Unakumbuka nini katika enzi za gazeti la Sani?

Hii ni Nakala ya gazeti la Sani la mwaka 1986 mwishoni kuelekea 1987 na kipindi hicho likiuzwa kwa shilingi 30 na Watanzania wakiburudika kwa katuni, hadithi, riwaya nk.

Wewe ulikuwa wapi kipindi hicho?

Tupe Taswira ya Taifa kipindi hicho (hata kama ulikuwa hujazaliwa ila umesoma au kuhadithiwa) katika nyanja za Elimu, Michezo, Burudani, Siasa nk.


Eleza kuhusu usafiri wa aina mbali mbali uliotumika miaka hiyo au hata kuweka picha zake.

Eleza kuhusu mavazi pendwa ya miaka hiyo na kila unachokijua kilitumia miaka hiyo na watu wa sasa hawavijui.

Lengo la uzi huu ni kukumbushana mambo ya miaka hiyo katika Taifa letu kwani wengine hawakupata fursa ya kuwepo miaka hiyo hivyo ni burudani tosha.

Picha ni muhimu sana....twende kazi.View attachment 1254454
Ila pimbi bishoo kitambo sana
 
Madenge ni mtu kabisa. Nilishawahi kukutana naye Tandale. Ila kwa sasa umri umesogea kidogo. Nilimpa 5,000 nikaachana naye. Namba yake nnayo
 
Miaka hiyo niliamini Madenge ni mtu kweli anaishi Dar es salaam.
Alikuwepo kweli pale Buguruni sokoni mtaa wa nyuma wowote unaitwa kwa Madenge japo sina uhakika na tabia zake kama zilifanya na kwenye gazeti.
 
Uhuru road
JamiiForums-1736884974.jpg
 
hivi haki miliki ya sani inahodhiwa na kampuni ipi kwa sasa ? halfu kwanini watu hwanunui haki miliki wakatutengenezea hata series ya animination ya wahusika toka ktk haya majarida
 
Back
Top Bottom