Unakumbuka nini katika enzi za gazeti la Sani?

Tosha

Member
Aug 18, 2011
72
95
Unakumbuka nini kuhusiana na gazeti la sani mwishoni mwa miaka ya themanini na mwazoni mwa miaka ya tisini?

Nimekumbuka enzi zile za gazeti la SANI, jamaa walikuwa wabunifu sana kwa matoleo yao,unamkumbuka kifimbo cheza na misemo mbalimbali(uchafuzi wa lugha?), kipepe na rungu lake, pimbi a.k.a dr. love yeye anatongoza kila demu! ndumila kuwili na wizi wake,aah wapi lodi lofa na kagari kake na kiko yake kitambi kule!madenge na vituko vyake akiwa na matanati yake !kuna mhusika moja hivi alikuwa chapombe sikumbuki alikuwa anaitwa nani vile?sukununu za babu sani je?wapi mechi ya bush star na born town?aah yale mazoezi kabla ya mechi hoiiii!uwanja wa fujo je? Hadithi za picha mambo ya kina Obi, Mzee Ole, Linda n.k ,wachapishaji walikuwa wabunifu kweli kweli, burudani zilizobebwa na wahusika wa kutengeneza lakini wanashambiiana na jamii!ilikuwa burudani sana kweli natamani ijirudie!


Wachoraji wa enzi zile ni kina John Kaduma(nasikia ni marehemu kweli?), Ibra Radi Washokera ndo ninaowakumbuka kama unakumbka wengine tukumbushane, watunzi wa hadithi pia walikua kina… aah km unakumbuka naomba tunikumbushe!

Jamaa walikuwa wakitoa toleo jipya basi wenye nazo wananunua then sisi wengine tunasubiria kuazima km ni shule basi utaona kikundi cha watu kibao wanasoma gazeti moja au km ni mtaani basi ndio kuazimana na ugomvi tele!natamani km nikusanye nakala za matoleo yale ya zamani!

Je wewe mdau unakumbuka nini katika gazeti la SANI?vipi kuhusu wahusika wake?hadithi na vituko je? 

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,338
1,225
Mh.Tosha umenifanya hadi nimepata huzuni ghafla.
Kwani imenikumbusha marehemu wengi niliokua nao nyakati hizo, aidha na wengi nisiojua wahai, ama wafu.
Nakumbuka vita ya aunt Zena & Betina !
Hadithi ya Mz Mayuku, Mz Ole.
Na mwenyewe Mz S.m Bawji
 

testa

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
442
250
Yule cha pombe alikuwa anaitwa Sokomoko,bado umesahau adithi ya Obi,Linda na mkulu Zumo ilikuwa balaa,gazeti lilianza kupoteza mwelekeo baada ya mchoraji mkuu kutoka Iringa John Kaduma kufariki
 

Tosha

Member
Aug 18, 2011
72
95
[Mh.Tosha umenifanya hadi nimepata huzuni ghafla.
Kwani imenikumbusha marehemu wengi niliokua nao nyakati hizo, aidha na wengi nisiojua wahai, ama wafu.
Nakumbuka vita ya aunt Zena & Betina !
Hadithi ya Mz Mayuku, Mz Ole.
Na mwenyewe Mz S.m Bawji]

Pole mkuu Jugment kwa huzuni lakini ndo hivyo tena ilikuwa enzi nzuri sana na natamni vipajivile viwepoleo hii!
ooh umenikumbusha betina mwembamba nyuma kapigwa pasi lakini matata huyoooo ngumi mkononi!yaani wale wahusika wanafanana sana na watu halisi katika jamii yetu!

Testa kumbe kweli Mchora Kaduma alifariki ooh jamani! (RIP JOHN Kaduma)
 

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,816
2,000
nakumbuka mechi za kina mapungo,vituko vya pimbi kila siku anahangaika kupiga sound bila nafanikio,zena na betina loh ,hivi wamiliki walifilisika ?
 

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,364
2,000
muasisi wa katuni na vikaragosi vya sani alikuwa PHILLIP NDUNGURU-RIP
 

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,393
2,000
Mechi ya Bush staz na Born town, kipa wa bush Madenge. Mzee Meko anapiga kona na kwenda kufunga mwenyewe!
 

nitonye

JF-Expert Member
Dec 18, 2011
7,275
2,000
Aisee nikimkumbuka Ndumila Kuwili na wizi wake nacheka sana alimtapeli jamaa madini akamucha kwenye lifti. Na pia ile mechi ya watani
 

Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,024
1,500
lodi lofa na madenge nilikuwa nawapenda sana.
Na zile riwaya za mapenzi sijui oscar, lilian, victor na nani vile, nshaaahau.
 

testa

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
442
250
Mechi ya Bush staz na Born town, kipa wa bush Madenge. Mzee Meko anapiga kona na kwenda kufunga mwenyewe!

hahahaaa..Kali ni ile mechi ya mabush star na maborn town mpira umepigwa golini kwa maborn town beki ni lodi lofa anaupisha mpira huku akimwambia golikipa wao "angalia huo mpira"golikipa nae anautazama ukiingia golini badala ya kuudaka zinatokea ngumi za lodi na kipa wake,yalikuwa yananichosha maandalizi yao kabla ya mechi
 

Puppy

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,843
2,000
Lodilofa alikuwa na majibu ya tofauti sana, Gari yake ilikuwa ya ukweli sana.

Madenge na mzee wake hawajawahi kuelewanaga.

Pimbi hajawahi fanikiwa kula Tunda

Na sijawahi kumuona Sokomoko Sober.

Hakukuwako DSTV mtaani kwetu kuangalia Manchester na Arsenal, kulikuwa na Sani unacheki Bush Stars Na watoto wa mjini kina chepe.


This thread takes me waaaaaaay back enzi nilizawadiwa T-Shirt ya sani
 

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,605
2,000
Mechi ya born town na bush stars ilikuwa kiboko. Wakati wa maandalizi ya mechi tizi la bush stars lilikuwa kiboko maana walikuwa wanakwea milima na kuruka visiki ajabuuu...
 

Puppy

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,843
2,000
nakumbuka mechi za kina mapungo,vituko vya pimbi kila siku anahangaika kupiga sound bila nafanikio,zena na betina loh ,hivi wamiliki walifilisika ?Kina mapungo wakapata mpaka usajili ulaya wakaenda wakarudi, walibadilika hao wakawa masharobaro
 

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
0
Kina mapungo wakapata mpaka usajili ulaya wakaenda wakarudi, walibadilika hao wakawa masharobaro

Umechanganya kidogo mkuu, golden boy mapungo alikuwa katika jarida la bongo. Pia enzi zile kulikuwa na gazeti pinzani la sani lilikuwa linaitwa busara.
 

muwaha

JF-Expert Member
May 13, 2009
741
195
Namkumbuka Obi na Linda, na shemeji yake Seba. Bila kumsahau Mzee Ole.
 

mwakaboko

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
1,905
2,000
the good old but gold days, hadithi murua, vituko vya madenge nad baba yake, lodilofa ,nk
 

Leonard Robert

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
10,085
2,000
mimi nalikumbuka sana bongo..hasa njomba nchumali,mapungo..na michoro kama ya kifo cha 2pc ilikua balaa tupu..mapungo kwa sasa ni kama balotel.
 

Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,224
1,195
Dah!mie nilikuwa nakoma na mazoezi ya bush star yani yule kocha angetokea na kupewa taifa star sijui km watu wangelogana kupata namba!

Yani wajamaa walikuwa wanakalia visiki vya ajabu tena bila kuvaa ngua mara saa ingine wachemshwe yaani mpaka nilikuwa nayajenga yale matukio kichwan mpaka naota lol!
 

Ralphryder

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
4,674
2,000
Hivi,kile kisa cha Mzee Meko ambaye alikuja mjini kununua trekta! akakumbana na akina ndumila kuwila kuna anayekikumbuka vizuri?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom