Unamfahamu aliye na mamlaka ya kutoa adhabu ya viboko shuleni kwa mujibu wa Sheria?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
630
957
Mwalimu mkuu ndiye mwenye mamlaka ya kutoa adhabu ya viboko au mwalimu mwingine ambaye atakasimishwa na mwalimu mkuu kwa uangalizi maalum.

Tukio la viboko kwa mwanafunzi sharti liwekewe kumbukumbu kwa kuandika jina la mwanafunzi, kosa alilofanya, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu kisha mwalimu mkuu ataweka sahihi taarifa hizo.

Kanuni ya The education (Corporal punishment) ilitungwa na Waziri wa Elimu mwaka 2002 kama sehemu ya mamlaka yake

Kanuni hizo zinasema kuwa adhabu ya viboko itatolewa iwapo utovu wa nidhamu utafanyika ndani au nje ya shule na adhabu itazingatia umri, jinsi na afya ya mwanafunzi na isizidi viboko 4.
 
Hii sheria ya kupuuzwa ililenga kuharibu kizazi cha Waafrika, turejee sheria hizi zilivyo haribu wanafunzi wa Kenya na mpaka sasa hivi wazazi wanaweka mikono kichwani watoto wameharibu mno
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom