Unakumbuka vioja vipi siku unatahiriwa?

INTROVERT MAN

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
993
1,337
kipindi hiko mimi binafsi ndio nimekuwa mkubwa (darasa la sita) nilikuwa namng'ang'ania mzee anipeleke baada ya kuona washikaji zangu wote wameshakatwa..

Basi siku tu mzee akanambia twende hospital moja hv binafsi ambayo daktari mkuu ni rafiki ake.Basi mzee akawasha baiskeli yake phoneix tukaondoka kuelekea huko mida kama ya saa tisa hv adhuhuri

tukafika mapokezi daktari akamwambia wee mzee baki hapa endelea kuangalia mpira (nakumbuka ilikuwa Argentina vs korea kusini)

tuakamuacha mzee ,daktari akiwa katangulia kunipeleka chumba cha mauaji.kiufupi nilikuwa na karoho ka kujiamini na sijui kalitokea wapi. tukaingia hcho chumba cha operation. duh kucheki hv mikasi na vifas kibao vya upasuaji vimejaa ohoo mbona ule ujasiri ukaanza kuniyoyoma.

dr. akanambia vua suruali panda hapo juu .nikapanda asa mule chumbani doctor alikuwa akisaidiana na nurse mmoja ambaye baada ya kupanda kitandani akaanza kumchezea abdala nae akakakamaa. mara paap nikasikia sindano ya kwanza,pili,tatu na nyingne hata sikuzisikia.. nilitamani kulia lakini nikasema mie ni kidume kulia hapana

nilisali sala zote huku akili zikiwa mbali nikisikia msuguano wa mikasi..aloo

baada ya kama saa hv nikaambiwa amka ..kucheki hv dushe limepigwa sijui plaster na bandej afu limevimba na kibaya walivoanza sikuwaambia kuwa nmebanwa na mkojo..nilivoamka doctor akanionesha kile kinyama baada ya operation.. sikuwa na hamu hata ya kukiona kilikuwa cheusi tii afu kina sura mbaya

nikavaa suruali fresh mikono mfukoni nikafika mapokezi mzee akalipa.ile tunatoka nje ya geti duh si ganzi ikakata alooooo yale maumivu sitaki tena kuyasikia afu mzee aliniudhi kinyama eti anataka anipandishe kwenye baiskeli na maumivu yale

nikakataa basi akasema chukua hela ukapande daladala me natangulia nyumbani.. mzee huyo akatokomea na baiskeli..ngoma ikawa kwangu daladala muda wa jioni zinakuwa hamna nikasubiri wee na yale maumivu basi bahati nzur nikapata ..nilichokuws nakiwaza muda huo ni kufika home tu then nilale ..ula mwendo wa daladal ukawa kama wa kinyonga..mara paap nikashushwa kituo cha nyumbani na ikabidi nivuke road. aisee misuli ya miguu nayo ni kama ilipoteza nguvu nikajikuta natembea polepole nikafika home mama hata hajauliza akanipa bonge la bukta (kitenge nilikataa) ila sio mbya mida ya saa 4, usiku maumivu yalikata

Aisee kukojoa ndio ikawa msala mkojo unatoka kidogo kwa kugoma afu unakuwa na njis kama zote.waweza maliza dk 10kibofu hakijawa empty ...

siku yakubadilisha bandeji ya kwanza ndio nililia aiseee kidonda chekundu balaa mpka nikawa najiuliza kitapona kweli..ile anaweka dawa mpya na kufunga bandeji mpya kwa yale maumivu nikawa naona akheri ya siku ile ndio nakatwa govi..

baada ya week hv nikawa fresh.. wazee wanaenda kazini me nmebaki ndani..wakiondoka tu me huyo mtaani nacheza mpira weee nikiona ndio mida yao ya kurudi chap narudi home kama kagonjwa vile.........

aisee kila nikikutana na yule doctor hiwa anacheka sana na kunitania "dogo ushaanza kukitumia?"

najua humu jf wapo waliokatwa govinda porini...leta ushuhuda wako hapa maana na sie wanaume tuna changamoto kama hii
 
Sijui hata ilikuwaje,mi nilikuwa najuwa ndio nimezaliwa hivyo hivyo,baadaye ndio nikaja kujua kumbe waliniwahi kabla sijawa na akili timamu...
 
Ilikuwa nikifunikwa nisione mi nafunua nataka nione!! Mpaka walichoka ila ganzi ilikuja kuniishia wkt wanashona Tena kwa huku chini nilitoa ukelele!! Wakaongeza.. nishamaliza daktari ananiita tena kunidunga sindano ya tako nilikasirika hlf kabla yangu kulikuwa na lijamaa kubwa tu ati limetoka kutairiwa duh! Nililicheki kinoma! Watu wengine huwa wanakuwa wapi mpk kufikia umri wa ujana kabisa ndi anatairiwa si shughuli pevu ile! Madaktari wanatabu😎😂
 
Mi wakat wa shughr mkojo ukabana.. na muambia dkt subir nikakojoe hasikii et mpk amalize kushona...

Aaah nikaurusha asingekua mwepes ange'unywa..
Mkojo ulipaa juu then ukarud kwenye dudu baada ya hapo ile chumvi chumvi ya mkojo ikamalza ganzi yote af hajamalza kushona nilijuta,
 
Nakumbuka nilikuwa na kama miaka 7 na kilichofanyika tulikuwa watoto 6 wa mtaa mmoja. Enzi hizo vijijini kulikuwa na umoja sana. Yaani majirani wenye watoto wanahitaji tohara wanachagua wakakae kwa mtu mmoja mwenye chumba kikubwa na magodoro yanatandikwa chini ndio tunalala hapo mpaka siku mnapona.
Sisi ilikuwa hakuna kulia kwakuwa tuliambiwa ukilia tu wenzako wanakucheka na unatahiriwa huku wenzako wanaona.
 
Naamka asubuhi naona tunavuliwa nguo tunavishwa lubega tulikua wawili. Mara doctor akaja na beskeli yake hapo tumefungiwa chumbani..Lia sana
Pale kwenye kuchoma sindano kunauma usiombe.
Yote kwa yote kuna madude yanakua kama ulimi shingoni kwetu huwa yanakatwa bila ganzi. Mweeeh usiombe wajameni Inauma sana
 
Nilikua kidato cha sita shule moja ipo Makete. Mwaka huo Makete na Njombe kukawa na kampeni inaitwa Operesheni Dondosha Mkono Sweta basi vijana wengi wa ile shule kumbe ni magovinda tukajikusanya tukavamia hospitali kuunga mkono juhudi.

Ilipofika zamu yangu yule Daktari akaniambia "Mdogo wangu una kadudu kadogo mno yaani kanaonekana kakubwa kwa ajili ya hiyo ngozi, tukiitoa na hiyo wazia betri za rimoti ya deki ya Singsung, nashauri usitahiriwe"

Nikajishauri mwisho nikaachana na huo mpango. Hadi leo mimi ni #ProudlyGovinda
 
Aisee mi nilienda wakati mkubwa mkubwa nipo secondary tena shule ya Boarding.. Kipindi icho kuna katabia nilikuwa nimetoka nako Boarding ka Pull table...

Ishu ni kwamba baada ya kukatwa mwezi mmoja mbele nikaona hii imekuwa too much lazima nirudi kwenye mchezo wangu wa pull table .. Kilicho tokea najua mwenyewe ili bidi nirudishwe upya hospital..
 
[QUOTE="Castr,
mwenye kibamia wa kwanza kuwa proudly hadharani, hongera kaka angu :D
 
utajidharirisha bure
kivipi mkuu? Yaani mimi niliyesimama naangalia mbele huku ngariba anafanya yake bila hata kutikisika nijidhalilishe kwa huyu aliyepigwa nusu kaputi ndo akakatwa?
 
Back
Top Bottom