Unakumbuka nini enzi za JKT?

Unakumbuka nini enzi za JKT?

Foffana

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2022
Posts
2,687
Reaction score
4,383
Habari zenu Wakuu
Natumaini mnaendelea vyema kabisa.Leo nimeona tuweze kushare matukio au mambo ambayo tulikutana nayo tukiwa katika makambi ya JKT iwe kwa mujibu wa sheria au kujitolea

Tukio ambalo sitolisahau ni kwenye kambi X tukiwa tunapiga kozi yetu na ikiwa tayari ishachanganya kilikuwa na kipindi cha sikukuu bhana ya Eid ya kuchinja kama wanayoiitaga wenyewe

Basi pale kambini kukaletwa ng'ombe wa kushato sijui hata Kibopa gani alijilipua watu tukasema mambo si ndo haya bhana leo mwendo wa minofu tu

Basi tukawa tunapiga kazi kwa morali mwenye kulima anapiga jembe kisawa sawa mwenye kujenga nae anatimiza wajibu wake hadi madoja nao hiyo siku ilibidi wawe karibu karibu wasije kupitwa na neema hiyo

Basi mang'ombe yalikuwa yanaingia tu likitoka gari hili linaingia hili na maandalizi jikoni yakiendeleaa

Hadi mda wa chakula ulivyofika tusogea mess kupata makulaji eeh bhana eeh tulikutana na nyama moja moja tena ni kipande kidogo sana tukawa twajiuliza ming'ombe yote ile iloingia ila tukasema fresh may be wamebakisha na siku zingine wiki hii yote tunaweza tukagusa nyama tu

Kumbe bhana kuna utitiri wa manyama yalikuwa yanafaulishwa na wajeda kwenda majumbani kwao mana nakumbuka walikuwa wanapita kwenye mahanga wakikuta ndoo wanapita nayo 🤣 wanaenda kujaza manyama wanapakia kwenye magari yao wanasepa nayo hawa wajomba wanafurahisha sana

Sasa hawakuweza kumaliza yote kuna lundo tu likabaki wakaiacha haikupikwa bado sasa nadhani kwenye utunzaji haukuwa vzuri mpaka ikaharibika kabisa na wao nahisi hawakuweza kugundua ilivyofika siku ya kupika nyama wakaipika watu wakala hvo hvo matokeo yake sasa

Tatizo la kuharisha almost kila mtu katika kambi alipatwa na hiyo kadhia watu waliharisha sana na kulikuwa na uhaba wa vyoo kulingana na idadi ya watu matokeo yake huko maporini watu walijisaidia hovyo sana

Ni Mungu tu alituokoa ndani ya siku mbili tulitaabika sanaa yaani sio makuruti sio maservice man hata hao wajeda nao walipatwa na hilo tatizo ilikuwa patashika mtu unaweka machupa matatu ya maji kwenye rasketi ngoma ikipiga hodi unatafuta kichaka🤣🤣

Ni kipindi kigumu kilikuwa nakumbuka tulikuwa tumefolen night tumbo likaanza kuzingua nikakimbia chap chap bombanj kuchukua maji nikazama porini usiku ile kutafuta chaka nashusha mambo nikastuka kuona mbele yangu kuna mtu mdada kuruti alikuwa naye anashusha mambo na alikuwa na kachupa kadogo ka maji ikabidi aje kuniomba maji bila aibu🤣

Niwatakie mchana mwema
"Amani ni tunda la haki pasipo na haki hakuna amani"
 
Kupigwa banzi, na mtama ukawa mwisho wa kwenda uwanjani,

Afande akasema ambao hawawez kwata tokeni mbele nikawa wa kwanza, na akadai kesho tungefikishwa kwa kamanda kikosi,

Kesho yake akaamka anaumwa na kuandikiwa c2, hivyo hakuweza kutekeleza mpango wake na tokea hapo tukawa washikaj sana,

Nakumbuka tunapangwa kwenye makundi kama kwata, ngoma, single, Kombat akanitoa akaniambia hizi sio kazi wewe ni mujibu wa Sheria tuu, njoo nikupeleke jikoni huko nikaingia huko mpk naapa,
 
Kwahiyo fatiki yako ilikuwa jikoni tu hadi unaapa hata usiku ulikuwa huendi kufoleni?
 
Kwahiyo fatiki yako ilikuwa jikoni tu hadi unaapa hata usiku ulikuwa huendi kufoleni?
Kwani muda wa kula inakuwa saa ngp? Nadhani ni kumi na mbili jion mpk moja kasoro mzabuni amemaliza kazi na jikoni sana sana labda kukanda ngano ya mikate, lkn usiku naenda ku foleni nikaimbishe chenja
 
Ila maovyo ovyo na doso ulikutana nayo🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom