Unamfahamu mnyama Squirrel

Unamfahamu mnyama Squirrel

Wafahamu SQUIRRELS, wanyama wadogo ambao Dume ndio hulazimishwa na jike kipindi cha Mating.


Hawa ni wanyama wadogo wanaopatikana sehemu zote hapa duniani, ila hapa Tanzania sijui wanaitwaje (tusaidiane hapo hata kwa kilugha
).[emoji23]


Ni wanyama wanaoishi katika makundi madogo yaani dume, jike na mtoto, Mara nyingi wanaoishi ardhini huchimba mashimo mfumo wa tanuli na kuishi humo. (huku hamna kuishi na wajomba wala shangazi kama kina nguchiro ).


Na wale waishio juu ya miti pia hutengezeza viota juu ya miti na kuhakikisha hakuna predator anayekuja kuwaharibia makazi yao, Squirrels ni Omnivores yaani wanakula chochote kama binadamu, majani pamoja na nyama.

wanaweza kumwangusha mpaka nyoka kama akikaa vibaya, hula sana mizizi na mbegu mbegu na pia hula minyoo ya chini ya ardhi.


Hawa ni kama sungura wana speed kali ya kula na wanatabia ya kuhifadhi chakula kwa vipindi vya njaa.


Squirrels ni CREPUSCULAR hii inamaanisha ni wanyama ambao wako active wakati wa asubuhi na jioni tu, Hivyo wakati wa mchana na usiku hukaa kwenye nyumba zao na kupanga maisha.[emoji23]


Wanatabia ya kuota jua ili kuwasaidia katika kuchangamsha damu.
Wakati wa uzao hakuna mashindano, maana wanakuwa tayari wameshajuana tangu ujanani,


Ila mara nyingi tatizo hutokea pale ambapo dume hajui kama bebi yupo tayari kwa uzao au laa..(yaani dume yupo yupo tu haelewi kitu kama wale wa Kinondoni)[emoji23]


Hali hiyo humlazimu jike kujiongeza kwa kumpeti peti, na baada ya mating jike hushika mimba kwa siku 30-66 na huzaa watoto 2-8 ambao huitwa KITS.Kwa wastani wanaishi miaka 6-20.


View attachment 1167636
[emoji3][emoji3][emoji3]daah ulivyoelezea sasa
 
Nimewaona nchi za nordic ila Tanzania sijawahi kuwaona

Acha utani, hawa si kichakulo au kindi, mbona wamejaa tu? unataka kutuamiaminsha kuwa wewe umesafiri nje ya nchi?
 
Hata sasa hivi hapa nilipo nawaangalia. Huku kwetu wanaitwa njindi au kichakoro! Nimeshindwa tu ku upload picha.
 
Bongo wengi tu huwa wanasimamia miguu ya nyuma

Nafikiri mkuu umewafananisha na Meerkat maana hawa ndio wapo wengi sana kwetu
Ila hawa squirrels wanaishi kwenye nchi za baridi zaidi
IMG_1365.jpg
 
Back
Top Bottom