Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,675
- 40,555
Imepita miaka mingi na kumbukumbu zetu zimeanza kufifia; wengine hawana kumbukumbu kabisa lakini kwa wengine siku ile iko kama jana... kwa mara ya kwanza Tanzania bara ilimpoteza kiongozi wake wa kitaifa, na likawa pigo la kwanza kwa wananchi wa bara kumpoteza kiongozi wa juu wa kitaifa akiwa bado madarakani na bado inabakia ndio tukio pekee ingawa kama Taifa, lilitanguliwa na tukio la kuuawa kwa Karume.
Siku ile ya Alhamisi ya tarehe 12, 1984 ni siku ya kukumbuka kwa wengine machozi na kwa wengine siku ambapo yawezekana kabisa mafisadi walipojua kuwa huko mbeleni hakutakuwa tena na kiongozi hodari na jasiri kama yule. Mwaka mmoja baadaye Rais Nyerere alistaafu na mabadiliko makubwa yalitokea. Taifa likajikuta halina mtu kwenye uongozi wa juu mwenye uwezo wa kusimamia ukweli na kuwaambia viongozi wenzie ukweli...
Pamoja na mapungufu yake mengi na labda jazba kubwa ya kuwatafuta "wahujumu uchumi na walanguzi" alijijengea maadui au aligusa makasri yasiyoguswa; lakini hadi leo hii tukimlinganisha na waliokuja baada yake na viongozi wengine ni wazi kuwa bado anasimama kwenye kundi la peke yake.
Tunapoendelea na mapambano haya dhidi ya mafisadi najikuta leo nikikumbuka na kummiss Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine na nikiamini yaliyosemwa wakati ule kuwa "pengo aliloliacha haliwezi kuzibika". Yanayoendelea sasa nchini yanathibitisha kabisa kuwa watu kama Sokoine wanakuja mara moja kila nusu karne!
Mhe. Edward Moringe Sokoine... watu bado wanakukumbuka hasa wale wanyonge wa Taifa hili..