Unajua vyuo vya Mtwara! Pitia hapa...

Unajua vyuo vya Mtwara! Pitia hapa...

MR LINKO

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2016
Posts
3,034
Reaction score
3,544
Habari wandugu,

Nilikuwa naomba kujua vyuo ambavyo viko Mtwara vile bora.
Kuna binti mmoja anataka kusoma sasa kaniomba msaada na mimi sio mwenyeji wa huko wala sijawai kufika Mtwara na kaniomba ni mchagulie chuo kizuri sana sana cha nursing maana ndo kamaliza 4m 4

Nitashukuru sana

xc.JPG
 
Mwambie akasomee ufundi VETA, hasa hasa secretarial courses. Hata akienda kusomea ualimu siku hizi hakuna ajira.
VETA wana vyuo kila mkoa, nadhani na Mtwara watakuwa nacho.
sawa mkuu ila yeye amefauli kiwango cha kwenda 5 sema hataki
 
Kuna sauti na utumishi ndio wanatoa kozi ya sheria. Kwa mtazamo wangu aende utumishi wako poa
 
Aombe STEMMUCO ni university college ya SAUT. Wana diploma na certificate za sheria.
 
Vyuo vya Mtwara
VETA- Hiki chuo kipo maeneo flani hizi hatari sana yaani kila siku upo beach kwa kweli kwa pembeni wana hotel linaitwa Naf Hotel huku mbele kuna Beach, Chuo kuna mazingira mazuri tu ya kusoma, lakini pia ujihadhari maana wanafunzi wa day na bweni wakiwa free basi wanaenda kupumzika baharini so uroda tu hapo.
  • Lab
  • Computer courses
  • Drivings
  • na vingine vingiii
King alexander college_ Hapa ndio utaamini vyuo vya mtwara vimepata location mzuri hiki pia hawako mbali na bahari lakini ni mbali kwa stand kuu wapo na shule fulani inaitwa King David schools, na kwa zamani kulikuwa na club flan inaitwa LAsindimba Disco Show maarufu kama LITINGI, IKi ni chuo cha habari.
  • Journalism
  • TV & Radio Boroadcasting
  • Mass communication
TPSC- Sifa ya hivi vyuo vingi vipo maeneo ya ufukwemi na hawa wapo na ufukwe beach wanaenda sekunde kadhaa tu, miaka ile kulikuwa na sehemu wanaita millenium but kwa sasa wana police mess ambapo kila wikiendi burudani tu.
  • Secretary courses
  • Record keeping
  • nk
STEMMUCO- Hili ni tawi la SAUT kama vile Jordan cha morogoro, Location ipo beach kama nilivyosema svyuo vingi vipo baharini, wanafunzi wa hapa kila siku wako chuoni ili waende kuvuka na pantoni wakafanye ufuska upande wa pili wa bahari.
  • Law
  • BBA na diploma
  • Education
  • Philosophy
TUA (tanzania university of accountant)- Tawi la uhasibu mtwara TIA, but siku hizi naona wanajiita TUA chuo kwa sasa kipo eneo fupi kutoka stendi kuu, chuo kina fensi ila wanafunzi wa hapa sifa chipsi mayai tu unakula mzigo, ila wanafunzi wakiume wengi wako busy na mambo yao kama hawapo chuo, ila soon chuo kinahamishwa kuelekea maeneo ya Mji mpya ambapo chuo kilikuwa kinajengwa na awamu ya kwanza imekamilika, na mpaka sasa hawatoi degree ni diploma na cheti
  • Logistics
  • Accountancy
  • Human resources
  • DBA
  • Procurement and supply
Chuo cha Uhazili- Hapa naona wanasoma ngazi ya cheti tu.

Open University of Tanzania- Hiki chuo wanafunzi wachache alafu wengi wafanyakazi kiukweli hakuna muamko wa watu kujiuanga,
kozi kama education, law nk zipo
 
Mm nipo Sauti ila hapa Saut hawatoi kozi ya nurse bali wana course nyingine ambazo ni community development ngazi ya dip na certificate, account, Kuna chuo cha NTC kipo Ligula ndo wa natoa nurse, Kuna utumishi, Kuna TIA na VETA
 
Mtwara vyuo vya nursing ni vng.. Asubir muda wa maombi Nacte wakifungua dirisha aombe
 
Lakini mkuu kwa matokeo hayo nursing ni ngumu hebu angalia anaufaulu wa BIOLOGY TU tens kapata D hapo aangalie kozi nyingine tofauti na hiyo kozi kama za KILIMO mifugo na afya hawez pata mkuu
 
Back
Top Bottom