Unakumbuka nini katika enzi za gazeti la Sani?

LODI LOFA - Enzi za gazeti la Sani, misemo mipya kila toleo! kweli kukosa toleo moja ilikuwa zambi


553072_308355669311232_163297764_n.jpg
 
We acha tu mkuu yaani ilikuwa raha sana, nilikuwa nalipenda sana hili jarida, kitu tapeli Ndumilakuwili huyu jamaa zake ni mazabe tu, pale kuna dr love Pimbi huyu jamaa ana lugha tamu sana ya kukamata mademu lakini hafanikiwi kuduu nao!
 
Jitu la miraba mitatu Dkt Zumo,
hii story ilikua inanihamasisha kujifunza kutumia mtutu. Sema bac tu ila ww ngoja naona March 23 iko karibu. Na hivi msure ashatangaza hatuchukui mateka:laser:
 
We acha tu mkuu yaani ilikuwa raha sana, nilikuwa nalipenda sana hili jarida, kitu tapeli Ndumilakuwili huyu jamaa zake ni mazabe tu, pale kuna dr love Pimbi huyu jamaa ana lugha tamu sana ya kukamata mademu lakini hafanikiwi kuduu nao!

hahaha kuna vitu enzi za mwalim vilikuwa safi sana!! Mzee sokomoko yeye na ugimbi tuu, Kipepe mzee mapori eti lodi lofa alikwenda uwanjani akakuta timu zinapiga mechi, Lodi lofa akashangaa kishenzi wanaume 22 wanagombania mpira mmoja, si akaenda dukani akanunua mipira 22 akawagawia wachezaji wote ili wasigombanie mpira mmoja!
 
Mmenikumbusha mbali...Chino alikuwa amejaza balaa....bila kusahau mapenzi ya Linda na Obi

Chino!, yaani hili hili dubwana lilikuwa linafungiwa kwenye pango na lilifunguliwa kwa kazi maalum hasa pale wanapozidiwa!
 
Mambo ya John Kaduma (r.i.p)

Ki ukweli bado sijapata kuona mchoraji mahiri kama huyu. Huyu ndiyo kioo cha wachoraji wengi Tanzania, lakini cha kushangaza sijaona juhudi zozote za kumkumbuka huyu mtu na kuenz kaz zake.
 
Mzee Mwinyimpeku alikua hapitwi na story ya kitaa

Vijana wa kitaa walimkoma sana huyu mzee, ile bakora yake ndiyo aliitumia kuwakamatia na kuwachapa, alikuwa hapendi kabisa kuona kiswahili kikiharibiwa na hao wahuni.
 
Siku moja Ndumila Kuwili aliiba TV walipokuwa kwenye kibanda kuangalia kombe la dunia. Umeme ulipokatika tu jamaa akajitwisha TV huyooo mtaani akakutana na Polisi wa doria ya usiku akawa anajisemesha "Rijama rimenunua kideo". Umeme uliporudi watu aaaaaaaaaaaaaahhhh...Hivi naweza kupata wapi yale majarida?
 
Back
Top Bottom