Unakumbuka Siku ile ya machozi...

Ufunuo wa Yohana

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
320
225
Na ndo maana hata viongozi wa UFISADI hakuna anayedhubutu kuwagusa, maana yeyote atakayeelekea kufanya mambo ya kutafuta haki na sheria kifo kinamyemelea kutoka kwa Mafisadi, na viongozi wengine wa serikali??

Sasa kifanyike nini jamani?
Mimi naona hapa solution pekee, ni kuanzisha vita jamani? Vita yenyewe, sio ya ukabila au udini kama zilivyo nchi zingine, ila ni vita kati ya wanyonge na Mafisadi, vita hii inalenga kuhakikisha kuwa mali zote za wananchi zinarudi mikononi mwa wananchi!! au mnasemaje wakuu, hivi hivi tutakaa kuongea tu mpaka basi, na hakuna kitakachofanyika kwa sababu hata kikwete anaogopa anaweza kuuliwa muda wowote, sasa ni sisi kuhakikisha mafisadi wote tunawamaliza na kuanza kuijenga Tanzania mpya jamani
Mara zote vita huwa ni suluhu ya mwisho kabisa na hii haipangwi ila huja automatically. Ukisema uanzishe vita utajikuta uko peke yako unavunja ukuta wa nyumba ya Lowasa wenzio wako majumbani. Tatizo tulilo nalo TZ ni ukosefu wa elimu hasa ya kujua haki zetu za msingi kutoka kwa watawala tuliowapa dhamana ya kutuongoza. Bado tunawaza kuwa kupiga kura ni kutimiza wajibu na hatuoni thamani ya kura tunayopiga. Siku tutajua thamani ya kura ndipo hata vita itakuwa ni rahisi kuwepo kama hiyo kura yangu ya thamani haijatendewa haki.

Siku mwananchi amejua thamani ya kura yake ndipo mambo yatakuwa ktk mstari. Ninayo mifano mingi kutoka kwa rafiki na ndugu wa karibu wakati wa kupiga kura wanasema hawaendi au hata kujiandikisha wanaona ni usumbufu kwao. huu ni ushahidi tosha kuwa mtu huyu hajui thamani ya kura yake. Hata wewe mwana JF inawezekana unao watu wa hivyo au hata wewe mwenyewe wanadharau u-thamani wa kura zao. Hili ni hatari na linahitaji msukumo wa kipekee kwani hata wasomi wengine ni Ma-prof siku ya kura hawaendi wako busy na reseach zao bila kujua hizo reseach haziwezi kutekelezwa bila kuwa na kiongozi muadilifu.

MTANZANIA THAMINI KURA YAKO KUANZIA LEO, USIKOSE KUPIGA KURA, UJUE UMUHUMU WA KUWEPO HAPA DUNIANI, JITHAMINI KWANZA WEWE KUWA UNAWEZA KULETA MABADILIKO. JIANDIKISHE KUPIGA KURA, NAFASI YA KUJIANDIKISHA UMEPEWA, FANYA HIVYO TAFADHARI.

MUNGU AWABARIKI
 

Ufunuo wa Yohana

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
320
225
Mimi nijuavyo ni kuwa Dr. Shaba ndite alifanya postmotem ya Moringe na ripoti ilikuwa siri sana kwa kweli. Kwa mara ya kwanza nilimuona Kambarage akitoa machozi hadharani pale Karimjee (bunge la zamani).

Niliambiwa kuwa Lowassa alikuwa na mpango kuwa baada ya Kikwete urais ungehamia Monduli kwa miaka 20 maana yeye angechukua kwa miaka 10 na kisha kumpisha mtoto wa Marehemu Sokoine ambaye yuko Marekanai kwa miaka mingine 10. Wakati yeye (Lowassa) akiwa rais mtoto wa Moringe angekuja kugombea ubunge wa Monduli (ambao angeupata kirahisi kutokana na jina la baba yake) na kisha baadaye kuwa waziri kwa miaka 10 ya uongozi wa Lowassa. Hiyo ingempa uzoefu wa kuwa rais baada ya Lowassa kumaliza kipindi chake.

Sasa mambo kidogo yamebadilika sijui itakuwaje.

Mpango huo haujafa ila umeongeza task kwa wanamipango kwamba ni lazima wamsafishe Lowasa kwanza ili aweze kunadika 2015 kwa wajumbe wa CCM. Hivyo mpango huo haujafa ila umeongeza majukumu tu kwa wanamipango wa mtandao
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
34,410
2,000
Bubu nadhani umechanganya masuala kidogo hapa. Dr Fupi (Ferdinand, MD) hadi hivi karibuni alikuwepo Morogoro kwa kadiri ya kumbukumbu yangu, na kuna wakati miaka michache iliyopita nilikutana nae huko katika vikazi vyangu vya "ungwini". Dr Fupi "aliyepotezwa" ni yule aliyekuwa mkemia mkuu wa serikali miaka ya 1990, enzi ya lile sakata la uingizaji wa vyakula vibovu, aliweka msimamo mkali sana juu ya maelfu ya tani za vyakula hivyo vilivyoagizwa kutoka nje kifisadi kuwa havifai kwa matumizi ya binadamu, na alikuwa shahidi muhimu mahakamani. Alifariki katika mazingira ya kutatanisha kabla hajatoa ushahidi huo.
Nadhani Kithuku uko sahihi.
Shehena ya vyakula hivyo si ilikuwa imeingizwa na Mohamed Enterprises! Na baada ya kifo cha Mkemia huyo na kesi nayo ikaingia kaburini.Inasikitisha sana.
 

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,729
2,000
Bubu nadhani umechanganya masuala kidogo hapa. Dr Fupi (Ferdinand, MD) hadi hivi karibuni alikuwepo Morogoro kwa kadiri ya kumbukumbu yangu, na kuna wakati miaka michache iliyopita nilikutana nae huko katika vikazi vyangu vya "ungwini". Dr Fupi "aliyepotezwa" ni yule aliyekuwa mkemia mkuu wa serikali miaka ya 1990, enzi ya lile sakata la uingizaji wa vyakula vibovu, aliweka msimamo mkali sana juu ya maelfu ya tani za vyakula hivyo vilivyoagizwa kutoka nje kifisadi kuwa havifai kwa matumizi ya binadamu, na alikuwa shahidi muhimu mahakamani. Alifariki katika mazingira ya kutatanisha kabla hajatoa ushahidi huo.
Yawezekana uko sahihi nami nikawa sahihi na Dr aliyemfanyia postmoterm EMS ndiye haswa niliyelenga kwamba alikwenda tusikopenda kwenda huko japo lazima twende.
 

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
7,006
1,225
Mara zote vita huwa ni suluhu ya mwisho kabisa na hii haipangwi ila huja automatically. Ukisema uanzishe vita utajikuta uko peke yako unavunja ukuta wa nyumba ya Lowasa wenzio wako majumbani. Tatizo tulilo nalo TZ ni ukosefu wa elimu hasa ya kujua haki zetu za msingi kutoka kwa watawala tuliowapa dhamana ya kutuongoza. Bado tunawaza kuwa kupiga kura ni kutimiza wajibu na hatuoni thamani ya kura tunayopiga.
Nadhani vita anayomaanisha babaH si ya mtutu wa bunduki. Ni sawa na vita unayoizungumzia katika sehemu ya mchango wako kuhusiana na watanzania kutokuwa na elimu kuhusu haki zao.
Zifanyike jitihada za kuhakikisha kwua watanzania wanajulishwa haki zao ili waweze kuendesha mapambano haya na kufanya maopinduzi ambayo yatawapatia fursa ya kuona aina nyingine ya utawala/uongozi itafanyaje.
Hakuna haja ya kuogopa mabadiliko kuwa yanaweza kutuletea hali mbaya kwa sababu hii tuliyonayo hivi sasa ni hali mbaya tayari. lakini kuna faina nyingine, iwapo tutapata moyo na nguvu ya kufanya mabadiliko, watakaokuja tukiona nao hawatufai, bado tutakuwa na moyo ule wa kufanya mabadiliko hivyio tunaweza kufanya mabadiliko mengine bila kutumia nguvu nyingi kwa sababu tutakuwa na uzoefu wa kufanya hivyo.
 

Single D

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
458
195
Yawezekana uko sahihi nami nikawa sahihi na Dr aliyemfanyia postmoterm EMS ndiye haswa niliyelenga kwamba alikwenda tusikopenda kwenda huko japo lazima twende.
Bubu nahisi Dr aliyefanya post mortem ya EMS ni Prof.Shaba.
RIP Sokoine
 

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,225
Kifo cha Sokoine ilikuwa ni mara ya Pili kwa Mwalimu kushindwa baada ya Azimio la Arusha kabla ya kushindwa tena kwenye Uchaguzi wa mwaka 1985 pale chaguo lake DR.Salim Ahmed Salim kushindwa dhidi ya Alhaji Mwinyi kwa shinikizo la wahafidhina

Mwalimu inasemekana kabla ya kifo cha Sokoine siku hiyo hakutulia kabisa Ikulu kwa madai kwa alijulishwa mapema kwa kuna njama za kumuua Sokoine na inasemwa kuwa hata suala la sokoine kutumia njia ya barabara ni kutokana na ushauri wake

lakini kuna hoja kwamba walinzi wake walifyatua bunduki kwa bahati mbaya na risasi zikampata bwana mkubwa. Lakini hapa kuna hoja ya msingi.ni hadi lini mambo yanayowahusu viongozi wetu yanatakiwa yawe siri?
 

Jamco_Za

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,333
1,225
Swala la msingi ni kutoa elimu kwa wananchi ili tutumie kura zetu vizuri, mfano elimu kidogo waliyopata wananchi wanaweza kuwazomea viongozi wabovu kwa hiyo wakipata elimu ya kutosha kila kitu kinawezekana. Shime watanzania tujitahidi kuwaelimisha wanachi hasa vyombo vya habari vina nafasi kubwa sana. Hizi NGO kazi zake nini maana wenzetu wa zimbabwe wamesaidiwa sana na NGO zao na wananchi wana mwamko mkubwa sana wa kutaka kumwondoa Mugabe. Kwa Tanzania NGO zinaitaji kuangalia role zake upya ili ziweze kusaidia wananchi kufaamu haki na wajibu wao.
 

FDR Jr

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
249
0
UMMA UMTENDEE HAKI EDWARD MORINGE SOKINE, TUNAYO HAKI YA KUJUA NI NANI WALIOKUWA NYUMA YA KIFO CHAKE, JE NI KWELI KAWAWA? MSUYA? NA NANI WALE? TUNAPENDA KUUFAHAMU UKWELI MAANA KAMA NI KWELI ALIUAWA BASI TUWAANGALIE VIONGOZI WETU WA ZAMA HIZO WALIOKUWA NA SURA ZA KIBEPARI NA KUJIFANYA WAJAMAA, NILIKUWA KIJANA WA MIAKA 11 BY THEN BUT NAIKUMBUKA HALI YA MVUA NZITO KULE KIJIJINI KAMA ILIVYOKUWA 2WEEKS HIZI HAPA DAR,YALIKUWA NI MAOMBOLEZO TOKA ROHONI TOKA KWA WATOTO MPAKA WAZEE,NI MAUMIVU YA KWELI,ndio maana ninahamu ya kuangalia TBC1 kama wana lolote kwa kutwa ya kesho hao wengine sitarajii maana wengine ni matunda ya kifo cha Sokoine ila wanajifanya wanataka haki sasa na kusahau walichoifanyia Tanzania zama zao.
 

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,194
0
Bubu nadhani umechanganya masuala kidogo hapa. Dr Fupi (Ferdinand, MD) hadi hivi karibuni alikuwepo Morogoro kwa kadiri ya kumbukumbu yangu, na kuna wakati miaka michache iliyopita nilikutana nae huko katika vikazi vyangu vya "ungwini". Dr Fupi "aliyepotezwa" ni yule aliyekuwa mkemia mkuu wa serikali miaka ya 1990, enzi ya lile sakata la uingizaji wa vyakula vibovu, aliweka msimamo mkali sana juu ya maelfu ya tani za vyakula hivyo vilivyoagizwa kutoka nje kifisadi kuwa havifai kwa matumizi ya binadamu, na alikuwa shahidi muhimu mahakamani. Alifariki katika mazingira ya kutatanisha kabla hajatoa ushahidi huo.
Mhhh JF ina vichwa,

Asanteni wazee Kithuku na wengine kwa facts nzito!
 

Kalamu

JF-Expert Member
Nov 26, 2006
874
0
Naam, Tutakukumbuka na kuenzi mchango wako katika kuleta mageuzi katika taifa letu la Tanzania. Tutakukumbuka daima mwanamapinduzi na mzalendo wa kweli Moringe Sokoine.
 

BabaH

JF-Expert Member
Jan 25, 2008
704
225
Ni wambie tu kwa wepesi tu, mnayoyaona Zimbabwe ndo hayo yatakayotokea Tanzania siku CCM ikishindwa
Hivi unadhani hata wananchi wakakubali kupigia wapinzani kura, unadhani kwa mtandao uliopo sasa hivi kila mahali ni pa CCM , unategemea matokeo yatangazwe kuwa Upinzani umeshinda???

Hili haliko tu Zimbabwe, ila ni karibia nchi zote, angalia kenya kilitokea nini, tume ya uchaguzi ilitangaza Kibaki kashinda wakati sio kweli, angalia Zimbabwe, sasa mnategemea nini??
Hata tukapiga kura vipi, bado hawa jamaa watangangania kwa njia yoyote hile jamani

Angalie yanayotokea Zimbabwe, yaliyotokea Kenya, mnategemea nini Tanzania upinzani ukishinda???
 

FDR Jr

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
249
0
Wananchi wetu bado wana elimu ndogo katika suala zima la upigaji kura. Kinachoweza kuvunja mtandao huu ni kuua CCM. Ikifa inakufa na kila kitu.
PUNGUZA DHARAU KWA WATANZANIA , TUJIANGALIE SISI TUNAOUZA HOJA HIZI ZA KUIUA CCM KAMA TUNAFANANA NA KAULI ZETU KIMATENDO,UNAFIKIIIIIII NDG NDIO ULIOTPELEKA HAPA, MWALIMU ALIZINGIRWA NA WANAFIKI NA WALE WALIOTHUBUTU KUSEMA UKWELI NDIO WALIKUWA MAADUI WA NCHI HII,UGONJWA HUU BADO UPO SI KWA CCM TU NI PAMOJA NA VYAMA VINAVYOTOFAUTIANA NA CCM ,TAFADHARI WATANZANIA WALIO WENGI WAMELAZMIKA KUIMBA NYIMBO ZA HAWA WANAFIKI WALIOWATEULE WA WENYE NCHI,HAWAKUWA WAKWELI 60S NA SASA HAWATAKI KUWA WAKWELI SI KWA UMMA TU BALI HATA KWA NAFSI NA MIOYO YAO.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,634
2,000
Mwanakijiji,Kithuku,FDR Jr,Single D,Mpita Njia,...

..naikumbuka siku aliyofariki Waziri Mkuu Sokoine. Ilikuwa siku ya kawaida na mara matangazo ya RTD yakakatizwa na wimbo wa Taifa.

..Kwasababu nilikuwa mdogo sikujua nini kinaendelea kutokana na matangazo ya redio kukatizwa. Baba yangu alielewa kwamba kuna jambo kubwa limetokea. Baadaye ilisikika sauti ya huzuni ya Baba wa Taifa akisema " Ndugu wananchi ndugu yetu kijana wetu Edward Moringe Sokoine alipokuwa akisafiri toka Dodoma kuelekea Darisalama gari lake lilipata ajali. Amefariki dunia."

..Zaidi kilichosindikiza msiba ule ni zile nyimbo za dini kwa muda wa wiki. pia kulikuwa na nyimbo za kimapinduzi.Naweza kusema Watanzania waliomboleza kifo cha Waziri Mkuu Sokoine kwa namna ya kipekee, kwa heshima zote zinazostahili.

..Pia niliweza kufuatilia mazishi yaliyofanyika Monduli Juu. Mazishi hayo siyo tu yalihusisha taratibu zote za dini, lakini pia yalijumuisha mila za kabila la Wamaasai.

..Nikifuatilia matangazo ya RTD niliweza kujua kwamba mwili wa Waziri Mkuu ulipakwa mafuta yaliyotoka kwenye kifua cha dume la ngombe. Mafuta hayo alipakwa na wanawe wa kiume ktk paji la uso na miguu.Pia kulikuwa na majani maalum ambayo yalitumika katika shughuli hiyo ya kuuandaa mwili wa marehemu kimila.

..Kulikuwa na kamati ya Jeshi iliyoshughulika na kuandaa kaburi la marehemu. Kamati hiyo iliongozwa na Maj.Gen.John Walden.

..Risala ya serikali kutokana na kifo cha Sokoine ilisomwa na Mzee Rashidi Mfaume Kawawa "simba wa vita." Nakumbuka Mzee Kawawa alizungumza kwa uchungu mkubwa

..Taarifa ya familia ilisomwa na Mzee Kimesera, ambaye ndiye aliyechukua jukumu la kuwa mlezi wa familia ya marehemu. Kwa maneno yake Mzee Kimesera alisema, kama Sokoine angepata nafasi ya kusema lolote kabla ya kifo chake basi angeomba msamaha kwa yale wale wote aliowakosea!!
 

Single D

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
458
195
Mzee wa Kijijini.

Namkumbuka vilivyo huyu jemedari Moringe Sokoine wakati wa vita vya uhujumu uchumi alikuwa imara kweli kutetea wanyonge.Huyu hastahili kusahauliwa katu kwa kazi yake njema maana amekuwa piawaziri mkuu ktk nchi hii tena kwa vipindi viwili tena wakati chama kikiwa hiki sisiem.Yaani mwaka 1977-80 na Mwaka 1983-84.Huyu jemedari hakuangalia uso wa mtu,kwa kweli tulipoteza mwarubaini wa Taifa hili.

Wakati wa kifo chake Moringe sokoine nakumbuka yule Kijana wake wa kwanza aitwaye LAZARO alikuwa anasoma Cuba.Toka hapo sijasikia kama naye kaingizwa NEC au hata jumuia ya vijana ya sisiem ili kukumbuka mchango wa huyu jemedari.Nyerere akifufuka na kukuta sisiem hii atakufa tena maana imekuwa ya mke na mme na watoto wote NEC.
Wako wapi hawa watoto?huyu LAZARO NA MWINGINE ALIIITWA JOSEPH MORINGE SOKOINE?

Wake zake pale Monduli juu sijui kama wako safi kimaisha maana kipindi kile hakikuwa na mwanya wa kupora kama tunavyoona wake wa marais na mawaziri wakuu wanavyotengeneza mafuko ya fedha ya kuleta maendeleo na pia fursa sawa kwa wanawake wote(ha ha ha),ngoja nicheke kidogo.

Tudumishe mema yote ya MORINGE SOKOINE
 

Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
7,689
2,000
Joka kuu,
Umenikumbusha mengi kuhusu huyu shujaa. Nilipata fursa ya kuuaga mwili wake pale Dar. Kama kumbukumbu yangu bado ni safi nafikiri aliyesoma kwa niaba ya familia alikuwa mzee Solomon Ole Saibul. Tumeambiwa mengi, wengine wanasema alipigwa risasi, ukweli ni kuwa kifo chake kilitokana na uzembe au unprofessionalism ya walinzi wake.
 

KakindoMaster

JF-Expert Member
Dec 5, 2006
1,357
1,225
PUNGUZA DHARAU KWA WATANZANIA , TUJIANGALIE SISI TUNAOUZA HOJA HIZI ZA KUIUA CCM KAMA TUNAFANANA NA KAULI ZETU KIMATENDO,UNAFIKIIIIIII NDG NDIO ULIOTPELEKA HAPA, MWALIMU ALIZINGIRWA NA WANAFIKI NA WALE WALIOTHUBUTU KUSEMA UKWELI NDIO WALIKUWA MAADUI WA NCHI HII,UGONJWA HUU BADO UPO SI KWA CCM TU NI PAMOJA NA VYAMA VINAVYOTOFAUTIANA NA CCM ,TAFADHARI WATANZANIA WALIO WENGI WAMELAZMIKA KUIMBA NYIMBO ZA HAWA WANAFIKI WALIOWATEULE WA WENYE NCHI,HAWAKUWA WAKWELI 60S NA SASA HAWATAKI KUWA WAKWELI SI KWA UMMA TU BALI HATA KWA NAFSI NA MIOYO YAO.
Mkuu Ukweli unauma siyo kwamba tunao ona suluhu la kupatikana maendeleo Tanzania labda tuna chuki na CCM, hata baba wa taifa kuna kipindi aliona na akasema CCM siyo baba wala mama yake. Pia marehemu Kolimba aliona hilo. Pia katibu Mkuu mastaafu wa CCM Mangula ameisha ona hilo. Na pia Mzee Butiku. Wana CCM wenye nia nzuri na nchi hawana uwezo wa ku-control chama chao. Sasa suluhisho ni nini?

Ukiwa na shamba lako zuri jirani kuna Msitu uliofuga kila aina ya ya mambo mabaya, pamoja na kwamba kuna mazuri lakini mabaya yakizidi mazuri unafanyaje?

Mkuu kama kuna watu wanapenda CCM idumu na tuendelee kunyosha mikono kama zamani hawana budi kuhakikisha wanakisafisha kwa ajili ya maendeleo ya vizazi vya sasa na vijavyo. Otherwise mimi kama Mtanzania nikizunguka nikaona Tatizo lilipo lazima niseme tu.

Nina uhakika kama Mwalimu angelikuwa hai angelikuwa ameisha rudisha kadi ya CCM.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,634
2,000
gagnija,

..inawezekana Ole Saibul alisoma risala kwa niaba ya familia. lakini pia Mzee Kimesera alikuwa na role kubwa ktk shughuli nzima ya mazishi ya Sokoine.

NB:

..bado naamini kwamba kifo chake kilitokana na ajali ile ya gari. sidhani kama kulikuwa ni hujuma ya namna yoyote ile. vyombo vya usalama wakati ule vilikuwa makini sana, tena sana.

..mimi nadhani tusigeuze thread hii kuwa sehemu ya kuchafua watu na kuendekeza conspiracy theories.

..haya masuala ya kupigwa risasi, na mambo mengine ya kuhusisha kifo chake na "mkono wa mtu" ni bora yakafunguliwa thread yake.

..nimewahi kuambiwa kwamba Sokoine alikuwa karibu sana na Mzee Rashidi Kawawa "simba wa vita." tena inadaiwa mara kwa mara Sokoine alikuwa akitafuta ushauri wa Mzee Kawawa, kwasababu ndiye aliyemtangulia kama Waziri Mkuu.

..Sielewi mantiki ya kumhusisha Mzee Kawawa na chuki au hujuma yoyote ile dhidi ya Sokoine. Kama ni uwaziri mkuu mbona Mzee Kawawa aliwahi kumuachia wadhifa huo Mwalimu Nyerere bila matatizo yoyote?? Tena Uwaziri Mkuu wa Nyerere na Kawawa ulikuwa na hadhi kubwa kuliko huu wa kina Sokoine.

..Sokoine pamoja na kasoro zake kibinaadamu, za kiuongozi na kiutendaji, hakuwa mtu wa majungu-majungu hata kidogo. Naomba wakati tunamuomboleza tuache kuleta majungu na fitina.
 
Top Bottom