Unakumbuka tukio gani ulilonusurika na ukaamini ni mkono wa Mungu umekunusuru?

Hapana mkuu,nilimsamehe kwakuwa inawezekana hakuwa yeye,kwani mpaka sasa siamini kama ni kwa akili zake angeweza kufanya tukio la hatari kama lile na hata yeye alijilaumu sana kwanini alichukua ule uamuzi...
alikuwa tungi? karibu hapa Chaugingi tupate beer baridi
 
1. Niko primary darasa la sita tukatoloka kwenda kuogelea mto kanoni Bukoba mjini tulikuwa mtu nne Ila mm sijawai kabisa kuogelea toka nizaliwe. Mwenzangu wakafika wanachojoa nguo wakaanza kuyapiga maji, kuona wanavyo ogelea na mm nikaona ni simple mbona ikabidi nivue nguo nikajitosa nikapiga maji mpaka mbele kabisa Ila ghafla nikawa nimechoka nikasema Sasa ngoja nisimame ile kujalibu kusimama kumbe kina nikirefu miguu haifiki chini, nikaanza kunywa maji, nikazama mara ya Kwanza nikainuka, nikazama mara ya pili nikainuka ile naingia mara ya tatu jamaa ya ngu mmoja akawa amefika akanishika mkono kunipeleka ngambo ile ndo ilikuwa pona yangu. Kwenda tulipo vulia nguo tunakuta akuna kitu yaani ni patupu. Kimbembe ilikuwa jinsi ya kutoka pale kufika nyumbani tukiwa watupu maana shule yenyewe ipo mjini kabisa.

2. Tukiwa primary tukawa tunacheza ile michezo ya kuingia kwenye tyre ya gari alafu unasukumwa inaanza kuzunguka kwenye mtelemko nawewe ukiwemo kwenye hyo tyre. Basi bwana ikawa zamu yangu nikaingia jamaa zangu wakasukuma kitu ikakolea speed kumbe mbele inakuja hiace iko speed nashukuru dreva alisimaa ile tyre ikaenda kujigonga kwenye hiace ikadondoka pembeni yule jamaa alitandika makofi sijawai kuona.

3. Nikiwa nimemaliza kidato Cha sita natoka kijijini usiku nikiwa na braza yangu amenibebe kwenye pikipiki tunaingia kwenye barabara ya lami. Kusogea mbele ikatokea fuso moja jamaa akatupiga full braza akawa aoni vzr mbele ikabidi haipishe ile gari kushoto kumbe mbele kidogo walikuwa wanalekebisha barabara kwahyo walikuwa wamepanga mawe makubwa magari yasipite pale. Kutokana na ule mwanga wa gari aliokuwa ametupia braza akuona Yale mawe kwahyo akayapalamia kwa nguvu mm nilitoka kiti Cha nyuma nikaenda kulala kalibu na katikati ya barabara wakati uwo kumbe Kuna semi teller inakuja yani ilipita centimiter Kama tatu kutoka kichwa changu kilipo dondokea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom