Unakumbuka nini katika enzi za gazeti la Sani?

nlkuwa nasoma Mzumbe Sec aiseh lile gazet limenibhrudsha sana, nktoka class tu ni kwenda Mzumbe Chuo kulitafuta kusoma stori na udaku mOto moto..dah limepotelea wapi?? hyo ni 2011 apo
 
Lodilofa alikuwa na majibu ya tofauti sana, Gari yake ilikuwa ya ukweli sana.

Madenge na mzee wake hawajawahi kuelewanaga.

Pimbi hajawahi fanikiwa kula Tunda

Na sijawahi kumuona Sokomoko Sober.

Hakukuwako DSTV mtaani kwetu kuangalia Manchester na Arsenal, kulikuwa na Sani unacheki Bush Stars Na watoto wa mjini kina chepe.


This thread takes me waaaaaaay back enzi nilizawadiwa T-Shirt ya sani
Kwa hiyo hakuwahi kula tunda kimasihara hahaaaaa
 
Miaka ile, katuni hizi zilikuwa maarufu kiasi kwamba baadhi yetu tulipewa majina ya katuni zile kama majina ya utani.

R.i.P Mtunzi wa katuni hizi marehemu
Philip Ndunguru, aliyefariki mwaka 1986 akiwa na umri wa miaka 24. Katuni zake ziliendelea kuleta tabasamu miaka kadhaa iliyofuata. Kwa kumkumbuka mtunzi huyu, na kufurahia kazi zake.
Daahh!

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom