Unajua kupigika? Nilikuwa nimepigika nikapigika haswaaa!! nasijui nilitokaje?

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,160
11,483
Mara nikamaliza Chuo na kupata kazi safi yenye maslahi si haba! Kutokana na kutojitambua nikaishia kupoteza ajira kutokana na totooz na ulevi! Nikaangukia pua mpaka chini kabisa! Yaani mpaka aibu! Nikajisajili kusoma Masters UDSM na kupata admission. Sasa shida ikawa kusajiliwa kwasababu ulitakiwa uonyeshe sponsor au uwezo wako wa kipesa kuweza kusoma!

Mimi nikawapiga sound na kunisajiri! Masomo yakaanza sijalipa karo na sina kitambulisho hivyo kuwa ngumu kuingia darasani! Huku nadaiwa kodi ya chumba nilichokuwa napanga! Hela ya kula sina! Nimekonda mpaka mbavu za kuhesabu huku macho yamenitoka njee na jasho la Dar! I seeeh!! Nakumbuka wakati huo sera za kuchangia gharama za Chuo Kikuu na kuanzisha Bodi ya mikopo zikaanza kutekelezwa.

Bodi ya mikopo hapo mwanzo ilikuwa kwa ajili ya Undergraduate (Degree ya kwanza) kwahiyo mimi nikapiga mwamba! Duuuh! Unajua nini? Aya maisha acha tuu! Hapo baadaye chuo nikaja kuona aliyekuwa na changamoto ya kulipa karo hakuwa mimi peke yangu kumbe wengi zaidi ya %70 hawakuwa na udhamini!

Basi tukajiunga pamoja na kwenda kumvaa Nimrod Mkono (RIP) kipindi hicho ndo alikuwa mkurugenzi wa Bodi ya mikopo! Basi vuta nikuvute huku na huku mwishowe tukakubaliwa kupewa mkopo wanafunzi wa Postgraduate!

Huo mkopo wa Loan Board ndo ulikuwa kama cheche ya moto katika petrol kuniwezesha kutoboa! Nawapa moyo vijana wanojitafuta kuwa watumie bongo na akili zao na macho yao ya ndani! Fursa za kutoboa zipo!

Kila Halmashauri ina mamillion ya hela kwa ajili ya kuwakopesha vijana! Ebu jaribu kujiunga pamoja na nendeni Halmashauri mnaweza kupata pa kuanzia!
 
Wewe jamaa bhna!

Umesema mpaka ulipo anza kupokea hela mkopo wa masomo ndio ukaanza kutoboa. Kwa hiyo kila mtu atatoboa kupitia hela ya mkopo wa masomo.?

Huko halmashauri unafikiri ni rahisi sana? Kijana jobless unafikri wanampa huo mkopo?
 
Ngoja waje Mimi mwenyewe natafuta njia ya kutoboa, mamlaka za uteuzi zipo wapi! By the way June 2024 nitakukuwa headquarters
 
Wewe jamaa bhna!

Umesema mpaka ulipo anza kupokea hela mkopo wa masomo ndio ukaanza kutoboa. Kwa hiyo kila mtu atatoboa kupitia hela ya mkopo wa masomo.?

Huko halmashauri unafikiri ni rahisi sana? Kijana jobless unafikri wanampa huo mkopo?
Wajiunge pamoja! Nasisi kubadilisha sera za wanufaika wa mkopo wa loan board kutoka undergraduate pekee na kuwaingiza postgraduate ilikuwa ni vita!
 
Hiyo pesa ya halmashauri sio rahisi hivyo kuipata japo na sisi vijana tuna kauzembe pia.
 
Back
Top Bottom