Unajua historia ya bendera ya taifa lako tangu 1885?

bendera yetu hubadilika mara kwa mara!bendera ya sasa huchanika na kupauka baada ya muda mfupi sana !
 
ningependa kabla mjadala haujashika kasi mleta mada atuhakikishie kuwa hakuna mgongano wa kimaslahi.
Isije ikawa umekosa tenda ya kutengeneza bendera sasa umeamua kumuharibia mwenzako.
 
hiyo ni bendera ya tanzania bara na si tanzania nzima zipo tofauti kiasi
 
Huu ujio wa huyu Obama utaibua mengi maana kila kukicha utasikia hiki kimebadilishwa. Sasa mi cjui huyu mtu kuja kwake kunaisaidia nn taifa yetu.


Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Ujio wa Rais wa Marekani unaweza kubaki kuwa ni kumbukumbu kubwa kwetu kama nilichokiona jana, yaani kubadilika kwa muonekano wa Bendera ya Taifa; kutakuwa kumesababishwa na ujio wa Rais Barack Obama!!

Barabara ya Julius Nyerere inayotoka Uwanja wa Ndege atakapopita Rais huyo kumepambwa bendera zinazofanana fanana na Baendera yetu ya Taifa la Tanzania niliyoizoea.

Naomba Watalaam wa mambo ya uraia na wazalendo wa nchi hii, mnijulishe kilichotokea mpaka bendera ikibadilishwa au ni kitu gani kinacho sababisha bendera ibadilishwe!

Naomba mnijuze ni chombo gani chenye mamlaka ya kubadilisha bendera ya taifa na hatua zipi zinazofuatwa mpaka Bendera ikabadilishwa!

Nilicho kiona kwenye bendera ya sasa ni kuufanya mchirizi mweusi unaokatiza kutoka ncha moja kwenda nyingine kufanywa mkubwa sana na kuifanya rangi hiyo kuwa dorminant kwenye bendera yetu, kinyume na Bendera ya zamani.

Siku zote huwa naamini kuwa Bendera ya Taifa ni tunu na Alama yetu ambayo ina vipimo halisi na haiwezi kuwa inachezewa chezewa!

Kama kuna mtu alipewa tenda ya kutengeneza bendera za Taifa kwa ajili ya ujio wa Obama na badala yake akatuletea bendera iliyobadilishwa bila kufuata utaratibu wa kubadilisha Bendera ya Taifa; Naomba asilipwe na achukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu.

Maskauti wa Nchi wa sasa, mnaona kama mambo yako sawa na bendera yetu?
ungeweka picha tungekuelewa unakuja na manene miiiiiiingi ambayo haivunji mfupa
 
bendera iliyochakachuliwa.jpg Hii ni Bendera mpya ya Taifa
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom