Hivi Vicky lengo lako haswa lilikuwa nini?

Hivi Vicky lengo lako haswa lilikuwa nini?

Mcheza Viduku

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2020
Posts
1,150
Reaction score
2,926
Hii ni story ndefu kidogo ndugu wajumbe, ni ya kweli kabisa sio chai kama ambavyo watu wanaweza kuiita, matukio mengi nimeyakata ili kupunguza urefu kwa hiyo kama mtakuwa na maswali kuhusu baadhi ya mambo niliyoyaruka ninaweza kuyajibu ikibidi, lakini pia mimi sio mtaalamu sana wa kuandika na kupangilia visa kwa mtiririko mzuri kwa hiyo naomba mnivumilie popote patakapokuwa na makosa.

Kama mara mbili hivi nilipandisha uzi kule jukwaa la Love Connect kutafuta rafiki atakaekuwa mpenzi, mchumba hadi kuwa mke wangu (nilikuwa serious kabisa sio masikhara) katika kusubiri subiri huku kila wakati nikichungulia Pm, hatimae akajitokeza Vicky (kwa heshima naomba tumtambue kwa jina hilo tu, na samahani kwa wenye jina hilo) tukaanza mahusiano ya awali kwa kutumiana jumbe kule kule PM huku tukifanya taratibu za kubadilishana namba za simu na kutengeneza mipango ya kuonana.

Akanipa namba yake ya simu na mimi nikampa ya kwangu, cha ajabu sasa yeye alinipa ile ambayo haitumii WhatsAp hata mimi pia sikufanya ivo (nadhani kila mmoja hakutaka kujiweka wazi mapema kwa mwenzie), maisha yakaendelea......sms za kimahaba zikaendelea hadi tukapanga siku rasmi ya kuonana ambayo ilikuwa jumapili 02/08/2020, likapangwa eneo la tukio na muda.

Siku ya miadi ikawadia nikajivuta mapema sana eneo la makutano huku ka moyo kanadunda sana, kwanza ni kule kwenda kuonana live na mwana JF mwenzangu, lakini la pili ni kwenda kuona matokeo ya nilipobet, nikabana kona moja nimetulia na ka bia kangu mezani huku nikiwa makini sana kwa kila anaeingia simu yangu nimeitolea mlio lakini mawasiliano na Vicky yanaendelea kwa usiri mkubwa huku nikimdanganya kwamba nakaribia kufika eneo la tukio, meza kama ya tatu hivi kushoto kwangu alikuwa amekaa jamaa mmoja hivi ambae kwa muonekano tu anaonekana ni mtata sana yani hakawii kuzingua, muda mwingi huyo bwana alikuwa bize na simu na wakati mwingine alikuwa akipigiwa anatoka kuongelea nje, hilo sikulitia manani sana kwa sababu pale kulikuwa na mziki.

Kuna kitu nilianza kukitilia shaka pale, kuna wakati nilijaribu kumpigia simu Vicky akakata halafu akanitumia sms hii "sms pls" lakin pia ilikuwa kila nikituma sms baada ya sekunde 5 hadi 8 hivi namuona jamaa nae anashughulika na simu na haupiti muda meseji inaingia kwenye simu yangu kujibu kile nilichouliza, na namba inayotumika ni ya Vicky. Hapo nikaanza kukaa 50/50.....nikampigia jamaa yangu mmoja mwehu mwehu hivi anapenda vurugu kuliko kula, nikampa mkanda mzima ulivyo na nikamueleza kuwa nahisi pale siko salama sana, akaniahidi atafika hapo.

Wakati huo nipo kwenye kumsubiri Vicky, lakini pia nipo kwenye wasiwasi wa nini kitatokea pindi tukionana, na muda huo namsubiri jamaa yangu ambae atakuwa pale kuni back up kwa lolote lile ambalo lingetokea kuhatarisha usalama wangu, nikiwa kwenye wakati mgumu wa kusubiri, pale mlango mkubwa wa kuingilia akaingia mdada mmoja hivi, alikuwa amependeza na pia ni mzuri tu wa kiwango cha uchumi wa kati, nikawa nafuatilia hatua zake hadi zikaenda kuishia kwa yule jamaa mtata, nikajikuta naionea wivu ile njemba kukaa na mtoto mzuri vile asiyeendana nae.

Kama dakika 3 au 5 hivi nikiwa bado naburudisha macho yangu kwa yule dada simu yangu ikapokea meseji mbili zilizoachana kama sekunde mbili hivi, sikuwa na haraka ya kushika simu (hii mbinu nilifundishwa na huyo rafiki yangu), sms ya kwanza ilikuwa kutoka kwa Vicky inasema ameshafika nimekaa upande gani, sms ya pili kutoka kwa jamaa yangu niliyemuita aje aokoe jahazi kama litataka kuzama, yeye pia alisema ameshafika na ameniona nisiwe na wasiwasi, yeye sikumjibu.....Vicky nikamuelekeza nilipokaa na nilivyovaa, lakini zikapita kama dakika 5 hivi bila kupokea majibu.

Pale kwenye meza ya jirani zangu niliona kama kuna ka msuguano ka chinichini kanaendelea, mwanamke ni kama anashurutishwa jambo fulani hivi, wakati nipo kwenye hatua za mwisho mwisho kuelekea kuwapuuzia nikashangazwa kuona jamaa kaachia kibao kikali sana kwa yule mwanamke, na wakati huo huo sms nyingine ikaingia kwenye simu yangu "dogo hao jirani zako ndio wabaya wako" nikashangaa wabaya wangu kivipi sasa, lakini pia nikashangazwa na ukimya wa Vicky kutokujibu sms yangu kwa wakati muafaka, nikaamua kupiga......

Wakati simu yangu inaita nikashuhudia jambo lingine pale kwenye meza ya jirani zangu pakavamiwa na utulivu wa ghafla, wote wakatazama kwenye simu yao iliyokuwa mezani, jamaa akamuangalia mwanamke halafu akamwambia kwa sauti niliyoisikia kabisa "kapokelee nje, na ole wako uniletee ujanja wako kishenzi hapa kumficha huyo malaya mwenzio leo nitakuumiza nakwambia" akatoka nje huku mimi nikifuatlia hatua zake kwa usiri mkubwa sana kuepusha li jamaa lisinione, lakin huku nikimuonea huruma kwa majanga ya kupigwa hadharani, na kwa mbaaaaaaali eti nikitamani yeye ndiye awe Vicky, kwa kweli alikuwa ni mzuri yule dada.

Hellow.......simu yangu ikapokelewa, roho yangu ikalipuka kwa hofu na tashtiti kubwa, aliyepokea simu ndio huyo aliyetoka hapo akiwa kalambwa kibao!!!! Nikakata simu na hapo hapo sms nyingine kutoka kwa jamaa yangu ikaingia "nadhani sasa umeniamini" yule dada ambae sasa nikaamini moja kwa moja ndiye Vicky akarudi kwenye meza yao "amesemaje" likawa swali la kwanza la yule jamaa yake "nimepokea akakata" akajibu. Kibao kingine kikali kikaunguruma kwenye shavu la Vicky

Nikampigia jamaa yangu nikamwambia tuondoke nikiamini kwa 100% huyo ndiye Vicky.......

Hebu wajumbe naomba tusaidiane kujaribu kuwaza na kujiuliza maswali haya

1- Hivi lengo la Vicky lilikuwa nini haswa kwangu, kuamua kunikubali huku akijua ana mume/bwana

2- Au amechoshwa na mahusiano aliyonayo anataka kujichomoa huko au alikuwa anataka kutengeneza uchepukaji tu.

3- Au walikuwa wanataka kutengeneza fumanizi ili wanipige hela, jamaa yake alifuma mawasiliano yangu na ya Vicky kwa bahati mbaya au walikusudia.

Tusaidiane kung'amua hilo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hapo walitaka kukugeuza mbuzi wa 'kafara'.

Uzuri umejitambua na nina uhakika ulicheza karata yako vizuri mtoto wa mjini.

Bila kufanya hivyo tungesikia habari ya mtu kuchanwa marinda tangu uchumi wa Kati uanze!
 
Kilicho kukwamisha kukosa mpenzi ktk mazingira yaliyo kuzunguka ninini?

Yawezekana Wapo kwenye mahusiano lkn sio ndoa, labda alitaka amtose huyo bwana ndo akaishia kufumwa.

Achana na mahusiano yasio eleweka. Tafuta mke kwenye mazingira yaliyo kuzunguka.
 
1. Na 2. Ndio yaweza kuwa uhalisia.

Ingekuwa kutaka kukubananisha, hayi yangefanywa bila kuvuta muda wala kusengo kuwa na makofi.

Yawezekana huyu dada ni mtu wa mambo mengi na ameshwa onywa sana, hasikiii hadi kufikia hatua jamaa anaona waminyane tu. Ndio hizo kauli za kuwa ole wako ufanye janja zako. Lakin jamaa alitegemea kukuta mtu anaye ruka na mkewe ni jirani, rafiki au anaye wafaham ili wanukishe, ila akakutana na mtu mwingine kabisa. Ndo maana hata hakuanzishiwa balaa, na wala si kwa ujanja wako kama udhanivyo.

Yawezdkan na mahusian ambayo Vicky, ameyachoka ,lakin anatokaje, anakwenda kwa nani. Labda jamaa ndo anamuweka mjini, so naye alikuwa anabet ukisomeka tu, atoroke.

Zote ni fikra,ila ukweli anao vicky na yule jamaaa mtata
 
Hahahahahahaha

Mchezo ufanyiwe ??? noooo... Demu asingepigwa 0%


Demu amechoshwa hayo mahusiano.... 51%



Demu kukubali uku akijua ana bwana 49%.



Mwisho wa siku, Shukuru maana Lijamaa lingekutia madole ya Tgoni kama alivo vicky.


Vicky Acha Ujinga.... Kama umechoshwa na Jamaa ,acha ujinga wa kukomaa naye.

Kama Jamaa anakuishi poa tu, acha ujinga wa Tamaaa.
 
Hamna hilo halikupangwa bali inaonesha huyo dem hajatulia,madem wa humu huwa wanadhani wanaume wa jf ni wasomi wana pesa ni matajiri kwaiyo alitaka ahamie jf akashtukiwa.
Nimpe pole vicky nimemuonea huruma kuliko wewe.
Wakina dada acheni tamaa ridhikeni na mliokuwa nao au achana na uliokuwa nae kisha sajili mwingine.
Wengine tumo humu hatuna uhakika wamaisha lakini jf tunakula bia, kuku na magar tunayo ila tunaendeshea humu.
Bila kusahau tunapiga bao1 kuanzia dk 45 na kuendelea.
 
Manzi za jf ni pasua kichwa,kuna baadhi ya app ukizikuta kwenye simu ya mkeo Anza kua makini nae.

Madem wa jf Kama sio wake za watu ni masingle mama alafu sasa akija pm utafikiri ndio kwanza anaingia 4m4.

Ongera kwa kutegua tego mwana.
 
Ni upumbavu mkubwa kumpiga Mke/mpenzi wako kibao hasa mkiwa sehemu ya starehe!

Ficha hasira na upumbavu wako mkamalizane nyumbani!

Kwani gunia la mkaa shingapi beans!
Mkuu mda mwingine kuzimaliza hasira zako mapema ni salama zaid iv unafikiri jamaa mbabe angemshika mkono Vick mpaka nyumban nn kingetokea maana pasingekuwepo na wakuwaamua
 
Hamna hilo halikupangwa bali inaonesha huyo dem hajatulia,madem wa humu huwa wanadhani wanaume wa jf ni wasomi wana pesa ni matajiri kwaiyo alitaka ahamie jf akashtukiwa.
Nimpe pole vicky nimemuonea huruma kuliko wewe.
Wakina dada acheni tamaa ridhikeni na mliokuwa nao au achana na uliokuwa nae kisha sajili mwingine.
Wengine tumo humu hatuna uhakika wamaisha lakini jf tunakula bia, kuku na magar tunayo ila tunaendeshea humu.
Bila kusahau tunapiga bao1 kuanzia dk 45 na kuendelea.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kwa hyo mkuu jf ni Chaka la kufichia umaskini na kufurahia utajiri hewa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom