Kuna wakati Mapung'o alipata timu ulaya...teh teh!!
Nakumbuka alishuka airport akiwa amepga boonge la ReebokKuna wakati Mapung'o alipata timu ulaya...teh teh!!
Namkumbuka Chino, Mayuku, Obi! Nilikuwaga sikosi series ya hii kitu.View attachment 581042
View attachment 581043
View attachment 581044
View attachment 581045
View attachment 581046
View attachment 581047
View attachment 581048
View attachment 581049
View attachment 581050
View attachment 581051
Unakumbuka nini ,wapi Mhenga mwenzangu?
Na sijui hili gazeti lilipoteleaga wapi.
Hahahah kitambo sana ni vile tu hazeeki.Pimbi kaanza umalaya zaman
Mtu akiwa na gazeti hilo ilikuwa anathaminiwa sanaSeries za enzi zetu, kitu unakisubiri hadi basi na ukisikia kimetoka ni balaa tupu
Dah! Hongera mkuu...hakika miaka hiyo dunia ilikuwa na raha zake.Nilikuwepo, japo nilikuwa dogo lakini nilijua kusoma na kuandika. Hili toleo lilikuwa linatoka mara 1 kwa mwezi mara mbili kama sikosei.
Nilikuwa moshi ambapo ndio kwetu. Nakumbuka kipindi hiko mabasi ya town trip kcmc, kiboriloni yalikuwa ni SHIMAWIMO. Yaani (SHIrika la MAendeleo WIlaya ya MOshi)
Kumbi za cinema zilikuwa mbili. ABC na Plaza Cinema. Nilikuwa sikosi kwenda pale plaza kila jumapili saa nne kuangalia sinema. Hata kama sijapewa hela na mshua lazima niende ongalao niambulie fungulia mbwa.
Masteling wa wakati huo, Amitha Batchan, Mithuny Chakraborty, Rish Kopoor,Rajesh Kumar, Denzolpa, kwa upande wa kina mama walikuwepo kina Jaya, Hemma Malini, nk.
Movie nazozikumbika, Nasseb,Amne Samne, nk. Kotambo sana.
Kumbi za disco zilikuwa ni Vijana club, Libert hotel iliyokuwa karibu na green view ambayo ilikuja kuungua baadae.
Mafuta ya kupaka wakati huo ni YOU na YOLANDA yaliyokuwa kwenye mkebe. Mengine ni rays, Ashanti. Wajanja walikuwa wanavaa jenzi na rabber mtoni kama Ascot. Suruali za kitambaa zilikuwa Cacha rell, Mr Dio nk.
Wahusika wa kuu kwenye kazeti la Sani. Kipepe, Lodi lofa, Sokomoka, Pimbi, Madenge,na Yule mpiga roba nani sijui nimemsahau.
Mc Sukununu.
Hadithi zilizowahi kutamba wakati huo kwenye gazeti la sani na mtunzi akiwa marehemu Hammie Rajab ni pamoja na Pumbazo La moyo, Usiku waGiza ya Joyce na Dalanda na kibibi Gula.
Dah muda umeenda aisee, ila kama juzi tu.