Unamshaurije huyu dada?

Mimi ni msichana wa miaka 20 naishi magomeni jijini dar nimejitokeza kwenu kushare tatizo langu. mimi sina wazazi wote walifariki kwa ajali ya gari mwaka 1998, Mimi waliniacha nasoma shule ya msingi. Sasa baada ya kumaliza nilifanikiwa kujiunga na sekondari nilisoma hadi form 4 nikamaliza pia nikapass mitihani yangu. nikatakiwa kidato cha tano,kabla sijaenda shule nilibahatika kupata mchumba muuza genge na akaahidi kunisomesha kwani mimi nilikosa ada. Nashukuru mungu kanisomesha hadi chuo kikuu na nimemaliza hadi sasa nimepata kazi yangu. siwezi kuishi na muuza genge hata siku moja kwanza hajui kuvaa akapendeza pili hana elimu.Sasa je nifanyeje kumwambia ukweli kwamba mimi siwezi kuishi na yeye bila kuumiza moyo wake.
"NIMEIKUTA MAHALI NIKASHIKWA NA BUTWAA NIKASHINDWA KUCOMMENT .........HIVI MTU KAMA HUYU UTAMSHAURI NINI!!"

**** u bitch..!
 
ewakati ule ulimuita mchumba sasa unamuita muuza genge! basi usimuonyeshe kuwa humpendi tafuta namna utakavolipa fadhila unaweza kushawishi aongeze elimu kwa kumlipia pia unaweza kumwongezea mtaji au hata ukamjengea kajumba au kumnunulia ka stalet lakini ukimwacha taratibu bila kumdhalilisha
 
Hamna kitu hapo; cwezi poteza muda wangu kukoment kitu cha kupika kiac hicho na kwa umri huo kwa hapa kwetu tz huwezi kuwa na degree...kwaherini wanajf!!!!

Hapo umefanyaje?? au umepost?? ...... sio kosa lako!! ni ID yako.
 
Hapo kweli mkuu Maprosoo, tena mfano ukumfungilia biashara anaanza kupendeza wajanja wanaanza kumuona sasa hapo ni kumwachia mungu tu kama ni wako atakuwa wako kama sio ndio imekula kwako

Kwa mademu wa siku hizi walivyokua vicheche ukimwachia mungu aisaidii!! atamegwa mpk basi.
 
Whenever I get a chance, huwa nasema ukitaka kumsaidia mtu, msaidie bila kutegemea kurudishiwa chochote. Kumsomesha mwanamke ili baadae awe wako ni kujitafutia maumivu tu hasa hasa ukiwa masikini. Mtu yeyote akipata elimu, anajiona yupo kwenye class nyingine na atahitaji watu wa class yake ili wa-fit in together.

Bora ujielimishe wewe kwanza, then mpeleke yeye.
 
Haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah, inauma sana, jamani watu hawana aibu wala huruma. Imagine ingekuwa ww ungefanyaje?
 
Aisee :D

-"Wanawake wenye akili zao huwa hawadate wadogo zao au watu ambao wana hadhi ya chini yao."-

.......Swahiba, is this really coming from you au ni usingizi tu ulikupitia?

No wonder wanaume wengi wenye mawazo pumba hawakubali wake zao kujiendeleza kielimu na hata kuchukia wake zao wanapopata mafanikio ya kikazi au kibiashara (uanaume wao usijeshuka hadhi!)

Imekushangaza hiyo swahiba wangu Mbu??

Najua kuna watu wengi wanaweza kuwa wamekwaza na hiyo kauli...ila nakuhakikishia mkuu kwamba huo ndiyo ukweli mchungu....

Ni mifano hai kibao...I wish I could narrate some of them...

Na kama huamini au mtu yeyote ana doubt kuhusu hiyo basi afanye utafiti wake aje na data za kutosha ku nullify hiyo theory....but I personally buy it with sufficient empirical evidences ...za uzoefu na data!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
JF ni kiboko, naona umeanza ku-link matukio na umri na kugundua haiwezekani ni kisa cha kutunga, but all in all kabla ya kuingia kwenye committment ya kumtunza mtu lazima mjiulize kitu gani kinachowafanya kushindwa kuingia kwenye ndoa sasa huku anasoma chuo na badala yake unaacha mpaka anamaliza chuo wakati hata kama walikuwa hawatambuliki kama wanandoa but still walikuwa karibu kama mtu na mpenzi wake kitu ambacho kinawezekana kabisa wakawa karibu kama mke na mume huku anasoma.

Kama muuza genge ameweza kumsomesha mpaka akafika chuo kikuu maana yake huyu jamaa na skill ya ujasiamali hivyo kuna possibility kabisa kama atatumia degree yake na kumbadilisha mpenzi wake kutoka kuuza genge na kufanya biashara nyingine ambayo mwanamke ataona ni ya hadhi yake (na hii ndio kazi ya msomi na si kuwa na cheti na kutegemea kuajiriwa tu). hata hao anaoona wanaendana akifuatilia miaka 6 nyuma ukute walikuwa warugaruga tu kwani sifa ya binadamu ni kubadilika hivyo hata huyo muuza genge ana nafasi ya kubadilika na wakaendana (kila kitu kinawezekana mbele ya fedha)


Inawezekana unachosema kina ukweli....ila ni kwa nadharia zaidi....

Kama huamini ni sawa tu..ila ukweli ni kwamba wanawake wanapata shida kuvumia kuishi kwenye ndoa na mtu wa hadhi ya chini yake....Mtaani atasema unapaka shombo au unamtia aibu....Hawezi kutoka na mtu wa namna hiyo na kwenda naye kwenye high profile meeting au party....., Graduate na muuza genge wapi na wapi jamani??

Tuwapende tu, ila huo ndiyo ukweli kuhusu mama/dada/binti/wajukuu zetu.....!

It is a bitter fact....but it is still a fact!!

Babu DC!!
 
Aisee hapo patachimbika jamaa hatomwelewa kabisa huyo dada tena huo ni utapeli,kingine mamen mwanamke is undifined leo yuko fresh kesho anakutia maumivu yani hasa kabila la ........................hakishajua kuna mali atakupa fake love mwisho anaweza kukuua hata kama mna watoto xo careness ni muhim kwa hawa watu!!!nawasilisha!!

Mbona wapo wanaume kibao wanafanya mambo ya namna hiyo??

Hebu soma huo mfano hapo chini.....

Hii mada imewaumiza sana wanaume ila nadhani ni kwa sababu binadamu wengi tunatawaliwa na ubinafsi (selfishness). Vinginevyo, kila mtu anaweza kufanya mambo ambayo wengine wanaona ni upuuzi bila kujali jinsia yake!!


Ukistaajabu ya musa utaona ya Firauni!!!! Wanawake, wanawake, wanawake!!!! Hivi pia haijawahi kutokea mwanamke akamsomesha mume wake, mwishowe mwamaume anamwona mke ni tambara bovu?

Nina kesi moja ya mwanaume ameajiriwa tena Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano ambaye mke wake alijinyima akawa anamlipia sehemu ya ada akiwa anasoma dedree ya pili. Ila tu mwanaume yule hakuwa na uungwana na mkewe. Kwa sasa baada ya kupata mafanikio na kuanza ujenzi, au kama ameshamaliza basi akachukua wanawake wengine lukiki na sasa hata mke mwenyewe kashatimuliwa na watoto watatu!!! Sasa anajiandaa kufunga ndoa na kidosho wa mjini ambaye hakuwahi hata kumsaidia!!

Kwa hiyo haya mambo yako pande zote mbili!! Ndiyo maana siku hizi ndoa nyingi ni kwa machale sana!!! Hakuna mwanaume au mwanamke anajitoa full kwako!! Huo ndiyo ukweli, wanandoa wanachekeana kiunafiki ili siku zisonge tu!!

Hilo ndilo ambalo baadhi ya wachangiaji wamelisahau....

Hata wanaume wanafanya mambo ya kuwaumiza wake zao ambao wamehangaika nao enzi zao kusota kusaka maisha.

Huyu msichana ni very right. Kusema kweli tangu awali hakumpenda muuza genge. Alitaka pesa za kulipia masomo yake. Hakuwa na njia nyingine ya kufanya. Alipojitokeza muuza genge aliyekuwa tayari kukidhi haja yake ya kusoma ilikuwa ahueni yake. Hapakuwa na mapenzi pale. Muuza genge alitakakumdhalilisha mtoto yule kutumia pesa yake ya genge. Msichana yule angekubali kuolewa naye kabla ya kumaliza masomo, angemharibia. Mtoto wa kike alimwambia SIDANGANYIKE. Subiri ni some. Baada ya masomo anatoa maamuzi ya kiutu uzima.
Muuza genge na graduate wapi na wapi?
Kama muuza genge angekuwa na busara angemwambia aendelee na ustarabu, ikiwezekana amkumbuke katika ufalme wake


That's my word!!

Babu DC!!
 
Yaani hizi ishu ni nyingi sana mi si shangai c'z kuna rfk yangu yeye alisomeshwa na fundi kinyozi kuanzia form one mpaka six kwa sababu wazazi wake walikuwa wamefariki akawa analelewa na ndg tu isitoshe uwezo ulikuwa mdogo sana wa huyo ndugu yake. Sasa alipofika chuo akaanza kumzingua jamaa, mwisho ikabidi amwambie kwa elimu yangu ya chuo siwezi kuwa na fundi kinyozi Ikabidi jamaa amwambie poa lkn nikisema unirudishie gharama zangu ntakuwa najifedhehesha endelea na maisha mama Kijana alikuwa alikuwa anachekwa mtaani balaa, washikaji wenzake wakawa wanamwambia hy hela ni bora ungefungua Baba Shop. Amekuwa hana jinsi, hivyo wameachana.
 
hastahili kutolewa kafara.
Fanya uchunguzi kidogo, utagundua kuwa zaidi ya 70% ya wanawake ambao wamesaidiwa na mabwana wanaotafuta riziki kwa tabu, huwa wanawakimbia hao mabwana mara baada ya mambo ya hao wanawake kuwa super sana.
Ukiwauliza kwa nini? Wanakwambia hatuendani. Ukiwauliza mbona ulikuwa nae kwa mingi tu hukuliona hilo? Hawakupi jibu la kueleweka.
Hii imeshatokea kwa watu wengi tu, sio kitu cha kushangaa wala kushtuka.

Solution ni kuwa mwangalifu tu wakati una-invest kwa mwanamke, na utambue anaweza akabaki na wewe au akala kona baada ya kufanikiwa hivyo uandae jinsi ya ku-ease the pain.

Kwa upande wangu nita-invest kwa mwanamke mwenye mtoto wangu manake hata akikimbia atalea mwanangu.

exactly! Hiyo ndo principle yangu
 
Mimi ni msichana wa miaka 20 naishi magomeni jijini dar nimejitokeza kwenu kushare tatizo langu. mimi sina wazazi wote walifariki kwa ajali ya gari mwaka 1998, Mimi waliniacha nasoma shule ya msingi.

Sasa baada ya kumaliza nilifanikiwa kujiunga na sekondari nilisoma hadi form 4 nikamaliza pia nikapass mitihani yangu. nikatakiwa kidato cha tano,kabla sijaenda shule nilibahatika kupata mchumba muuza genge na akaahidi kunisomesha kwani mimi nilikosa ada.

Nashukuru mungu kanisomesha hadi chuo kikuu na nimemaliza hadi sasa nimepata kazi yangu.

Siwezi kuishi na muuza genge hata siku moja kwanza hajui kuvaa akapendeza pili hana elimu.Sasa je nifanyeje kumwambia ukweli kwamba mimi siwezi kuishi na yeye bila kuumiza moyo wake.

"NIMEIKUTA MAHALI NIKASHIKWA NA BUTWAA NIKASHINDWA KUCOMMENT .........HIVI MTU KAMA HUYU UTAMSHAURI NINI!!"[/QUOTE
Haya yanatokea sana USA mtu anabeba mzigo kusomesha mtu halafu mwanamke akigraduate tu bye .shoga Angu alimfanyia boyfriend wake hayo.
 
This is bad. ni vyema bint ajiulize kwamba asingekuw huyo muuza genge angekuwa wp leo? Asimsaliti coz anaweza kum badilisha mwanaume kifedha na wakawa na gd life
 
wee dada unaona umefanya fair eeh? kwani elimu ya chuo kitu gani.angalia.TAKE CARE B4 THINGS GET WORSES
 
mimi ni msichana wa miaka 20 naishi magomeni jijini dar nimejitokeza kwenu kushare tatizo langu. Mimi sina wazazi wote walifariki kwa ajali ya gari mwaka 1998, mimi waliniacha nasoma shule ya msingi.

Sasa baada ya kumaliza nilifanikiwa kujiunga na sekondari nilisoma hadi form 4 nikamaliza pia nikapass mitihani yangu. Nikatakiwa kidato cha tano,kabla sijaenda shule nilibahatika kupata mchumba muuza genge na akaahidi kunisomesha kwani mimi nilikosa ada.

Nashukuru mungu kanisomesha hadi chuo kikuu na nimemaliza hadi sasa nimepata kazi yangu.

Siwezi kuishi na muuza genge hata siku moja kwanza hajui kuvaa akapendeza pili hana elimu.sasa je nifanyeje kumwambia ukweli kwamba mimi siwezi kuishi na yeye bila kuumiza moyo wake.

"nimeikuta mahali nikashikwa na butwaa nikashindwa kucomment .........hivi mtu kama huyu utamshauri nini!!"

yani huyu dada ndio aone aibu mwenzio na genge ndo kafanya umesoma badala ya kumbadili na yeye akae kisomi eti unataka kumkimbia utalaaniwa wewe tabia gan hiyo dada mwenzio kaumia ajili yako
 
Inawezekana unachosema kina ukweli....ila ni kwa nadharia zaidi....

Kama huamini ni sawa tu..ila ukweli ni kwamba wanawake wanapata shida kuvumia kuishi kwenye ndoa na mtu wa hadhi ya chini yake....Mtaani atasema unapaka shombo au unamtia aibu....Hawezi kutoka na mtu wa namna hiyo na kwenda naye kwenye high profile meeting au party....., Graduate na muuza genge wapi na wapi jamani??

Tuwapende tu, ila huo ndiyo ukweli kuhusu mama/dada/binti/wajukuu zetu.....!

It is a bitter fact....but it is still a fact!!

Babu DC!!

Kiukweli ni nadharia tu mkuu kama ulivyo note ila kama alifikia hatua ya kumvulia chupi muuza genge kipindi hicho sijui alikuwa anamwonaje. Niliweka hiyo nadharia based on uzoefu wa wanawake ktk kuwabadilisha wanaume hasa kwenye mavazi, unaweza ukajifanya hupendi kuvaa suti au kuchomekea lakini atatumia kila mbinu mpaka utabadilika na kuanza kupigilia pamba ambazo ulikuwa huzipigi pia nikaangalia huyo muuza genge kama amesomesha mtu chuo kikuu wakati wajanja wa mjini ambao wanaonekana wana hadhi kutoa service kwa mrembo ni issue basi kwa namna ama nyingine alikuwa ana possibility ya ku-grow kibiashara. (KIUKWELI MWANAUME WA UKWELI ATACHUKUA MWANAMKE AMBAE ANAMWONA YUPO NDANI YA UWEZO WAKE KIFIKRA NA OTHER ISSUES NA KAMA AMEMZIDI BASI LAZIMA NA YEYE YUPO KATIKA MCHAKATO FLANI WA KU-MOVE TOKA HATUA MOJA KWENDA NYINGINE NA WAKATI MWINGINE DEMU ANAWEZA KUKUBALI UKAJIULIZA MARA MBILI MBILI MWISHO WA SIKU TUTAISHIA WAPI MAANA ULIPOMTOKEA NA WEWE THE WAY MUONEKANO WAKO ULIVYO AKAJUA NI INTELLECTUAL FLANI KUMBE KILAZA MJANJA WA MJINI NA MUDA MCHACHE UJAO ANAKUKAMATA KATIKA MAZUNGUMZO YA KAWAIDA ANAGUNDUA UPO SHALLOW)

Ni kweli tuwapende ila sometimes na wao ndio maana wanatendwa kwa kupenda kuchagua partner ready made ambao miongoni mwao kuna ambao wana hadhi kweli na kuna ambao pretender akija kugundua ameshanasa na amekabidhiwa zawadi ya mtoto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom