Unajua kwanini Mwakyembe alikaa kimya?

Unajua kwanini Mwakyembe alikaa kimya?

Mwakyembe aliingia bungeeni na kutaka kutuaminisha kuwa mahakama imetuzuia kujadili mambo yatokanayo na PAC. Tena kwa kujifanya mkali akatuambia tuiombe radhi mahakama kumbe alikuwa katumwa na mafisadi. Hiki kitendo kimemshushia sana heshima huyu Harison
Teh teh teh!alikuwa anataka kumtetea rafiki yake Victor Mwambalaswa mbunge wa Lupa!
 
Tunaomba issue ya mwakyembe ianze kujadiliwa na wana jf.
 
mwakyembe hana lolote la maana yuko njia moja na MAFISADI alisha poteza uadilifu ndio maana yuko tayari kuwalinda name haaminiki kabisa.

Sio kupoteza uadilifu, hajawahi kabisa kuwa mwadilifu. Lile sakata la richmond tatizo lilikuwa ni "uwaziri mkuu" kwahiyo alipopata upenyo akatumia fursa effectively.
 
Mwambalaswa ni mwenyekiti wa kamati ya nishati, pia kama sijakosea ntasahihishwa ni makamu mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya tanesco

Pia ni ndugu yake na msemaji wa familia ya Mwakyembe wakati wa ugonjwa wa Mwakyembe. Ndiye aliyewaambia wanahabari kwamba Mwakyembe kapewa sumu na mafisadi.
 
Lukuvi na Januari walikuwa wapi? Sikuwasikia hawa wasemaji na viherehere vyao vyote vya kila siku
 
Kati ya watu wanaopiga nchi hii kw makeke ni mwakyembe
 
Hoja ya mjadala kuahirishwa kutokana na uamuzi wa mahakama ulikuwa ni mkakati wa Serikali kujinusuru. Mimi naamini Dkt Mwakyembe hakuitoa kama hoja yake mwenyewe bali alitumwa na sheria ikiaminika kuwa kwa sehemu kubwa anaheshimika ndani ya Bunge mbali na ukweli kuwa ni mwanasheria pia.
 
Mwakyembe dili yake ya bandarini na
kiwanja cha bilioni moja alichonunua Bahari beach tayari wabunge kama akina Mdee wanajua. Aliogopa kulipuliwa bungeni.

Pia kuhusika kwa marafiki zake Werema na Mwambalaswa kulimfanya awe bubu.

Mwanzoni alijaribu kushauri bunge litii amri ya mahakama.
 
Katika sakata la escrow mh Harison Mwakymbe alitaka kusababisha mjadala usiendelee baada ya kuja na hoja ya Mahakama. Wabunge wengine walimshtukia kwamba ametumwa na wakampuuza. Sasa wakati sakata linaendelea aliona aibu sana maana kaidhalilisha taaluma yake ikambidi akaekimya mwanzo mwisho.

SISI WANAKYELA TUNASEMA KWAMBA HUU NDIO MSIMU WAKE WA MWISHO WA UBUNGE , ataFUTE KAZI YA KUFANYA MAPEMA , HATUTAKI LAWAMA , ' ALILE KAKO '
 
Mwakyembe aliingia bungeeni na kutaka kutuaminisha kuwa mahakama imetuzuia kujadili mambo yatokanayo na PAC. Tena kwa kujifanya mkali akatuambia tuiombe radhi mahakama kumbe alikuwa katumwa na mafisadi. Hiki kitendo kimemshushia sana heshima huyu Harison

Huyu Mwakie mwisho wake utakuwa Ilima,kwa wale watu wa Kyela huyu ndugu sioni anachokifanya aishie Ilima
 
Januari Makamba naye je? Membe je? Waliongea nini? Au hawakuwepo?
 
Sikumsikia selasini sijui yupo

Selasini aliongea mbona au sababu ya umeme kukatika mkuu,pia muda ulikuwa kidogo haikuwa kila mbunge achangie ingawa kuna wengine waliutumia vibaya huo muda kwani walichangia pumba
 
Mwambalaswa ni mwenyekiti wa kamati ya nishati, pia kama sijakosea ntasahihishwa ni makamu mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya tanesco
Uwajibikaji upo wapi kama ni hivi?. Kuna conflict of interest. Wabunge wanapaswa kutokuwa kwenye Bodi za mashirika ya umma. Na ndio GOOD GOVERNANCE.
 
Anajua kuweka ndugu zake kwenye mashirika yalio chiniyake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom