa hivyo na tukashinda"UWEZO WA KUMPIGA TUNAO,SABABU YA KUMPIGA TUNAYO NA NIA YA KUMPIGA TUNAYO TUNAOMBA DUNIA ITUELEWE HIVYO"hayo ni maneno ya RAIS wa watu aliyekwenda ikulu kufanya kazi na ikawa hivyo lakini naye JK alisema hivi mwaka 2005"MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" akisindikiza kwa chorus ya Ari mpya,nguvu mpya na kasi mpya watanzania wakajua mwanaume mwingine amekuja ikulu na maisha bora ni baada ya miezi mitatu tu kumbe ni hewa bwana na hizi kauli harudi tena-Heeeeeeh kidumu chama chetu
   
 6. m

  mkulimamwema Senior Member

  #6
  May 5, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Samahani Nyakarungu naomba unipe details za kutosha juu ya hayo mashindano ya hotuba nina kijana wangu nataka nimpeleke yanafanyika wapi,wanajiandikisha wapi?
   
 7. VISIONEER

  VISIONEER Senior Member

  #7
  May 5, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nchi yetu haina ubaguzi, hatumchagui mtu kwasababu ya dini yake
   
 8. m

  muraweto Member

  #8
  May 5, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  babu nyerere mzee wa vitendo huyu jk kazi yake vijembe!!!!!!! sasa vijembe vina utekelezaji? ndo maana hana jipya kwa kipindi chake chote sijui atakumbukwa kwa lipi! bora mkapa tunamkumbuka kwa kujenga barabara kwa kiwango alichoweza? huyu jk katiba tu imeisha mtoa jasho.
   
 9. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,147
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Jk wa maisha bora kwa kila mtanzania yaani we acha tu.. Chondechonde msijaribu kabisa kumfananisha na mzee wetu wa butiama,hadi watoto wanamdauti pindi wanapokaa chini ya mti badala ya darasani,ila mcheshi na mwingi wa tabasamu...
   
 10. N

  Nonda JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mimi nimeipenda hii. Aliitoa Bungeni 1994 alipozima hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano.

  Muundo wa Muungano, pamoja na kwamba hatutaki uwe ukitibuliwatibuliwa mara kwa mara, ni suala la sera, si amri ya Mungu. Uk 18


  “Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. Wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki iliyoungana kuwa Nchi Moja. kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili.” Uk 11

  Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Wala hakuna haja ya kulinganisha hotuba za muungwana na Mwalimu, hizi za siku hizi hadi aandaliwe yake ni kusoma tu wala hazina mvuto!
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hotuba hazishibishi kaka. Ingekuwa hivyo mbona tungeshiba makapi ya jk? Hotuba zina sababu na wala si kukaa na kutunga cha kuongea. Kadhalika huwezi kumshindanisha nyerere na huyu dogo no matter ni muda gani umepita
   
Loading...