OMKEIT 93
JF-Expert Member
- May 12, 2026
- 226
- 323
Kuna swali ningependa kila anayesema “Simwamini Allah” au anayekanusha kwamba Allah ndiye Muumba wa mwanadamu alijibu:
Kama Allah si Muumba wako, nani aliyekuumba? Na kama humkubali Adam kuwa mwanzo wa kizazi cha mwanadamu, kwa nini bado unajiita mwana wa Adam?
Qur’an iko wazi kuhusu jambo hili.
Allah anasema:
“Hakika mfano wa Isa mbele ya Allah ni kama mfano wa Adam. Alimuumba kwa udongo, kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa.”
(Qur’an 3:59)
Na Allah anasema:
“Na kwa hakika tulimuumba mwanadamu kutokana na kizalio cha udongo.”
(Qur’an 23:12)
Pia anasema:
“Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni kutokana na nafsi moja, na akaumba kutokana nayo mwenza wake, na akaeneza kutoka kwa wawili hao wanaume wengi na wanawake.”
(Qur’an 4:1)
Hivyo Qur’an inatufundisha kwamba Adam ndiye mwanzo wa kizazi cha mwanadamu, na kizazi chake kikaendelea kuenea duniani.
Ndiyo maana Allah anawaita wanadamu:
“Enyi wana wa Adam!”
(Qur’an 7:26, 7:31, 7:35)
Kwa hiyo kama mtu anasema “Mimi si mwana wa Adam”, basi atuambie anatoka kwa nani.
Na kama anasema “Adam hakutengenezwa na Allah”, basi swali linakuwa:
Adam alitoka wapi? Nani aliyemleta kuwepo?
Na kama mtu anazungumzia evolution, tusipotoshe mjadala kwa kusema “sayansi inasema mwanadamu alitokana na nyani wa leo.” Evolutionary biology huzungumzia common ancestry, si kwamba mwanadamu wa leo alitokana moja kwa moja na sokwe wa leo.
Lakini swali letu kwa mtazamo wa Qur’an linabaki:
Mwanadamu wa kwanza ni nani, na nani aliyemuumba?
Qur’an inatoa jibu:
Adam — ameumbwa na Allah.
Allah ndiye Muumba, Adam ndiye baba wa mwanadamu, na sisi ni Bani Adam — wana wa Adam.
Sasa mwenye kupinga haya aje na ushahidi wake.