Unakumbuka tukio gani ulilonusurika na ukaamini ni mkono wa Mungu umekunusuru?

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,146
33,295
Nikiwa nimejilaza kitandani kwa kupumzika tu,miguu iko chini, yaani nilikaa kitandani halafu nikaamua kujilaza. Nilikaa kwa upande ambao mtu akiwa amelala kawaida huweka au kuelekeza miguu yake, baadae nikajilaza.

Baada ya dakika kadhaa nilimuona nyoka akinitazama, akiwa amesimama upande wa kushoto wa kitanda, tukawa tunatazamana yeye akiwa chini sakafuni. Tulitazamana hatimae nyoka akaamua kushusha kichwa chake na kugeuka na kuondoka zake.

Niliishiwa nguvu, sikuamini kabisa nilichokiona.yaani kitendo cha kuinuka nusu mzima nyoka ndio kilinishangaza, hapo ndipo nilipojua kuwa kumbe nyoka anaweza kupanda kitandani kirahisi tu.

Naamini ni Mungu tu ndio alikuwa mwamuzi wangu siku hiyo.

Unaamini katika Mungu? Wewe ulinusurika vipi, uliokoka vipi? Ulipona vipi? Tuwekee tukio lako tafadhali.
 
Sasa mpka nyoka aingie chumbani kwani unakaa porini? Halafu haujamalizia baada ya hapo nyoka alienda wapi? Hii ni chai

Sent using Jamii Forums mobile app
niliacha mlango wazi,ni yalikua makazi mapya watu ndo wanajengajenga,ukweli ilikua ni bado watu hawajajenga sana wala hawajahamia sana.
Niandike chai kwa manufaa yapi labda .
 
Sikuamini kabisa kama ingetokea katika maisha yangu ,yani bila kutazamia ilitokea tu! Kwa kweli kuna mambo yanaweza kutokea bila kuzaniwa wala kufikiri ila nazani ni kwa ajiri ya maombi ya wengi hali yoyote inaweza kujiri.

Kwa kweli siamini hadi leo kama naweza kuwa hapa,yani ilikuwa mwaka 2015 miezi ya mwishoni ambapo mimi nilikuwa katika shughuri zangu mida ya saa 7 mchana maeneo fulani,alipita jamaa mmoja ambaye sikuzani kama angeweza ila ndo ikaja kuwa ,ndo huyu tunaye sasa ni JOHN POMBE MAGUFURI akiomba kura kwa wana nchi wa Tanzania na baada ya hapo akashika hatamu ya kuongoza nchi, dah siamini kabisa,jamaa anapiga kazi sijawahi ona,yani hata huyo nyoka wako angemuona huyo jamaa angetoka speed ya jet.viva POMBE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkono wa Mungu upon nami mambo mengine nayajuwa mengine siyafahamu Ila najuwa ameninusuru kwayo.nakumbuka haya

Nilikoswa koswa na gari wakati navuka barabara kuu ya lami nilichosikia badae ni honi nyingi na watu wakiwa wamehamaki

Nilinusurika kuzama kwenye kisima cha maji kikiwa na tope zito chenye urefu wa kama futi 7 nikiwa mdogo

Nimedondoka Mara nyingi na Mara zote nainuka ni kwa sababu ya neema zake tu nasonga juu
 
Napandisha mlima mdogo baaada ya kukunja njia nne Goba kuelekea madale, majira ya saa kumi na mmoja na nusu asubhi, uoni wangu ni kama mita tano tu mbele tangu mwanzo wa safari huko kati kati ya jiji. Usingizi na mzio vinanifanya nashindwa kufumbua macho kwa ufasaha...lahaulaaa☠👻☠👾🤖 Ppuuh.!!.... Nilikuja kusikia sauti za watu tu wanaulizana kuna mtu humu lakini? au wenyewe walishakimbizwa hopsitali kwa matibabu!!. nilichomoka katika mabati ya mjapan yaliyokuwa gari huku yanavuja damu, mafuta na kila fluid ambayo ilikuwamo mule...Ndiposa nikaaamini kuwa Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi nazo zimejaa taabu....😤😤
Kuwa mzima hadi leo namshukuru MUNGU WA MBINGUNI sana kwani sina kovu wala sijawahi kuvunjika mfupa kati ya mifupa aliyoniumbia ila NILIVUJA DAMU ....ni miujiza eeeh 🥴,,,Mkono wa MUNGU ulininusuru!!
 
Mwaka 2005 kama Vijana wengi wa Kibongo nilidhamilia kuzamia South Africa... Niliondoka Dar Mimi na Rafiki yangu tukapitia Mtwara tukaibukia Mji wa Pamba Vijijini Upande wa Mozambique....

Tukiwa njiani tulikutana na Mbongo 1 so safari yetu ikawa ya watu 3...

Usiku ulikua Umeingia tukaenda kwenye Nyumba moja Maeneo ya Kijiji kimoja huko Pemba kuomba Hifadhi japo kwa usiku huo then Kesho yake asubuhi tuendelee na safari....

Mwenye Nyumba akaenda kushauriana na mkewe baadaye akaja na Mifuko ya Salfeti, akatwambia wametupa Hifadhi ila si ndani ya Nyumba, akatuonesha sehemu ya kulala chini ya mti wa Mwembe ambao Upo jirani na Nyumba yao.

Hatakua na jinsi kila mtu akachukua kilago chake tukaenda kutandika chini Mwembe na kujilaza.....

Wale wenzangu wawili hawakua comfortable kulala pale chini, wakashauriana wakaamua wapande juu ya mti na kujiegesha huko.... Mimi nikaamua kuendelea kulala pale chini.....

Kifupi asubuhi kunakucha Mimi nimejikuta naamka pembeni kabisa ya Makazi ya ile Nyumba, ile kuangalia pembeni naona Mistari ya Mburuto wa kile Kiroba nilichotumia kulalia, nikafata ule Mburuto mpaka pale chini ya mti, naona alama zingine za Unyayo zimekatiza pale pale nilipokua nimelala, alama Zile za Unyayo zinaonekana juu ya Mburuto wa kile Kiroba, Nikiwa Najiuliza nini imetokea.... Kutizama juu naona wenzangu wanatetemeka hatari na mmoja wetu Suruali yake Ilikua imelowa..... Nawauliza kuna nini....?

Wananambia kama Nusu saa iliyopita Simba kapita pale chini ya mti nilipokua nimelala, wao wameshtuka wanagundua Simba yupo chini ya mti... Wakashindwa kufanya chochote juu yangu baadaye kulivyoanza kupambazuka kidogo wakawa hawanioni pale chini zaidi ya kuona Mburuto kwa mbali..

Mpaka Leo sinaga jibu ni nini kilitokea, nani aliburuta Kiroba nilicholalia....!
 
lee van cliff, Huyo hakuwa Koboko.... (Black Mamba). Manake huyu hana simile .. haujamchokoza lakini anakutoa nduki.

Mimi siamini kwenye "God intervention" kila jambo linafuata misingi na kanuni za asili... hapo ilikuwa nyoka akugonge au akuache, au wewe umuue. Hakuna cha ajabu hapo (hakuna kanuni iliyovunjwa).

Nyoka kuingia ndani kwako inawezekana, nyoka kukudhuru au kutokukudhuru inawezekana pia.

Jiulize hivi angekugonga je, ungesema nini kuhusu Mungu (virse versa ??)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh.. .

Nilikaa I.c.u..mda sana tu..

Lakini ajabu..nilikuwa pembeni ya mwili wangu ulipolala...natoka na kuingia wodini...naona ndugu na madoctor...tatizo nilikuwa siwezi kushika mtu au kitu wala kuongea na nikitembea nilikuwa sikanyagi ardhi!

Nikajiuliza sana sana...kwa nini iwe hivi? jibu sikupata!

Kwa ufupi...nilirudi .. katika hali ya kushangaza mno.
Lakini ndugu zangu ... huu ulimwengu
una mapana!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asubuhi saa 12 naamka na wenge nikimbie shule.. naenda kushika kitasa ili nifungue nakuta black mamba kajizinga pale kwenye kitasa ananikodolea macho..
Yaani umbali wa nyoka na mkono wangu kama inch 5 tu.
Nilishtuka sana..hua siui mdudu yoyote baada ya mbu so niliamsha wengine waje wamtoe nikawaambia wamfukuze nje. Bahati mbaya wale binaadamu walimuua yule nyoka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom