Unakumbuka nini ulipokuwa mdogo

Trial balance

JF-Expert Member
Jun 16, 2020
202
159
Nilipokuwa mdogo niliwahi kumwagikiwa na uji wa ubaga ambao badae uwa kama pombe mama yangu na Dada yangu walikuwa wanafanya biashara ya pombe kutokana na mkoa wetu kuwa na asiri ya baridi siku iyo uji wa ubaga ulikarishwa tangu asubuhi lakini ilipofika jioni ilibidi uipuliwe yalikuwa majira kama ya saa moja ivi mara yakasikika matangazo ya mziki kama unavyojua maeneo ya vijijini watu hukimbilia zile sauti kubwa zinaposikika mfano matangazo n.k.

Kwaiyo Mimi nilikuwa nimelala pembeni ya pipa la ubaga wa pombe Dada na mama walianza kuchota kidogo kidogo ubaga toka jikoni na kujaza kwenye mandoo. mandoo yalipojaa wakaanza kuingiza ndani ndoo moja moja Dada angu aliposikia matangazo ya mziki alinyanyua ndoo haraka haraka ili aweze kwenda ambako ule mziki ulisikika pombe ilijaa kwenye ndoo ivyo kutokana na haraka zake ndoo lilijiachia toka mikononi hadi nilipokaa nikaungua mguu mzima tangu nikiwa na miaka saba hadi Leo kovu halijatoka.
IMG_20200630_103503_113.jpg
 
Nimemiss tu namna nilivyokuwa mtaalum wa kumwaga kojo!
Hata niwekewe plastic mkojo lazima utapata njia utafikia godoro..๐Ÿ˜…
Najiuliza kipaji changu hicho kiliishajeishaje..๐Ÿ˜Ž
 
Hata niwekewe plastic mkojo lazima utapata njia utafikia godoro..
Najiuliza kipaji changu hicho kiliishajeishaje..
Mkuu sio wewe mimi nilikuwa natandikaaa mpaka chini na wameweka plastic ila mzee wapiii aisee hata niseme nichelewe kulala ila kojoo ni pale palee.

Na nilichelewa kuachaa
 
Mi hata mchana kweupe kwenye Kochi nilikuwa nauweka tu..๐Ÿ˜‚
Vitu vyengine uvumilivu ukikushinda unamwaga radhi tu.. hakuna cha hiana wala hisana mambo ni njenje Kama jeje!

Utoto Raha..๐Ÿ˜…
 
Nimemiss tu namna nilivyokuwa mtaalum wa kumwaga kojo!
Hata niwekewe plastic mkojo lazima utapata njia utafikia godoro..๐Ÿ˜…
Najiuliza kipaji changu hicho kiliishajeishaje..๐Ÿ˜Ž
Hakuna ndoto tamu kama ile unaota afu unamwaga kojo... Sema ushenzi wa ile ndoto ukimaliza kumwaga kojo lazima uamke. Hapo unaanza kutafakari kitakachojiri wakubwa watakapoamka asubuhi...

Either bakora, kejeli, matusi au msuto.

1593504630940.png
 
Nimemiss tu namna nilivyokuwa mtaalum wa kumwaga kojo!
Hata niwekewe plastic mkojo lazima utapata njia utafikia godoro..
Najiuliza kipaji changu hicho kiliishajeishaje..
Kuna siku nikapanda juu ya mti sikuvaa chupi kupanda nikaweza kushuka nikashindwa nikaanza kuning'inia kwenye mti huku niko uchi waliokwepo chini wananicheka kabisa huku mimi nalia tu huko juu badae nikapata wazo la kujiachia kujitupa juu mpaka chini ha ha ha sitasahau
 
Mi hata mchana kweupe kwenye Kochi nilikuwa nauweka tu..
Vitu vyengine uvumilivu ukikushinda unamwaga radhi tu.. hakuna cha hiana wala hisana mambo ni njenje Kama jeje!

Utoto Raha..
Mkuu yanii sijuiii nilikuwa naumwa nini mzee.

Yanii hiyoo yako ndogoo sana. Nilisha wahii lazwa kwenye chaga ila mzee wapiiii.

Kila siku saa 6 wananiamsha kwenda choonii baada ya nusu saa kurudi kitandanii tayariii nisha achiaa tena la kutosha hadi mlangoniii.
 
Kuna siku nikapanda juu ya mti sikuvaa chupi kupanda nikaweza kushuka nikashindwa nikaanza kuning'inia kwenye mti huku niko uchi waliokwepo chini wananicheka kabisa huku mimi nalia tu huko juu badae nikapata wazo la kujiachia kujitupa juu mpaka chini ha ha ha sitasahau
Kuna siku tena nikaanza kugombaniana na Dada angu sh 30 badae nikaanguka vibaya nikaangukia mkono wakanifunga pop.
 
Hakuna ndoto tamu kama ile unaota afu unamwaga kojo... Sema ushenzi wa ile ndoto ukimaliza kumwaga kojo lazima uamke. Hapo unaanza kutafakari kitakachojiri wakubwa watakapoamka asubuhi...

Either bakora, kejeli, matusi au msuto.

View attachment 1493073
Niliwahi kukurupushwa na sisteri asubuhi muhuni nishaharibu mambo!..
Alinikimbiza mtaani nipo uchi wa mnyama dudule nje tu halafu sina habari nachekelea tu๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Utoto raha hakuna cha aibu wala nini mambo yalikuwa moto.. niliitembeza dudu siku hiyo utafikiri gari la mauzo๐Ÿ˜‚
Mpk anakuja kunikamata alikutana na kisanga cha aina yake!.. halafu anakuja kunipeleka bafuni ati nifue wakati hata sijui! Shida yake niijue shida ya kufua!! Nashukuru alikuja mazeri akapiga tafu maana sikuhiyo aliona njemba kazidiwa.. raia walichoka tabia yangu..๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Mkuu yanii sijuiii nilikuwa naumwa nini mzee.

Yanii hiyoo yako ndogoo sana. Nilisha wahii lazwa kwenye chaga ila mzee wapiiii.

Kila siku saa 6 wananiamsha kwenda choonii baada ya nusu saa kurudi kitandanii tayariii nisha achiaa tena la kutosha hadi mlangoniii.
Dadeki we ndo kiboko..๐Ÿ˜‚
 
Kuna siku tena nikaanza kugombaniana na Dada angu sh 30 badae nikaanguka vibaya nikaangukia mkono wakanifunga pop.
Kingine ninachokumbuka Bibi angu alikuwa na shida ya mgongo ivyo kila ikifika jioni unakuwa na kazi ya kumkanyaga mgongoni kama unatembea mwanzo wa mgongo hadi mwisho wa mgongo
 
Niliwahi kukurupushwa na sisteri asubuhi muhuni nishaharibu mambo!..
Alinikimbiza mtaani nipo uchi wa mnyama dudule nje tu halafu sina habari nachekelea tu
Utoto raha hakuna cha aibu wala nini mambo yalikuwa moto.. niliitembeza dudu siku hiyo utafikiri gari la mauzo
Mpk anakuja kunikamata alikutana na kisanga cha aina yake!.. halafu anakuja kunipeleka bafuni ati nifue wakati hata sijui! Shida yake niijue shida ya kufua!! Nashukuru alikuja mazeri akapiga tafu maana sikuhiyo aliona njemba kazidiwa.. raia walichoka tabia yangu..
mzee aliwahii nitandikia kwenye banda la kuku wa nyama nilale naooo.

Miaka ya 90. Alivyo ona badoo hali ile ile akasema sasa unaenda kushindana na mbuzii kunyaa,na kukojoo akaniweka siku 3 kwenye banda la mbuziiii akija mbaoo hazifaiiii nguoo zotee ni maji tu kama nimetoka kuogelea.

In short walichoka wakaniachaaa.
 
Kingine ninachokumbuka Bibi angu alikuwa na shida ya mgongo ivyo kila ikifika jioni unakuwa na kazi ya kumkanyaga mgongoni kama unatembea mwanzo wa mgongo hadi mwisho wa mgongo
Jamani kwa wale wakristu wezangu kuna kitu kinaitwa kipaimara mnakuwa mnafundishwa na mwalimu kwa mda wa miezi kadhaa na badae kunakuwa na kipindi cha kukaribia kupata kipaimara lakini uwezi kupata hadi huulizwe maswali kuhusu ulichojifunza niliulizwa maswali nikaweza badae nikaambiwa nisali nia njema kila nikisali nachanganya na sala ya asubuhi ikabidi muuliza maswali aniambie nikamwambie mtu atakayenisimamia anifundishe tena nililia hapo nilishanunuliwa nguo za sikukuu nikaona sitapata kipaimara ndo basi tena.
 
Niliwahi kukurupushwa na sisteri asubuhi muhuni nishaharibu mambo!..
Alinikimbiza mtaani nipo uchi wa mnyama dudule nje tu halafu sina habari nachekelea tu๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Utoto raha hakuna cha aibu wala nini mambo yalikuwa moto.. niliitembeza dudu siku hiyo utafikiri gari la mauzo๐Ÿ˜‚
Mpk anakuja kunikamata alikutana na kisanga cha aina yake!.. halafu anakuja kunipeleka bafuni ati nifue wakati hata sijui! Shida yake niijue shida ya kufua!! Nashukuru alikuja mazeri akapiga tafu maana sikuhiyo aliona njemba kazidiwa.. raia walichoka tabia yangu..๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Sistaako kumbe kama wangu. Alijuaga sana kunizodoa.

Siku moja kalala fofofo, mjeda usiku sikulala nimemkamia. Taratibu nikaingia chumbani kwao... mwanaume nikachomoa dudu na kumwaga kojo kitandani kwake taratibu kama nakamua jipu. Sister kuamka asubuhi anakuta kitanda kimeloa... Sista akauchuna kimtindo

Sasa mimi nikawa bwege, nikataka nimuumbue kwa maza. Nikaenda kumsemea. Mama akafanya ukaguzi akakuta kweli godoro limeloa... Sista akaulizwa akabaki kaduwaa...

Sasa huyu mazeri wangu alikuwa ticha, machale yakamcheza... akaniuliza wewe ulijuaje dadaako kajikojolea kitandani? Nilikuwa sijajipanga kwa hilo swali...

Wewe ni mtanzania mwenzangu na umepitia utotoni. Sina haja ya kukuambia kilichotokea kwangu siku hiyo... Ila ujue tu kwa ufupi, baharia mwenzio nilikiona kilichomnyoa kanga manyoya
 
mzee aliwahii nitandikia kwenye banda la kuku wa nyama nilale naooo.

Miaka ya 90. Alivyo ona badoo hali ile ile akasema sasa unaenda kushindana na mbuzii kunyaa,na kukojoo akaniweka siku 3 kwenye banda la mbuziiii akija mbaoo hazifaiiii nguoo zotee ni maji tu kama nimetoka kuogelea.

In short walichoka wakaniachaaa.
Mkuu we ndo mwenyekiti wetu wa ukojozi heshima kwako..๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Ulistahiri kuimbiwa kindumbwendumbwe..๐Ÿ˜…
Mi ilikuwa nikinywa juice cola jua sikuhiyo mgodi lazima utatema.. Tena harufu ya mkojo itakuwa ileile ya colacola..๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Jamani kwa wale wakristu wezangu kuna kitu kinaitwa kipaimara mnakuwa mnafundishwa na mwalimu kwa mda wa miezi kadhaa na badae kunakuwa kipindi cha kukaribia kupata kipaimara lakini uwezi kupata hadi huulizwe maswali kuhusu ulichojifunza niliulizwa maswali nikaweza badae nikaambiwa nisali nia njema kila nikisali nachanganya na sala ya asubuhi ikabidi muuliza maswali aniambie nikamwambie mtu atakayenisimamia anifundishe tena nililia hapo nilishanunuliwa nguo za sikukuu nikaona sitapata kipaimara ndo basi tena.
Mimi kipaimara nilihudhuriaa siku nime lala kwenye benchii kuna jamaa alinipiga kofiii kama,anauwaa aisse nililia ile siku na sikurudi tena mpaka leoo mwaka wa 29
 
Kuna siku nikapanda juu ya mti sikuvaa chupi kupanda nikaweza kushuka nikashindwa nikaanza kuning'inia kwenye mti huku niko uchi waliokwepo chini wananicheka kabisa huku mimi nalia tu huko juu badae nikapata wazo la kujiachia kujitupa juu mpaka chini ha ha ha sitasahau
Wewe ni he/she?
 
Sistaako kumbe kama wangu. Alijuaga sana kunizodoa.

Siku moja kalala fofofo, mjeda usiku sikulala nimemkamia. Taratibu nikaingia chumbani kwao... mwanaume nikachomoa dudu na kumwaga kojo kitandani kwake taratibu kama nakamua jipu. Sister kuamka asubuhi anakuta kitanda kimeloa... Sista akauchuna kimtindo

Sasa mimi nikawa bwege, nikataka nimuumbue kwa maza. Nikaenda kumsemea. Mama akafanya ukaguzi akakuta kweli godoro limeloa... Sista akaulizwa akabaki kaduwaa...

Sasa huyu mazeri wangu alikuwa ticha, machale yakamcheza... akaniuliza wewe ulijuaje dadaako kajikojolea kitandani? Nilikuwa sijajipanga kwa hilo swali...

Wewe ni mtanzania mwenzangu na umepitia utotoni. Sina haja ya kukuambia kilichotokea kwangu siku hiyo... Ila ujue tu kwa ufupi, baharia mwenzio nilikiona kilichomnyoa kanga manyoya
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Ulitaka kufanya ujasusi wa kichochezi๐Ÿ˜‚
Vyema kabisa ulivyokamatwa..๐Ÿ˜…
 
Mkuu we ndo mwenyekiti wetu wa ukojozi heshima kwako..

Ulistahiri kuimbiwa kindumbwendumbwe..
Mi ilikuwa nikinywa juice cola jua sikuhiyo mgodi lazima utatema.. Tena harufu ya mkojo itakuwa ileile ya colacola..
Mimi kila siku iendayoo kwa munguu. Hakuna siku silimwagiii. Siku ikitokea sijakojoo basii nitakuwa na furaha kama nimepata tanzanite.

Ninywe maji nisinyee nishinde jaa nilee ila mzigoo lazima utemee. Sema kilicho niuma ni kuchelewa kuachaaa aisee sitaki hata kuongea na siku ime stop yenyewe kizembesana.
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Ulitaka kufanya ujasusi wa kichochezi๐Ÿ˜‚
Vyema kabisa ulivyokamatwa..๐Ÿ˜…
Dah nikajua ungenionea huruma...

Sitakusimulia tena majanga yaliyonipata utotoni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom