Unajua kwanini Mabasi yakaitwa Ester Luxury Coach?

Hizo fununu hazijaanza leo na kila mtu alikuwa anazisikia. Kama si za kweli, kwa nini wahusika hawakuona umuhimu wa kujitokeza kukanusha. Hili pia linawahusu wale Lake Oil.
kwanini waseme ya mwigulu? kwanini wasiseme labda ya majaliwa au abduli?

Watu wakishaamua lao huwezi wabadilisha. Vitu vingapi vilikua vya Ridhiwan miaka ile? Simtetei MN by any means ila huu ndo uhalisia wa watanganyika.
 
kwa hiyo huyu mama ndio mmiliki wa Esther?
Esther Luxury Coach ni jina tu la kampuni

Ukitaka kujua mmiliki halisi, tafuta nyaraka za kisheria za kampuni hiyo ambazo hata yeye hajazionesha ktk kujitetea kwake

Au basi wafanye hivi. Ajitokeze mmiliki halisi wa kampuni hiyo, atoe nyaraka zote za kisheria kuonesha nyaraka za kisheria ambazo kila mtu anaweza kuzi - verify toka mamlaka za usajili wa biashara.
 
Watu wakishaamua lao huwezi wabadilisha. Vitu vingapi vilikua vya Ridhiwan miaka ile? Simtetei MN by any means ila huu ndo uhalisia wa watanganyika.
Jana siyo leo. Pia watu wanaona na kujua mengi.
 
Zamani kila kitu kilikua cha Ridhiwan hata ukijenga nyumba wewe watu wanasema ya Ridhiwan. Kuna uwezekano mkubwa sana haya mabasi sio ya MN na hana uhusiano wowote ule na mmiliki wake ila wabongo wana caption yao tayari. Wabongo wape picha tu maelezo wataweka wenyewe.
Sasa si simple tu wamiliki wajitokeze kuclear the air .
 
Hata wakijitokeza nani ataamini?

Lake oil kila mtu anajua wamiliki wake ila bado watu wanaamini ni ya JK na walichoma moto sheli na tankers zake kwa sababu hiyo tu. Mtu anaamini anachotaka kuamini.
 
Jana siyo leo. Pia watu wanaona na kujua mengi.

Kila mtu anajua Lake oil ya nani ila bado wanasema ya JK na wamechoma vituo. Simtetei MN hata kidogo ila Watu wanaamini wanachotaka kuamini hata useme nini.
 
Kwa nini wahusika walikuwa wanasikia hizo fununu siku hizo zote ila hawazikanushi hadi yalipotokea haya?
 
Kwamba wawe wanatoka hadharani kusema mali ni zao? Who does that? Ili mseme anajishtukia sio zake kweli?

Lini GSM au Bakhressa wametoka kusema mali zao ni zao kweli? Lake oil ni kama wao tu hana sababu yeyote ya kutoka kujitangaza. Acha watu waamini wanachotaka kuamini.
 
Sasa kwa nini wametoka sasa kukanusha? Si wangeendelea kukaa kimya
 
Nani katoka? Lake oil amekanusha? Mwenye mabasi ya Esther amekanusha? Hao insurance zitawalipa, they're good.
 
Lake Oil wamekanusha. Na hao Esther kama hawajatoka wajiandae kisaikolojia ingawa ni wazi "coincidences" zinathibitisha fununu
 
Kwahiyo sasa unaamini JK hana ubia na LO kwa kuambiwa tu au bado unaamini unachotaka kuamini?
 
Kukanusha kidogo kunafanya fununu zikose nguvu ila wewe hauamini kama kufanya hivyo kuna umuhimu wowote.
 
Hata MN amewahi kukanusha mabasi sio yake back in 2022 ila hadi leo wabongo wanaamini ni yake na bado wameyachoma moto wakiamini wanamkomoa MN. Mtu anaamini anachotaka kuamini hata umwambie vp.

Alikana Singida BS siyo yake ila dalili zote zinaonyesha zina mkono wake. Mwisho wakaamua kumficha kwenye chaka la "Mlezi".

Haya yote yanawezekana kwenye nchi inayoendeshwa kihuni.
 
That's what I'm saying hata akane bado wanaoamini ni yake watasema kafichwa. Acha watu waamini wanachotaka kuamini.
 
Umetumia akili za kuvukia barabara kufikiri na hata kwa akili hizo bado unaweza kugongwa na baiskeli.
 
Kama sijagongwa hadi leo basi, I might be doing something right.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom